Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:
1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)
2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)
3/Kutumia wabunge wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)
*SOURCE:Gazeti la Mwananchi
CCM. ndo chama tawala,kimepewa dhamana na wananchi hivyo pamoja na mambo mengine ni lazima kisimamie kwa ujasiri mkubwa maslahi ya taifa,,CCM inautazama mfumo wa serikali 3 kwamba utapelekea kuvunjika kwa muungano.jambo ambalo ni kweli, hivyo lazima kipinge kwa nguvu zote mfumo huo...kuhusu kutoa maoni ni kwamba wananchi wote,vyama vyote na taasisi na makundi mbalimbali ya wananchi yatapaswa kuipigia kura rasimu ya katiba,hivyo CCM ikifanya hivyo kitakuwa hakijavunja kanuni yoyote...HILO la wakuu wa wilaya na mikoa kuhusika kwenye mchakato ni la lazima maana wanasimama badala ya mkuu wa kaya in their areas of judisdiction
Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:
1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)
2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)
3/Kutumia wabunge wake wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)
*SOURCE:Gazeti la Mwananchi
Niliwahi kumsikia Nape akisema CCM haitaki kuwa pre-empty wanachama wao kuhusu rasimu ya katiba mpya na kwamba itawaachia wajadiliane katika mabaraza yao ili kupata muafaka!!
Sasa ni nini kimewatekenya hadi waanze kuweweseka na kuanza kutoa maelekezo kwa wanachama wao kwamba wapinge serikali tatu?!
Nape acha unafiki!!
Kiongozi!
Kama nimekuelewa basi inawezekana hujui unacho kitetea zaidi ya kutimiza wajibu wako wa kuwa MTWANA wa LUMUMBA. Ungekuwa unajuwa na kuelewa KATIBA ya JMT imewapa majukumu gani RCs na DCs usinge toka na kauli za wao kuwajibika kwa CCM. Ni kweli kwamba wana wajibika badala ya mkuu wa kaya, lakini sio kwa CCM.
Wapo Dodoma kupewa msimamo na maagizo kutoka kwa M/ Kiti wa CCM na sio kwa Mkuu wa Kaya.
Anyway, hatushangai kwani kila mTanganyika anajua kwamba sera ya kuandika KATIBA mpya haikuwa sera ya CCM ilikuwa ni sera ya CHADEMA. Na hata Waziri wa Sheria na Mwana Sheria Mkuu wa serikali alijiapiza kwamba hakuna haja wala ulazima wa kuandika KATIBA mpya. Hivyo yote yanayoendelea kuhusu KATIBA mpya, ni matokeo ya kuiga sera ambazo hazikuwa za CCM na kujikuta CCM inaji dhalilisha yenyewe mbele ya macho ya waTanganyika.
Kwa macho ya waTanganyika tunashuhudia kushindwa kwa kila ahadi iliyo ahidiwa na CCM kwa UMMA wa waTanganyika. Na ndio maana hata vile vipindi vya Lukuvi kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya NNE vimekufa, maana hakuna kitu ON THE GROUND.
Kauuli Mbiu: KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIIIII.....!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kiitikio: KIGUMUUUUU..........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Nape haaminiki, alisema watajivua gamba ndani ya siku 90, leo ni miaka gamba moja tu la igunga ndilo lililong'oka! Mengine yamemshinda!
Hakika wtz tuna kazi ngumu mpaka tupate katiba tunayoitaka! ila watawala waangalie wasije wakatufikisha kwenye machafuko!
Dawa ni kuingia vitani tu...tutwangane ndo tutakuja kupata katiba ya maana
Dawa iliyo kuu na tiba mbadala ya viini macho vya ccm ni kupata jeuri mmoja jwtz atufanyie kama yale ya Misri -1 kutufufulia Tanganyika yetu' 2 Kuwapa Zanzibar yao. 3 Kutuongoza kuandika katiba mpya itakayokuwa na manufaa kwa Watanganyika wote. Sababu ya kumtaka jeshi la wanachi Tanganyika huyo ni ugumu wa kupata katiba iliyo sahihi bila ya kupoteza rasilimali fedha nyingi zinazotumiwa na tume hatimaye kupata katiba ya pwagu na pwaguzi, kwa kuwa kama ccm wanaweza kuchukua jimbo kwa upande wa kanga na kofia watashindwa vp kuandika katiba kwa sahani ya pilau.....? Asilimia kubwa ya wajumbe wa mabaraza ya katiba ni wao kama si wote ondoa hao ma dc na rc......Sanduku la kura ni kujiangamiza...... Shime mwana jeshi la Tanganyika mmoja tuokoe.....!