VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
CCM ina msimamo wake rasmi juu ya Rasimu ya Katiba mpya.Msimamo huo unahusu hasa kupinga kwa nguvu zote uwepo wa Serikali Tatu. Msimamowa cahama chetu ni kutaka Serikali mbili. Si tatu kama Rasimu inavyopendekeza.
Pamoja na kutoa msimamo kichama,CCM inategemea makada wake walioko kwenye Tume ya Katiba iliyochini ya Jaji Joseph Sinde Warioba ili kuchukua msimamo huo wa chama kama'maoni ya wananchi wengi'. Mambo sasa ni tofauti. Wajumbe karibu wote wa Tume ya Warioba wanaupinga hadharani msimamo wa CCM-wa Serikali mbili na kutetea Serikali tatu.
Ningetarajia wengine wote waunge mkono 'usaliti' kwa chama lakini si Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi. Lakini jana,Prof.Kabudi,akiwa Kisarawe, amesema wazi kuwa Serikali tatu hazikwepeki. Naujua msimamo dhabiti wa Prof.Kabudi katika utetezi wa sera na misimamo ya chama na Serikali yake. Mfano wa hivi karibuni ni kuunga mkono katazo la mgombea huru katika kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila iliyokuwa na kuamuliwa na Mahakama ya Rufani Tanzania.
Huu wa jana ni mpya. Naye ameamua kuicha solemba CCM.Ameikatalia. Prof.Kabudi amesema kitu pekee kitakachosaidia kuwapo kwa maridhiano kati yetu kama watanzania ni Serikali tatu tu. Si vinginevyo. Baada ya hapo,Wajumbe karibu wote wa Baraza la Katiba Wilaya ya Kisarawe walikubaliana naye.
Wakabadili msimamo wao.Wakalaumu 'kulishwa kasa' kwa mambo muhimu kama haya;tena na chama tawala.Wajumbe hao wakaendelea kuchangia Rasimu kwa bashasha na utulivu.Wakauweka msimamo wa CCM kando. Wakaupuuza. Prof.Kabudi apaswa kwenda kwinginepo pia kuisambaratisha picha isiyovutia ya msimamo wa CCM.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam