CCM wang’ang’ania Serikali mbili katika Katiba Mpya

CCM wang’ang’ania Serikali mbili katika Katiba Mpya

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
666
Reaction score
426
Dodoma. Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika hatua ya rasimu na watu mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa wakitoa maoni yao.

Tayari Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa chama hicho kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na kupata nafasi ya kuichambua, kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ilitolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Habari za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na kuyatolea uamuzi.

Hata hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo zitatangazwa katika siku iliyopangwa.

Mmoja wa watoa habari alilieleza gazeti hili kuwa uamuzi uliotolewa na kamati hiyo, utawasilishwa kwa wanachama wake kwa utaratibu uliopangwa na kwamba wabunge wa CCM wataelezwa katika kikao chao kitakachofanyika keshokutwa Jumamosi katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.

“Sisi wabunge tunategemea kuelezwa uamuzi wa CC katika kikao chetu cha Jumamosi, tumeambiwa kikao hicho ni muhimu na tuhudhurie bila kukosa,” kilieleza chanzo hicho jana jioni.

Habari zaidi zilisema wakuu wote wa mikoa na wilaya tayari wapo mjini Dodoma na kwamba watakutana na Waziri Mkuu katika mkutano wa kichama uliopangwa kufanyika jana usiku.

Zinapasha kuwa katika mkutano huo uliotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Dodoma, MaRC na MaDc hao wataelezwa mkakati na msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya

source: mwananchi
 
Huo ni mchezo tu ambao tumeshaujua!lengo kupoteza muda na mipesa ya walipa kodi!Warioba amepelekewa mchezo mzima na yeye amekubali!wanajua serikali 3 haitafanya kazi kabisa ,Muungano utavunjika dakika 2 ,na tumesahau Warioba ni mfuasi mkubwa sana wa JKN.hawezi kukubali aandikwe kwenye vitabu vya historia kuwa alipendekeza na kuandikia serikari 3 na Muungano ukavunjika!Haiwezekani!sio Warioba yule alielelewa na JKN.

Hivyo wanapoteza muda ijadiliwe kwa muda mrefu ionekane serikali 3 imeshindikana!irudishwe upya kwenye tume mchakato wa rasimu mpya ya serikali 2 uanze tena!itoke rasimu mpya.....!!Lengo kuwazima midomo wazanzibar na watanganyika ....

Pia kumuongezea miaka 2 JK ili katiba ya serikali 2 imalizike na itoke katiba ya serikali 2.....
 
Well..wamesimamia sera yao..sioni tatizo. Si lazima kila mtu aku ali serikali tatu. Tupo na sisi wengine tunaoamini serikali moja mifumo mbalimbali.
 
Wanataka wanzanzibar waanze kujiripua kwa kuupinga muungano dhaifu then wawapige kwa propaganda ya udini

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Msimamo huo umefanywa na kamati kuu ya chama hicho katika kikao chake mjini Dodoma jana.

Habari zaidi zilisema wakuu wote wa mikoa na wilaya tayari wapo mjini Dodoma na kwamba watakutana na Waziri Mkuu katika mkutano wa kichama uliopangwa kufanyika jana usiku.

Zinapasha kuwa katika mkutano huo uliotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Dodoma, MaRC na MaDc hao wataelezwa mkakati na msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.

NAOMBA UFAFANUZI!!

Hawa maRC na MaDC wanahusikaje kwenye masuala ya CCM?

Na KATIBA ya JMT imewapa majukumu gani katika JMT?

Je kuna uhalali wa KIKATIBA viongozi hawa kuitumikia CCM?

Kwa vile kisheria wana nguvu ya ushawishi, katiba mpya si itakuwa ni ya CCM na si ya JMT?
 
Back
Top Bottom