Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Briefly More dataz kutoka CC, Dar:-
2. Kikao kwa kauli moja kimeamua kuwafuta wagombea wote wa uchaguzi wa uenyekiti wa UV-CCM kutoka bara, na kama alivyoomba rais kuwaachia nafasi hiyo wagombea watatu wa kutoka Visiwani.
3. Mwenyekiti wa kikao rais wa jamhuri, mapema aliomba kupitihswa kwa hoja, aksiema wka uchungu mkubwa sana kwamba kampeni za uchaguzi huo zilikwua zimeharibiwa sana na rushwa na hisia nzito zilizomhusisha hata mtoto wake, akaomba kuepusha mgawanyiko zaidi kwa kuwafuta wagombea wote wa kutoka bara, CC wameipitisha tayari.
- ...kuhusu Nape, CC imeamua kuukataaa kabisa uamuzi wa UV-CCM uliotolewa dhidi ya Nape, na kwamba rufaa yake itasikilizwa tena huko NEC, tarehe 8 na 9.
Mkuu,
Nina issues na hizi dataz.
Moja, kwani Umoja wa Vijana, kama ilivyo katika vyombo, vikao, na ngazi zingine za CCM, hawana utaratibu wa kuwa na viongozi tofauti kutoka bara na visiwani ? Itawezekanaje Rais ajiamulie kushauri eti wagombea wote watoke Zanzibar ?
Mbili, Kikwete amewezaje kutamka CCM kuna rushwa ? Hiyo kwake ni kukubali machafu ya chama tawala, na akitoa madai hayo anaweza kubanwa achukue hatua kwa kutumia ushahidi ambao atadaiwa, maana rushwa ni kosa la jinai. Kikwete atawezaje kweli kutangaza CCM kuna rushwa ?
Tatu, umetuambia kwamba CCM watasikiliza rufani ya Nape. Lakini hapo hapo umetoka kutuambia kwamba CCM wameshaamua, wameshapitisha kwamba ni Wazenji tu ndio watakaogombea. Hapo unaona pamekaa sawa kweli ?
Nne, Kikwete hawezi kumuongelea mtoto wake kwenye kikao cha Central Committee. Hususan kumuhusisha na rushwa. Ni kitu bizarre!!!
Tano, kuna thread ilianzishwa kabla inasema imekuwaje kikao cha CCM kimefanyika Ikulu. Wewe ukakimbia kutafuta "dataz" kali zaidi lakini zilipofika zikaonekana kama dead on arrival kwa sababu zilidai kikao kimefanyika Dodoma, hadi Wakuu kina Masatu walipokushtua. Ulichanganya vipi data hapo?
Unaona matatizo ya "dataz" zako ?
Sasa anza mashambulizi lakini I hope unaelewa kwa nini wengine huwa tunakataa kuzimeza nzima nzima.