CCM yampiga chini Fred Ngajiro (Vunjabei) Ubunge wa Jimbo la Isimani, yamteua Emmanuela Mtatifikolo

CCM yampiga chini Fred Ngajiro (Vunjabei) Ubunge wa Jimbo la Isimani, yamteua Emmanuela Mtatifikolo

Licha ya kuongoza kura za Maoni katika Mchakato wa Uchaguzi wa Ubunge, Jimbo la Isimani (Mkoa wa Iringa), Kamati Kuu ya CCM, imemuweka kando Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunja Bei kumteua Emmanuela Kaganda Mtafikolo kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa.

Pia soma
~
Fred Vunja Bei aongoza kura za maoni matokeo ya awali kumrithi Lukuvi. Awatupa wenzake mbali kama mshale
~ Emmanuela Mtatifikolo ajitosa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Isimani

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Katibu Wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi, imesema kuwa kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 105
(7)(f) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Julai 2025, Kamati Kuu imefanya uteuzi wa mgombea waCCM kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Isimani, lililopo wilaya ya Iringa Vijijini ambapo Mgombea aliyeteuliwa ni Emmanuela Kaganda MTAFIKOLO.
Mwenzake katoa kikojoleo, yeye ana nini!? Na uhakika Vunjabei hawezi toa jicho la tatu anajiheahimu sana, aendelee kufanya biashara tu mpaka Gen Z watakapochukua nchi atahitajika.
 
Kura za maoni zimepoteza maana,
Wajumbe wanakuonyesha chaguo lao, nyinyi mnawawekea mtu wasiyekubaliana naye.
CCM wafute utaratibu wa kura ya maoni, unapoteza muda na kuwaingiza wagombea kwenye hasara bila sababu.
 
Screenshot_20260427-082911~2.png
 
Back
Top Bottom