Pre GE2025 CCM wanatengeneza "elite clique"?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tulishasema hapa ccm ya kisasa ni ya watu 500-700 na koo zao, nani anamjua mwashamba? Yeye akae kutwa kucha jf kusifia kwa magazeti yake akitupiwa kifurushi na chipsi dume siku inaenda ila elites wanakwenda na ethnic groups zao! Wengine watawaimbia mapambio tu na kuvalishwa kijani km mbwa wa kizungu
 
Hawajielewi😃😀😆
 
Nakuunga mkono yote kwa maneno yako mazuri na yenye busara. Kwa taarifa yake ni kwamba kuna teuzi zimefanywa na mama ya watu wa vijijini huko ambao hawana majina wala familia zao hazijulikani popote. Fanya kazi utaonekana tu.
 
Ccm ni mchwa, hawashibi
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Nimewaza kuwa kama Dr. Emmanuel Nchimbi akifanikiwa kuwa Makamo wa Rais na baadae kuwa Rais wa Tanzania, nini kitazuia Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri Mkuu wakati huo?
Kwanini asiwe kama ana uwezo?.
Mtoto wa Mwigulu Nchemba, huko mbele ya safari si ndiyo anatayarishwa kurithi ubunge wa baba yake?
Kuna ubaya gani?.
Mifano ni mingi itoshe tu kusema kuwa ndani ya CCM kunatengenezwa kizazi Cha kisultani ambacho bila kuwa sehemu yake ama kukubaliwa na wao, itakuwa ni ngumu kwa mtu mwingine nje ya koo hizo teule ndani ya CCM, kuwa kiongozi.
Sii kweli!. Posts ni nyingi sana, hata viongozi wote wakileta wake zao na watoto wao, posts, zitakuwa bado zipo!.

Hakuna ubaya wowote, as long as wana karama ya uongozi na wana uwezo.
P
 
Kwanini asiwe kama ana uwezo?.

Kuna ubaya gani?.

Sii kweli!. Posts ni nyingi sana, hata viongozi wote wakileta wake zao na watoto wao, posts, zitakuwa bado zipo!.

Hakuna ubaya wowote, as long as wana karama ya uongozi na wana uwezo.
P
Pasco ukitaka kupindisha hii hoja (twist ) unachofanya ni kutaja wingi bila kugusia hata kidogo ubora.

Nani kiongozi anayewaza mtoto wake ateuliwe kuwa Katibu tarafa?

Yaani kiongozi anayelipia Dola zaidi ya 30, 000 (Karibia 78,000,000) Kwa shule ya "international" kama anavyosema LIKUD anasubiria mtoto wake ateuliwe kuwa DAS?
 

Katika mchakato wa uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika idadi ya wajumbe wanaoshiriki katika kura za maoni kwa wagombea wa diwani na mbunge. Katika ngazi ya kata, idadi ya wajumbe imeongezeka kutoka 150 hadi zaidi ya 1000. Haya ni mabadiliko makubwa yanayoashiria mwelekeo wa chama katika kujenga uwakilishi mpana wa wanachama.

Kwa upande wa uchaguzi wa mbunge, wajumbe wa kura za maoni sasa wameshikilia idadi ya zaidi ya 600, wakitokea kwenye jumla ya 9,000. Hii inaonyesha kuwa chama kinajaribu kuongeza uwakilishi wa wanachama katika mchakato wa uchaguzi, ingawa bado kuna maswali mengi kuhusu uhalali na ufanisi wa mchakato huu.

Licha ya ongezeko hili la wajumbe, kumekuwepo na ukosefu wa uwazi katika uchaguzi wa nafasi za uongozi za juu ndani ya chama. Hakuna wajumbe wanaoshiriki katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama Taifa wala Makamu Mwenyekiti Taifa. Badala yake, inasemekana kwamba wanachama wanapigiwa kura jina moja tu, jambo ambalo linaweza kuashiria kukosekana kwa ushindani wa kweli na demokrasia ndani ya chama.

Maswali haya yanahusiana moja kwa moja na dhana ya demokrasia ndani ya CCM. Je, ni kweli kwamba chama kinatoa nafasi sawa kwa wanachama wote katika mchakato wa uchaguzi? Au kuna nguvu fulani zinazodhibiti mchakato huu ili kuhakikisha kuwa watu fulani wanabaki madarakani? Hii ni changamoto kubwa ambayo inahitaji kujadiliwa kwa kina na kupewa ufumbuzi.

Wakati ambapo wajumbe wanapaswa kuwa na sauti katika mchakato wa uchaguzi, ni muhimu kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata nafasi ya kutoa maoni na kuchagua viongozi wanaowakilisha maslahi yao. Katika hali hii, ni dhahiri kwamba kuna mapungufu katika mchakato wa uchaguzi wa ndani wa CCM, ambayo yanahitaji kuboreshwa ili kuhakikisha kuwa demokrasia inachukua nafasi yake.

Katika kuendeleza demokrasia, ni muhimu kwa vyama vya siasa kuzingatia maoni ya wanachama wao na kuwapa nafasi ya kushiriki katika maamuzi muhimu. Hii itasaidia kujenga chama chenye nguvu na chenye uwakilishi wa kweli. Wanachama wanapaswa kuwa na uhakika kwamba sauti zao zinaheshimiwa na zinachukuliwa kwa uzito.

Kwa kumalizia, mchakato wa uchaguzi wa ndani wa CCM unakabiliwa na changamoto nyingi za kimaadili na kiutawala. Ongezeko la idadi ya wajumbe wa kura za maoni ni hatua nzuri, lakini inahitaji kuandamana na mabadiliko ya kweli katika mfumo wa uchaguzi. Kwa hakika, demokrasia inapaswa kuwa msingi wa kila mchakato wa uchaguzi, na ni jukumu la kila mwanachama kuhakikisha kuwa hii inatendeka. Ni muhimu kwa CCM kuangalia ndani yake na kufanya marekebisho yanayohitajika ili kuimarisha demokrasia na uwakilishi wa wanachama wake.
 
Kwa kutumia neno "elite clique" kwa CCM umekosea.

Kwa tafsiri hicho ni kikundi cha watu ambao wana lengo moja na huwa hawamkaribishi mtu mwingine asie na mawazo kama yao. Hivyo kwa CCM au hata Chadema hawako hivyo kwani wana watu wa aina zote iwe wanachama au wafuasi.

Neno hilo hutumika sana kwenye sayansi ya jamii ambapo watu wenye tabia fulani na mawazo sawa hutengeneza mtandao (Network) na mifano yao ni kama vile kwenye freemason, illuminati na makundi mengine.

Maneno ulopaswa kutumia ni kama vile "Nepotism" (upendeleo) ambapo watu wa kundi moja kama la familia hutumia nafasi zao ( kwa mfano ulotoa wa familia ya Kikwete) ndani ya CCM na serikali kujinufaisha binafsi.

Hivyo tumeona familia hizo zazidi kujikita ndani ya chama kwa kisingizio cha waanzilishi au wenye chama.

Lakini neno linofaa kutumia kwa ulivyokusudia ni neno "Factionalism" (kutengenezwa vikundi) yaani kwaibuka kikundi kidogo kutoka ndani ya kundi kubwa ndani ya chama kwa malengo kama hayo kujichukulia maamuzi ya kuyafanya maamuzi hayo kuwa ndo msimamo wa wengi .

Mfano hai tunao na tumeona Adam Kimbisa akitoa hoja (kutoka kwenye kakikundi) kwamba mwenyekiti awe mgombea wa chama wa uraisi na baadae mzee JK akakazia kuwa ndo hivyohivyo.

Na mfano mwingine wa Factionalism ni kuundwa kwa "Sukuma Gang" ndani ya CCM kikitetea maslahi ya kanda ya Ziwa huku yule mbunge maarufu akitumika kama chambo, na vikundi vingine kama "2030-2035"

Hivyo basi kutokana na hayo hapo juu basi twaweza kuthibitisha kwamba ndani ya CCM sasa kuna mambo kama "Nepotism" na "Factionalism" kwa kuzingatia mifano niliyotoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…