Uchaguzi 2020 CCM yagawanyika Vunjo

Majasho

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2009
Posts
413
Reaction score
220
Mgombea wa ubunge kwa tiket ya CCM, Charles Kimei ana wakati mgumu kushinda jimbo hilo baada ya CCM kugawanyika, Inock Koola Zadock, mtoto wa Tajiri wa Kimarangu Mzee Koola (Mmiliki wa makampuni ya Zadock A1outdoor Africa), ambaye alishinda kura za maoni amegoma kuungana na kumpigia kampeni Charles Kimei na ameondoka zake kwenda Dar es Salaam bila hata kushiriki mkutano wowote wa Kimei.

Tumeona kwenye majimbo mengine walioshindwa kuonesha umoja ndani ya chama kwa kuungana na mshindi kumsindikiza kuchukua fomu na kumpigia kampeni kwenye mikutano ya Mbunge huyo lakini imekuwa tofauti Vunjo. Wale wana CCM waliokuwa wanamuunga mkono Koola wamegoma kumpigia kampeni Kimei.
 
Ungesema tu wale waliokula pesa za koola wamegoma kum support Kimei.
 
Hii Nayo Huwenda Ikawa PETTY ACCUSATIONS....

Tuwekee USHAHIDI!!
 
Simu moja tu ya Mwenyekiti ataenda Vunjo yeye na wakwe zake na wazazi wake na wahakikishe kimei anashinda
 
Baba yake na huyo chalii aliyemshinda Kimei kwenye kura za maoni(mwenye Co. Ya Zadock A1outdoor) alishagombana pia na bwn yule kipindi kile akiwa Boss mkuu wa mabarabara maana alipeleka kesi mahakamani iliyozuia Tanroads kuondoa mabango yote yaliyokua barabarani hivyo kusababisha kampeni ya mkuu ya kuondoa mabango barabarani kushindikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…