hamuoni hata aibu wajameni?, elfu 70 kweli?.Shika adabu yako...!
natumaini hiyo Idodi ipo chini ya ZZM kama sio CCM, kwanini sasa msiangalie vyama vingine vimetoa nini, onyesheni mfano kwa vyama vingine!Kwani kidogo hiyo? Hivyo vyama vingine vimetoa nini?
Yeye alisimama kama mwenyekiti wa CCM mkoa na kuiwakilisha CCM taifa kuwa wanatoa 70,000/= dah inauma sana mkuu NL.
Tukiwa bado tuna majonzi kwa wanafunzi walio ungua moto bwenini shule ya sec. Idodi, CCM wametoa mkono wa pole 70,000/= ametangaza mwenyekiti wa CCM Mkoa Iringa Jah People huku shule ya msingi Idodi wametoa 500,000/=.
Mheshimiwa Lukuvi ametoa 1,200,000/=
Mheshimiwa Prof.Msola ametoa 500,000/=
Mheshimiwa Anna Makinda ametoa 100,000/=
Walio bakia wamechangia na kufikia 500,000/=
The more Dataz
--Mh.Lukuvi amewaambia wananchi wake wasisumbuke kuanza kufyatua tofali ameaidi kutoa mil.10 kwa ajili ya ukarabati wa bweni.
--Mmiliki wa mabus ya Upendo ya Dar-Iringa na Dar-Njombe ambaye ni diwani wa Idodi aliahilisha safari za Dar na kubeba waombelezaji toka Iringa mjini kwenda Idodi kuhudhuria mazishi.
Respect wakuu
Nawakilisha.
Je, anarudishiaje fadhila kwa customers wake? Hiyo ilikuwa ni venue nzuri sana ya kuonyesha anajali wateja wake yeye kama yeye.....!
CCM inawezekana mtoa habari amesahau baadhi ya sifuri mbele jamani . Kwani Idodi ina wakazi wangapi? na wangapi wanategemea kupiga kura mwakani na je hali ya upinzani ikoje pale Idodi ?
yah, kuna kaka yangu yuko huko iringa na alikuwepo mazishini, ni kweli mafisadi wametoa mkono wa pole 70,000 bila senti.
Naona alie rudisha fadhila kidogo ni mmiliki wa mabus ya Upendo yeye alihailisha safari za Dar na kubeba waombelezaji kupeleka msibani Idodi lakini Jah unajua tena huyu ni Mkinga dah bahili sana
FYI wakati uchaguzi wa sisiem wa mwaka 2007 uliowaingiza kina Jah madarakani nilikuwa Njombe na uchaguzi wa mkoa wa IR ulifanyika Njombe....!
Hehehe mkuu hiyo ndo pesa chama chako kimetoa kama pole kwa wafiwa yaani ubani.
Wacha nirudishe kadi mkuu!
Tukiacha hilo, je, ndo kusema hawajaguswa kabisa na huu msiba, yaani ni kitu cha kawaida kwao,
so hiyo 10million aliyotoa lukuvi kama sikosei ni bora wahakikishe hawarudishi mfumo wa zamani
Mkuu siasa za mkoa wa IR ni ngumu sana wakikukataa wanachama ndo basi tena hata aje JK kukupigia kampeni wanakutosa kama walivyo mtosa Mangula lakini unajua viongozi wengi waliopo kwenye system wa Mkoa wa Iringa wanasahau sana nyumbani ndo maana wanaamua kuweka watu wanao wapenda wao angalia mfano Mangula walimuuliza swali dogo tu wakati akiwa kama Katibu mkuu wa CCM taifa aliufanyia nini Mkoa wa Iringa jamaa blah blah kibao huwezi amini Mangula hajawahi mtoa MwanaIringa yoyote yule basi wakamtosa mpaka leo hii kafulia analima viazi Njombe. Hali kadharika Katibu mkuu Kiongozi Luhanjo ni wa Iringa lakini hajafanya mchango wowote ule katika mkoa wake unategemea huyu akigombea uongozi asimame na Jah people watampitisha nani si Jah atapita hata kama Kilaza. Angalia mfano mzuri wa Anna Makinda amekuwepo bungeni zaidi ya miaka 20 lakini ameshindwa hata kujenga daraja la kwenda kwa mama ake mzazi Njombe viongozi wengi wa Iringa wanajisahau sana na wanasahau nyumbani wananchi wanapo amua kuwatosa na kuwaweka vilaza nafikiri ndo wanaona ndo uamuzi sahihi maana wasomi bla bla kibao alafu wanaondoka wanaonekana kipindi cha uchaguzi.
Lakini mkuu hii challenge na sisi young generation inatakiwa tuichukue na tuanze kuaction now......tayari mi nimeanza on my side kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wangu....vipi mkuu huko?!
Yeah mkuu hata mimi nimeanza kujitengenezea mazingira lakini najaribu kumshawishi Geoff agombee Makambako ambwage Makweta kwa kupitia CHADEMA anaogopa kulogwa eti dah na jamaa pale anakubalika wanamfahamu wengi tumpe moyo jamaa agombee 2010.
Fidel, naona umeshikia bango mkono wa CCM... wewe umetoa ngapi vile..?