Mwanakijiji,
Chadema watabadili ILANI yao ili kukoleza MUNYU siyo? Hahahaaaaa.. (munyu=chumvi).
Nimekupata Ng'wana mbati......... Ngoja tuvute pumzi kusubiri Jumamosi.
Fanyeni juu chini, hotuba nzima iwe kwenye YOUTUBE.
Ingelikuwa heri, watengeneze FILM moja ikionyesha Slaa akielezea ILANI ya uchaguzi na kuweka vielelezo vya picha na film kwa yale anayoyaelezea. Kwa mfano akisema MAFISADI, basi wanaweka picha zao. Akielezea migodi, wanaweka picha za walioathirika. Akielezea kuuza mbuga, anaweka picha za Wamasaai wa Loliondo etc etc.. Hizi zinaweza kuwa VSD ili iwe bei rahisi kucopy na watu waruhusiwe kuzicopy na kugawia wenzao.
Yeah, CHADEMA inatakiwa waje na kampeni zenye ubunifu wa hali ya juu, ambazo sisiem hawawezi iga kabisa, wazo lako ni zuri na inawezekana kabisa kuweka Screen kubwa na kuelezea mikakati mbali mbali huku wakionyesha picha.
Kwa mfano, atakapo fafanua orodha ya mafisadi papa na nyangumi picha inakuwa Displayed .... kwa mfano kwenye tovuti ya chadema Mafisadi 11 wametajwa na picha zao zimeambatanishwa, http://www.chadema.or.tz/tamko/tamko.php?id=16&pg=110