CCM Yamchagua Sitta kuwa mgombea pekee

CCM Yamchagua Sitta kuwa mgombea pekee

Tunataka bunge linalosimamiwa kwa kanuni bora na mwenyekiti wake awe "msimamiaji wa kanuni" na sio itikadi yake kisiasa.Suala la katiba ni la kisheria zaidi na si siasa.
 
Nakumbuka Bwana Sitta (the CA Chairperson to be - nominee by CCM) alikaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni. I remember vividly hakuwa rafiki wa upinzani kwa maana ya kujiepusha na mapenzi kwa CCM. Hakujali hoja iliyokuwa mezani hata kama ina mashiko as long as imetoka kwa upinzani, he was totally unfriendly. Ni majamnga tena bunge la katiba. asina imani naye! He was contrary to our expectations! Kama wadau mnakumbuka
 
binafsi huwa namkubali sana sitta,lakini ukiona ccm wanamshabikia mtu basi ujue kuna majanga hapo.kama wamekubali kumpitisha ki urahisi rahisi kiasi hicho then tutarajia majanga
 
Tuesday, March 4, 2014.
HabariLeo
View attachment 142577

Sifa ya kwanza imetajwa kuwa ni utayari wake katika kuliongoza Bunge hilo.
"Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,"
alinukuliwa Sitta akizungumzia nia yake.

Source: Tuesday, March 4, 2014.
Habari Leo.
Via : wavuti: CCM yamteua Sita kugombea Uenyekiti wa Bunge la Katiba

Wakuu kwanini hawa wanasiasa wanapenda sana kucheza na akili za Watanzania?

Ebu tujiulize hili swala la kupata katiba mpya ni ndoto ya Raisi Jakaya Mtoto wa Mrisho Kijukuu cha Kikwete? au ni msukumo na sera toka vyama vya upinzani hususani Chadema?

NB:
Siku zote mtu mwenye akili anapokusudia kudanganya na wadanganywa wakakubali kudanganywa, hudharau na kuwaona hamnazo.
 
Sasa ndiyo watu mtaona true colors za Sitta ...................... Makinda atakuwa afadhari. Kama kweli ni mzee wa viwango nafikiri issue ya Richmoduli ingeshakuwa history ................. Mzee ni manafiki!!
 
Ni kwa nini apitishe na Chama kwanza!? Maccm bana
 
genekai
Siku zote tunasema Chadema ni wapiga deal hamna jipya; wao waliwaza posho zaidi; katiba tulipaswa kuipigia kura moja kwa moja; watanzania tunafahamu tunahitaji kitu gani; upinzani mlishindwa kushinikiza hilo kwa njaa zenu sasa unalaumu nini?

Unasubiri wenye njaa ndo wapige kelele ww uliyeshiba uko nyuma ya keyboard, ww mbona haukupiga kelele badala yao?
 
Last edited by a moderator:
nyota njema huangaza mapema alfajir.. Kwa mzee sitta naona njia imeanza kunyooka nami namtakia safari njema.. Huu ndio mwelekeo wa 2015 njia imefunguka... mzee el upooooo na wapambe wako?
 
Mm huwa nampa benefit of daught.Anaweza kuharibu sana au kufanya vema sana.
Issue ya Richmond huwa simlaumu sana maana exciutive ilmzunguka na baadae kuishiwa pozi
 
Hivi ukiacha Mh Sitta, ni nani mwingine anaweza kutimiza vigezo vya nafasi hiyo?
 
@CHUAKACHARA - Nakubaliana kabisa na hoja hii. Mr. 6 is a wounded lion, atakachokifanya ni kutaka kurejesha imani yake kwa CCM. Na najua ili wampitishe na kumbwaga Mr. Vijisenti watakuwa amemfunda na hapo ndo kazi inapoanzia. Six anaweza kwa mbaya kuliko Ndugai na dada yake!
 
Unasubiri wenye njaa ndo wapige kelele ww uliyeshiba uko nyuma ya keyboard, ww mbona haukupiga kelele badala yao?

Nimepiga sana kelele; tatizo mungu wenu hapo chadema yupo kimaslahi zaidi
 
KAMATI ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi ( C C M ) imempitisha Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwa kauli moja kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Pia kamati hiyo imempitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo ya uongozi ya CCM iliyoketi jana, zimebainisha kuwa Andrew Chenge aliyekuwa akitajwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti, amejitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa hiari yake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kanuni za Bunge kupitishwa, utaratibu wa kuchukua fomu utatangazwa ambapo Sitta atakwenda kuchukua na atakuwa mgombea pekee kutoka CCM.
Kitakachosubiriwa ni kuona wagombea kutoka makundi mengine kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo na kundi linalotarajiwa ni kutoka vyama vya siasa vya upinzani.
Sifa za Sitta
Sifa ya kwanza imetajwa kuwa ni utayari wake katika kuliongoza Bunge hilo.
“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alinukuliwa Sitta akizungumzia nia yake.
Kisheria, sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni pamoja na kuwa na Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika, pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Sitta anatajwa kuwa na sifa za kushika nafasi hiyo, ikiwemo uzoefu wa miaka mitano wakati alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inaelezwa kuwa katika Bunge hilo la Tisa wakati akiwa Spika, mijadala mizito ilijadiliwa lakini hakutetereka hata kidogo. Waziri huyo pia amekuwa akitajwa na wapambe wake kuwa anafaa kuwania nafasi ya uenyekiti kwa sababu uadilifu wake hauna shaka.
Mbali na uadilifu na uzoefu wake katika uongozi wa Bunge aliloliita la kasi na viwango, inadaiwa hata makundi mengine, wakiwemo wabunge wa upinzani na asasi za kiraia, wanamkubali.
Mwenyewe Sitta aliwahi kunukuliwa akieleza sababu ya kukubaliwa na wabunge wa upinzani kuwa wanaamini akikalia kiti hicho, ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.
Sifa ya nyingine anazotajwa nazo, ni uwezo wa kutumia busara kukabiliana na makundi yenye maslahi mbalimbali na kuwaleta pamoja.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo tayari wanamuona Sitta kuwa mjumbe pekee mwenye uwezo huo, kutokana na uzoefu mdogo uliopatikana katika wiki mbili za Bunge hilo Dodoma.
 
Kweli watu hawana wema;
sitta aliubeba upinzani hadi akaonekana kama msaliti wa ccm,
leo hii mnamkana.
 
hata spika awe sitta au nani si tunachotaka katiba itakayoangalia maslah mapana ya Taifa
 
Attachments

  • 1393912902779.jpg
    1393912902779.jpg
    32.6 KB · Views: 48
Jiwe vs chenge=JIWE
Sitta vs safari=safari
 
ni jambo zuri kuwa na mwenyekiti Sitta kuliko chenge. lakini kinachonishangaza ni kwa nini ccm wamekaa na kumteua mtu wakati pale hawaendi kuwakilisha chama na wala hatuhitaji uanachama? wa nini isingekuwa ni hiari na utashi wa mtu kwenda kuchukua form na kugombea? Kuna mtu anayejua terms walizokubaliana ccm kama chama na sitta kama mwenyeiti mtarajiwa? I am confused kwa staili hii ya ccm kuendelea kuliteka bunge la katiba,

KAMATI ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi ( C C M ) imempitisha Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kwa kauli moja kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
Pia kamati hiyo imempitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo ya uongozi ya CCM iliyoketi jana, zimebainisha kuwa Andrew Chenge aliyekuwa akitajwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti, amejitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa hiari yake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kanuni za Bunge kupitishwa, utaratibu wa kuchukua fomu utatangazwa ambapo Sitta atakwenda kuchukua na atakuwa mgombea pekee kutoka CCM.
Kitakachosubiriwa ni kuona wagombea kutoka makundi mengine kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo na kundi linalotarajiwa ni kutoka vyama vya siasa vya upinzani.
Sifa za Sitta
Sifa ya kwanza imetajwa kuwa ni utayari wake katika kuliongoza Bunge hilo.
“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alinukuliwa Sitta akizungumzia nia yake.
Kisheria, sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni pamoja na kuwa na Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika, pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Sitta anatajwa kuwa na sifa za kushika nafasi hiyo, ikiwemo uzoefu wa miaka mitano wakati alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inaelezwa kuwa katika Bunge hilo la Tisa wakati akiwa Spika, mijadala mizito ilijadiliwa lakini hakutetereka hata kidogo. Waziri huyo pia amekuwa akitajwa na wapambe wake kuwa anafaa kuwania nafasi ya uenyekiti kwa sababu uadilifu wake hauna shaka.
Mbali na uadilifu na uzoefu wake katika uongozi wa Bunge aliloliita la kasi na viwango, inadaiwa hata makundi mengine, wakiwemo wabunge wa upinzani na asasi za kiraia, wanamkubali.
Mwenyewe Sitta aliwahi kunukuliwa akieleza sababu ya kukubaliwa na wabunge wa upinzani kuwa wanaamini akikalia kiti hicho, ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.
Sifa ya nyingine anazotajwa nazo, ni uwezo wa kutumia busara kukabiliana na makundi yenye maslahi mbalimbali na kuwaleta pamoja.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo tayari wanamuona Sitta kuwa mjumbe pekee mwenye uwezo huo, kutokana na uzoefu mdogo uliopatikana katika wiki mbili za Bunge hilo Dodoma.
 
swamweli sita ni muumini wa serikali tatu, kosa kubwa la kiufundi ccm wamefanya muungano kaburi liko wazi
 
Back
Top Bottom