Mkuu 'Brazaj', naiona mada yako hii kuwa ni juhudi tu za kutafuta michango ya mawazo ni nini hasa wanachotakiwa kufanya CHADEMA ili kukomesha uharamia wa CCM kubaki madarakani.Kujipanga kwa ushindi katika hali yoyote nako hakuwezi kuwa impossible.
Hata hivyo itataka kusugua vichwa kweli kweli.
CHADEMA kama chama cha siasa, sioni chochote wanachoweza kunufaika nacho kwa kususia uchaguzi wowote tokea hapa kwenda mbele.
Mchango wangu katika hili ni kuwa, CHADEMA ni lazima wawe tayari kabisa kuweka wagombea wao katika nafasi zote za uchaguzi, bila kukosa hata moja, toka ngazi ya shina hadi juu kabisa. Kazi ya kuwaandaa watu hawa ni sasa hivi, wakati huu na siyo baadae. Mgombea yeyote kuenguliwa katika nafasi ya kugombea kwa sababu za kizembe au hila za CCM kama ilivyokuwa huko nyuma iwe ni mwiko kabisa. Na hili lisiwe swala la kujaza nafasi za wagombea tu, ni lazima wawe wagombea wenye sifa na uwezo wa kuongoza.
Pili, umegusia swala na "wenye vifua", nikidhani una maana ya "matumizi ya nguvu za Dola" katika uharamia wa CCM kuchafua chaguzi. Hili tulishalijadili huko nyuma, kama unakumbuka.
Huu ni "uhalifu" wanaofanya CCM, na wananchi wanajua ni uhalifu, ila hawana uongozi unaowaweka pamoja kuukataa uhalifu huo. Kazi iliyopo na ambayo ingepashwa iwe tayari inafanyika, ni kwa CHADEMA kuweka mikakati ya kuukataa uvunjaji huu wa sheria.
CHADEMA wanatakiwa kuzijua njia zote zinazotumika katika uhalifu huo, na kuandaa mipango ya kuizuia katika kila ngazi.
Siyo kazi ngumu kujua wanayofanya CCM. Kwa mfano, angalia tu sasa hivi wanavyojipanga kutumia njia zilezile! Umeangalia hizi ziara za hivi karibuni za Mwenyekiti wa Chama hicho, akitumia kofia ya URais wake? Soma vizuri mikusanyiko hiyo na mbinu zote tokea huko. Huyo huyo Mwenyekiti, anaunda serikali yenye madhumuni yaleyale wakati wa chaguzi zinazokuja. Kwa nini CHADEMA wasiyasome yote haya na kuyaelewa vizuri, na kujiandaa kuyaaangusha?
CCM hawana njia mpya watakazozitegemea kubaki madarakani, na mbaya zaidi kwao, hata hali ya kisiasa ya kawaida tu haiwapi nafuu yoyote, sasa CHADEMA watashindwa vipi kupambana na hawa majambazi?