CCM ya Baba na Mama kumbukeni hili

CCM ya Baba na Mama kumbukeni hili

Malcom Sr

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2021
Posts
1,163
Reaction score
1,647
Wakuu,

Tusameheane tu nimekulia nyumba ambayo baba, Mama, Bibi na Babu wote kwa ujumla na rejareja ni CCM.

Ukweli mchungu CCM HAIJADHAMIRIA kutuletea maendeleo ya kweli watu wa kusini, ukiangalia nguvu inayotumika awamu hii kuwekeza Kanda Kanda ya ziwa na kaskazini ni dhahiri mmetuona watu wa kusini hamnazo.

Na kwamba muda wa kuomba kura mnaamini huku kusini mtapata kiulaini. Sasa CCM yangu ya Urithi kumbukeni kuwa.

Rais ametembelea huko kanda pendwa na kutoa mabilioni

Katibu mkuu na mwenezi wake wanapita huko kukagua Miradi lukuki iliachwa na Bwana Yule.

Huku Lindi, Ruvuma, na Mtwara tunajua mtakuja kipindi cha kuomba kura tu hakuna jipya.

Huku hakuna kitu kikubwa mlichokuja kutuwekea kuanzia maji, barabara, umeme na elimu chakavu sambamba na uhaba wa walimu.

Nikiri wazi tu CCM haiwekezi kusini kwasababu inajua itapata kura tu. Sasa tambueni wapiga kura wa mwaka 2010 sio wale watakaopiga kura 2025.

Labda muendeleze ilani ya Baba yetu ya kupita bila kupingwa.

Nyie viongozi wa CCM endeleeni kuwekeza nguvu hukohuko, sisi wananchi wa Mtambaswala tuacheni tuendelee kuteseka na msije mpk muda wa kampeni.

Mabilioni ya Maji yametolea Arusha, Mabilioni ya Mikopo yametolea Kilimanjaro, Mabilioni yanatembea huko Kanda ya Ziwa.

Mabilioni Tanga. Mabilioni Dar.

USSR
ETWEGE
KINUJU
JOHN BAPTIST
utunzeni huu Uzi

Maendeleo hayana Chama
 
Kumbuka sanduku la kura linafika hata kusiko pitika kusini wengi vilaza ndio mana wanatumiwa kama toilet pepa. Kanga na chumvi tu kwisha habari yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwani hakuna jinsi ya sisi watu wa kusini (Lindi Ruvuma Mtwara) tukajitenga na kuanzisha nchi yetu kama ERITRIA.?

nafsi inaniuma sana ninapoona miundombinu iliyopo kwenye mikoa mingine hasa kaskazini halafu nikalinganisha na hali iiyopo kwetu kusini.
 
Kwani hakuna jinsi ya sisi watu wa kusini (Lindi Ruvuma Mtwara) tukajitenga na kuanzisha nchi yetu kama ERITRIA.?

nafsi inaniuma sana ninapoona miundombinu iliyopo kwenye mikoa mingine hasa kaskazini halafu nikalinganisha na hali iiyopo kwetu kusini.
Kuna mzee wetu mmoja aliwahi kutoa hii hoja nafikiri Ni Mzee Nandonde Basi mzee Nyerere nasikia alimakaripia vikali...

Inaniuma Sana Mimi naona ahueni tupate utawala wa majimbo Mana hata wabunge wa kusini hamna kitu kabisa
 
Kumbuka sanduku la kura linafika hata kusiko pitika..kusini wengi vilaza ndio mana wanatumiwa kama toilet pepa..kanga na chumvi tu kwisha habari yao.

#MaendeleoHayanaChama
Ipo siku polisi haitawasaidia
 
Nyie jamaa mbona mnaenda mbali sana? Tatizo lenu wote tangu waliotangulia mnawaza na kuona kufika/kuishi dar ndio ndoto zenu badala ya Songea, lindi na Mtwara. Rejeeni kwenu mkuendeleze kufananefanane!
 
Kuna mzee wetu mmoja aliwahi kutoa hii hoja nafikiri Ni Mzee Nandonde Basi mzee Nyerere nasikia alimakaripia vikali...

Inaniuma Sana Mimi naona ahueni tupate utawala wa majimbo Mana hata wabunge wa kusini hamna kitu kabisa
Hawa Ghasia anasemaje?
Bungeni nilikuwa namuona kama kusini hakuna shida
 
Back
Top Bottom