Pre GE2025 CCM wanatengeneza "elite clique"?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
sasa kama cha siasa hawajui hata wanako elekea , huo si ni sawa na uganga au ushirikina tu gentleman? 🐒
Wewe ndiye uliyeuliza " Sasa unadhani watafika wapi?" ndipo Mimi nikakuuliza kwani wanakwenda wapi?

Usiilaze akili yako kama yule Mzee aliyesinzia kwenye Kaburi la Mwalimu Nyerere.
 
Wewe ndiye uliyeuliza " Sasa unadhani watafika wapi?" ndipo Mimi nikakuuliza kwani wanakwenda wapi?

Usiilaze akili yako kama yule Mzee aliyesinzia kwenye Kaburi la Mwalimu Nyerere.
vyama vya siasa na wanachama wao wasio na maono wala kujua wanaelekea wapi,

huishia kunung'unika na kulaumu vyama vyenye malengo na mipango mikakati madhubuti ya kujizatiti kwenye malengo yao ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu, manung'uniko ambayo hayana athari zozote kisiasa 🐒
 
UZURI MUNGU HUWA YUPO. HUYU BABU WA MSOGA SI KITAMBO ATAREJEA KWA MUUMBA. TUONE HZ TKTK ALIZOANDAA ZITAKWENDA WP?
Hii habari ya Mungu yupo ndiyo upuuzi wenywewe. Mungu ni wa wote, hata hao tunaowalalamikia.
Muhimu ni kupambana kwa kutumia akili aliyotupa Mungu kwa ushirikiano na wengine.
Mungu ni wa wote, tupambane kwa haki na Mungu ataamua kwa haki ya pande zote. .
 
You are right Allen Kilewella.

Artificial Intelligence Descriptive Overview elaborates that.
"..An elite clique is a small, exclusive group of people who are considered to be elite. Shared interests, views, or purposes often characterize cliques. They can also be exclusive, thinking they are better than the others and may use manipulation to maintain their status.."

This dirty game started in 2005, but the trend was about to be reversed in 2016-2020, after which it has regained its mission to make it deceptively endorsed by the sleeping pumpkin.
 
Chalamila nae yumo???
 
Kwa nini umechelewa kuwaza na kuligundua jambo lililo wazi kitambo sana hili?

Wanakufa watu, lakini majina yao kwenye ofisi za umma hayafi na ndiyo yanayowabeba kushika nafasi hizo.

Nyerere alikufa, lakini jina lake kwenye ofisi za umma lipo, linaendelea kudunda.

Mwinyi kafa, lakini jina lake linaendelea kuwepo ofisi kubwa.

Walio hai, washastaafu lakini majina yao bado yamekamata nyadhifa kubwa za ukwasi.

Wasiojua madhara yatokanayo na mfumo huu hawawezi kueleza chochote cha maana zaidi ya ngebe za umimi na ubinafsi.
 
Hujamuelewa mleta uzi. Amexungumzia nafasi za juu ambazo ndio zenye maamuzi makuu. Unatoa mfano wa George Bush family Marekani, ndio sultan kama huo mtoa mmada anauzungumzia! Mnafikiri kule wamarMarekani wanabadilishana? Eti mtu wa kawaida tu anaweza kuwa Rais, ni vikundi vya watu, familia na matajiri wachache tu wanaotawala. Huku kwetu pia tunaelekea huko labda atokee kiongozi ndani ya ccm akemee baadhi ya mambo, simuoni kwa sasa, amebaki JMK tu ambae tumeona anashinikiza katiba ivunjwe then tufanye mabadiliko baadae!!
 
Wewe hutakaa uwe na akili milele
 
itoshe tu kusema kuwa ndani ya CCM kunatengenezwa kizazi Cha kisultani ambacho bila kuwa sehemu yake ama kukubaliwa na wao, itakuwa ni ngumu kwa mtu mwingine nje ya koo hizo teule ndani ya CCM, kuwa kiongozi.

Upo sahihi na hivyo ndivyo inavyokuwa kwenye uongozi wa nchi, huwa wanakuwa wamekula yamini ya kupeana vijiti...
 
Tunaposema kuna haja kazi za serikali ziwe za mikataba ya miaka mitano mitano muwe mnaelewa. Maslahi yaboreshwe watu wapewe mitaji kupitia mikataba ya miaka mitano hio. Upon end of Contract mtu alipwe stahiki zake zote hata kama ni million 100 apewe alale zake mbele.

Kwa style hii ya mtu kukaa ofisini miaka 60 halafu akimaliza anatafta namna ya kuwapachika na watoto wake kwa mgongo wa chama hatuwezi fika. Watu wawezeshwe kwa mikataba mifupi. Ukimaliza utafte namna ya kujiajiri. Hivyo ndio tutajenga uchumi wa kila mmoja wetu. Kila mtu atapata nafasi ya kufaidi keki ya taifa.

Vijana watatoka kazini wakiwa na nguvu na mitaji ya kufanya mambo makubwa.
 
Hivi chadema hoja zenu ni zipo haswa?!!!!!! Mbona kelele Sasa?
Ulaya kulikuwa na malkia mmoja alikuwa mjinga hivi. Aliulza ni kwa nini watu wa nchi yake wanaandamana, wasaidizi wake wakamwambia ni kwa kuwa hawana mikate. Yule malkia mjinga akajibu kirahisi tu, "si wale keki?"

Ujinga hauna kwao kila mahali upo.
 
Chama kile kina mizizi iliojichimbia chini sana🤣,,, hao watoto ndio at some point watatumia ile kauli ya "Babaangu alikipigania chama sana, hivyo naomba mwanangu nae apewe shea kwenye keki ya taifa."
Hiki ulichoandika kilikuwepo Bangladesh hadi Waziri wake Mkuu Sheikha Hasina alipofurushwa mwaka jana kwa sababu hiyo hiyo.

Wao Bangladesh walienda mbali waliweka kwenye sheria zao za nchi kuwa ni lazima watoto wa viongozi waliopigania uhuru watengewe ajira kwa asilimia 5 kwa ya ajira zote zinazopatikana nchini humo. Hata hapa CCM wanaweza kuweka huo utaratibu maana wameonesha kwa vitendo tayari kuwa huwezi kupata kazi kama wewe siyo mwanachama wa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…