MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Leo katika kipindi cha Jahazi cha redio clouds mtangazaji Kibonde amesema CCM imepata wabunge 10 waliopopita bila kupingwa katika majimbo 10 nchini. leo ndio siku ya kwanza ya kampeni je wapinzani watafika salama. Hii ni ishara kwamba CCM bado ina nguvu kwani sio jambo la kawaida kwa vyama vya siasa 18 nchini kushindwa kutoa upinzani wa kweli. Mwalimu Nyerere alishasema hakuna haja ya kukimbilia Ikulu kabla ya kuimarisha chama ngazi ya chini. Chadema kinaonekana kupyaya kwa kuwa ndicho kinaonekana kuwa na nafuu lakini kimefungwa 10 kwa 0 siku ya kwanza ya kampeni. Hii ni ishara ya ushindi wa kishindo kwa CCM ifikapo 2010.