PreGE2025 CCM yaitaka Serikali kuzalisha ajira 350,000 kwa vijana nchini

PreGE2025 CCM yaitaka Serikali kuzalisha ajira 350,000 kwa vijana nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania Prof. Kitila Mkumbo amebainisha kuwa katika kulinda mafanikio makubwa yaliopatikana wakati wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25,katika kukuza uchumi jumuishi na kuimarisha ustawi wa wananchi wote, serikali imetakiwa kuchochea mapinduzi ya uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani utakaojengwa katika misingi wa kuongeza thamani rasilimali zinazozalishwa nchini.

Prof. Kitila amebainisha hayo leo Mei 30, 2025 kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma, wakati akiwasilisha muhtasari wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Mwaka 2025/30.

"Kipaumbele kingune ni kuongeza fursa za ajira kwa vijana, kuongeza kipato kwa wananchi na kupunguza umaskini,
Kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii, kuendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kukuza na kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Kipaumbele kingine ni kudumisha demokrasia na utawala bora, kuendelea kudumisha amani, utulivu na usalama,
Kudumisha utamaduni wa taifa, na kukuza sanaa na michezo; pamoja na Kuongeza kasi ya maendeleo vijijini."- amesema Prof. Kitila Mkumbo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM ya Mwaka 2025/30.
 
Jana mlituambia sio kazi ya serikali kutengeneza ajira
 
Vijana wenyewe
163192.jpg
 
Kutengeneza ajira hata 1m na zaidi inawezekana kwa serikali ya CCM kama Rais ataacha kutumia karamu kwa watendaji wabovu na kutumia Magereza kuwaonya.... huku akibadili katiba ya nchi kwa ajili ya kulinda Cake ya taifa kwa ajili ya kizazi kijacho...
 
Back
Top Bottom