CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,357
- 6,424
binafsi huwa namkubali sana sitta,lakini ukiona ccm wanamshabikia mtu basi ujue kuna majanga hapo.kama wamekubali kumpitisha ki urahisi rahisi kiasi hicho then tutarajia majanga
Huyu Sitta ni chui anayejifanya kondoo!
Ujenzi wa ofisi ya mwenyekiti wa bunge la katiba utaanza punde Urambo. ..
Sita kama hajui ni kuwa ametegwa ajimalize, ama ndani ya chama au kwa wananchi.
akitenda matakwa ya wananchi atakosa "indozmenti" ya chama muda muhimu ukifika, akikibeba chama atakosa "kredibilite" machoni pa wananchi jambo linaloweza kusababisha "kura zisitoshe" ikalazimisha mitulinga kujaribu (sijui kama itafaulu) kuokoa jahazi.
ccm wanazidi kujibana kwenye kona, wamebakisha mipasho tu, hoja kwishnehi.
ah ....mbona hakukaliki?
Mimi niliacha kumuamini pale alipopindisha ile issue ya Richmond mwishoni kabisa. Huyu ndiyo aliyezima lile sakata la Richmond licha ya kuliendesha bunge la tisa kwa umahiri mkubwa.
Mkuu huyu bwana ana nafuu fulani ila kwenye mambo mazito hawezi kukisaliti chama chake na washirika wake.
Kumbuka,katiba bora haiwezi kuwaacha vigogo wengi salama.
Hili siyo bunge la katiba mpya bali ni self enrichment scheme!! Kwa kusema ukweli ni mazingaombwe yanaendelea ............. nakubaliana na MKJJ kuwa kwa vile tumekubali kuingia kwenye huu mchakato basi tukubali na matokeo yake!!
Hapa hatuangalii individuals bali tunaangalia taifa ikiwa ni pamoja na wajukuu na vitukuu wako!hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo hivyo
Habari wadau,
Naomba tu kuwapa tahadhari wale wote wanaoshabikia kupitishwa kwa jina la Samweli Sitta kugombea uenyekiti waelewe tu kuwa huyu ni "CCM damu damu" na wasisahau kuwa "zimwi likujualo halikuli ukawisha".
Ni mara ngapi Sitta amekejeli upinzani ndani ya bunge hata wapinzani wanapokuwa na hoja za msingi?
Je,yeye Sitta,ni msafi sana ukilinganisha na wana -CCM wenzake?
Je,Sitta yuko tayari kuona CCM inapoteza dola?
Je,washirika wake wa kisiasa wote ni watu safi?
Mtu ambae angefaa kushika wadhifa huo,kwa maoni yangu, ni mtu mwenye sifa zinazotakiwa lakini ambae hakuwahi kuwa kwenye system.
Salary Slip tangu asubuhi anahangaika tu na Sitta.