Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kwa watu ambao walimsikiliza Rais Kikwete jana huko Mwanza alianza kutoa ahadi ambazo haziko katika Ilani ya CCM bali ziko katika Ilani ya Chadema. Nimebahatika kupitia Ilani zote mbili nikiwa ni mdau maalum wa demokrasia. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ni kuwa kwa kadiri Chadema wanaendelea kusua sua kutoa Ilani yao ambayo kama nilivyodokeza uko nyuma kuwa "inatisha" CCM toka J'pili wamekuwa wakiidadavua na kuanza kuingiza katika ahadi mbalimbali za Rais.
Ndani ya kampeni ya CCM ambapo mambo yale ambayo CCM hawakuyafikiria wanayarusha kwa kutumia hotuba za Rais ili Ilani ya Chadema itakapotoka (nadhani hadi J'mosi) CCM watadai kuwa mipango hiyo "ilikuwa tayari ndani ya ahadi zetu na Chadema ndio wameiiga)
Mbinu hii ambayo katika propaganda za siasa huitwa "political triangulation" imepangwa kutumiwa vizuri na CCM dhidi ya Chadema na hivyo kuneutralize mipango na kampeni ya Chadema.
Hata hivyo kucounter mipango hiyo ya CCM, Chadema nao wamefanyia marekebisho sehemu kidogo ya Ilani yao na hivyo kuikoleza munyu...
Tusubiri vitu... kabla hatujachelewa...