CCM yajipanga 'Kuvuruga' Rasimu ya Katiba mpya

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
550
Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:

1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)

3/Kutumia wabunge wake wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)

*SOURCE:Gazeti la Mwananchi
 
Ijipange mara ngapi?inshort mawazo yaliyoko kwenye rasimu hiyo yaliyomengi yametoka kwao,sasa waliweka kwa makusudi issue ya serikali tatu ili mvutane hadi 2015 bila kuwa na katiba mpya waweze iba kura kama kawaida yao,kwahiyo watanzania hali ndo ilivyo believe me or not CCM wataendelea kuitafuna hii nchi hadi ibaki mifupa
 
Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:

1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)

3/Kutumia wabunge wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)

*SOURCE:Gazeti la Mwananchi

Niliwahi kumsikia Nape akisema CCM haitaki kuwa pre-empty wanachama wao kuhusu rasimu ya katiba mpya na kwamba itawaachia wajadiliane katika mabaraza yao ili kupata muafaka!!

Sasa ni nini kimewatekenya hadi waanze kuweweseka na kuanza kutoa maelekezo kwa wanachama wao kwamba wapinge serikali tatu?!

Nape acha unafiki!!
 
Muundo wa serikali ya muungano utaamuliwa na wananchi wote kwa ujumla wao na sio wanachama wa magamba peke yao!! A national refferandum on the structure of the Union will have to be carried out.
 
Sasa hapo ccm imevuruga wapi? Mbona mnapenda udaku sana?
 
Sioni dhambi au kosa kwa ccm kuwa baraza rasmi la katiba kwa sababu ccm ni taasisi kama taasisi zingine ambazo ni mabaraza ya katiba
 
Maoni ya watanzania kuhusu muundo wa muundo wa muungano yamegawanyika..wapo wanaotaka serikali moja, mbili,tatu,nne na tano. Msimamo na maoni ya ccm ni serikali mbili, ni haki yao kama watanzania
 
Sasa hapo ccm imevuruga wapi? Mbona mnapenda udaku sana?

1)Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

2)CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)

3)Kutumia wabunge wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)

*SOURCE:Gazeti la Mwananchi
 
Niliwahi kumsikia Nape akisema CCM haitaki kuwa pre-empty wanachama wao kuhusu rasimu ya katiba mpya na kwamba itawaachia wajadiliane katika mabaraza yao ili kupata muafaka!!

Sasa ni nini kimewatekenya hadi waanze kuweweseka na kuanza kutoa maelekezo kwa wanachama wao kwamba wapinge serikali tatu?!

Nape acha unafiki!!

Kiongozi!

Wamegundua kwamba huku mitaani hakuna kitu kinacho itwa WANACHAMA WA CCM, kuna wanao kula CCM na kulala CHADEMA. Kwa hali hiyo wameona ngoma itakuwa nzito wakiileta mtaani.

Mitaani waTanganyika wote ni CHADEMA watakuwa wamejimaliza kujiwekea wenyewekitanzi shingoni.

Ndio maana wameamua kuropoka wenyewe huko KITAANI Dodoma kinyume na ahadi yao ya kuipeleka rasimu ya katiba mpya ijadiliwe mitaani na kinachoitwa WANACHAMA WA CCM.

Sijui watakimbia vivuli vyao mpaka lini wakati 2015 ndiyo hiyoooo inakaribia!!!???
 
1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

Wanataka Serikali mbili kwa mfumo upi?

1. Tanganyika + Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

au

2. Tanzania(Jamhuri ya Muungano) + Zanzibar(SMZ)
 
Wakitaka Chama Cha Mauaji (CCM) 2 basi sisi Wazalendo tunataka Serikali 3 na Kama haiwezekani bora basi Muungano uvunjike
 
Hili la serikali tatu, hata mimi silitaki, kwa maana hiyo naungana na CCM kulipinga kwa nguvu zote!
 
CCM. ndo chama tawala,kimepewa dhamana na wananchi hivyo pamoja na mambo mengine ni lazima kisimamie kwa ujasiri mkubwa maslahi ya taifa,,CCM inautazama mfumo wa serikali 3 kwamba utapelekea kuvunjika kwa muungano.jambo ambalo ni kweli, hivyo lazima kipinge kwa nguvu zote mfumo huo...kuhusu kutoa maoni ni kwamba wananchi wote,vyama vyote na taasisi na makundi mbalimbali ya wananchi yatapaswa kuipigia kura rasimu ya katiba,hivyo CCM ikifanya hivyo kitakuwa hakijavunja kanuni yoyote...HILO la wakuu wa wilaya na mikoa kuhusika kwenye mchakato ni la lazima maana wanasimama badala ya mkuu wa kaya in their areas of judisdiction
 
kwa sasa hata tusipopata katiba mpy ila tukapata tume ya uchaguzi makini inatosha mengine tutafanya baadae make hapo ndo panakuja kuwa kikwazo
 
Muundo wa serikali ya muungano utaamuliwa na wananchi wote kwa ujumla wao na sio wanachama wa magamba peke yao!! A national refferandum on the structure of the Union will have to be carried out.

Nimewahi kusema na leo narudia ya kwamba wenye maamuzi ya kuwe na serikali mbili au tatu na muungano wa aina gani ni wananchi wa ZANZIBAR. CCM inayosema muundo wa serikali mbili ni hawa wa kutoka upande wa Tanganyika lakini sijamsikia hata kiongozi moja wa CCM kutoka Zanzibar akiunga mkono muundo wa serikali mbili. Ninawaomba CCM msilazimishe hoja ambayo dalili ya kukataliwa iko wazi kabisa. Hata hivyo kwani hata muungano usipokuwepo, wanadamu watafutika usoni mwa nchi hizi mbili. Muungano mzuri ni ule wa hiari na unaoamuliwa na wengi.
 
Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:

1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)

3/Kutumia wabunge wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)

*SOURCE:Gazeti la Mwananchi

Nimemuona na kumsikia mara kadhaa mjumbe wa baraza la wazazi ccm kutoka kisiwani Pemba aliyeambatana na alhaji Bulembo katika ziara zake huko mikoa ya kanda ya ziwa amekuwa mara zote akizungumzia uzuri wa serikali mbili na hatari ya kuvunjika muungano na kuparaganyika kwa zanzibar ikiwa kutakuwa na muungano wa serikali tatu. Hiyo tu ilitosha kuniambia kuwa ccm hawatakuwa tayari kubadilisha msimamo wao kutoka serikali mbili hadi tatu.
 
Wanataka Serikali mbili kwa mfumo upi?

1. Tanganyika + Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

au

2. Tanzania(Jamhuri ya Muungano) + Zanzibar(SMZ)
CCM wanataka mfumo uliopo uendelee, yaani Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya mapinduzi Zanzibar tu.
Hawataki kabisa kitu kinachoitwa serikali ya Tanganyika kwa gharama yoyote.
 
Kikao cha kamati kuu ya CCM chini ya mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete kimekaa kwa siri kwa siku mbili mjini Dodoma na kumaliza kikao chake jana na kutoa maadhimio yafuatayo kuhusu rasimu ya katiba mpya:

1/Kupinga kwa nguvu zote mfumo wa Serikali TATU uliopendekezwa kwenye rasimu hii(Wamesema msimamo rasmi wa CCM ni serikali MBILI)

2/CCM kuwa moja ya baraza rasmi ya Katiba.(Hivyo wanaCCM watakaa na kujadili na kisha kutoa mapendekezo yao ambayo yatachukuliwa na tume ya katiba kama maoni rasmi ya watanzania)

3/Kutumia wabunge wote, wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine wowote wa kiserikali kusimamia kwa nguvu zote maadhimio ya kamati kuu ya CCM juu ya rasimu ya Katiba mpya katika maeneo yao na taasisi zilizo chini yao(Tayari waziri mkuu alikuwa amepanga kuwa na kikao cha wabunge wote wa CCM pamoja na DC, na RC wote mjini Dodoma jana usiku)

*SOURCE:Gazeti la Mwananchi

Hawataweza, miti yote yatereza nyani lazima afe!

Wasi wasi wangu tu ni makamanda kuingiwa woga.
 
warumi 3:10-18
kama ilivyo andikwa:"hakuna hata mmoja aliye mwadilifu.
hakuna mwenye akili na kumfuata MUNGU.
wote wamepotea, wote wameharibika pamoja. hakuna mtenda mema hata mmoja
koo lao ni kaburi wazi, kwa ndimi zao hujipendekeza. wanasumu ya pili chini ya midomo yao.
vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
miguu yao iko njiani kumwaga damu..
maangamizi na taabu zimo njiani mwao.
njia ya amani hawaijui.
uchaji wa MUNGU haupo mbele ya macho yao"
 
Kama ndio hivyo basi hawajui aina ya Bomu wanalolitengeneza...maana kule Zanzibar tayari wananchi wa huko wameshaanza kuonesha wanaikubali rasimu ya sasa haswa kwa suala la Muungano.
Sasa kama CCM wakileta habari mpya zaidi ya hii ya sasa ya kwenye Rasimu, italeta mkanganyiko...

Back
Top Bottom