CCM yamulika wanaojipanga kwa Urais mwaka 2025

CCM yamulika wanaojipanga kwa Urais mwaka 2025

Wakati baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakitaka makada wenzao waendeleze utamaduni wa chama hicho wa kutochukua fomu za kuomba uteuzi wa urais ndani ya chama hicho mwaka 2025, baadhi wanataka utamaduni huo usitishwe ili kuwa na ushindani zaidi.

Licha ya hoja hiyo kutozungumzwa kwa uwazi lakini tayari kuna makundi yanayosigana juu ya jambo hilo na hivyo kuanza kutoa ishara kuwa huenda Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi watakabiliwa na upinzani ndani ya chama wakati ukifika.

Kauli aliyoitoa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka siku chache zilizopita visiwani Zanzibar kuwa Rais Samia na Dk Mwinyi ndiyo watakaokwenda nao hadi 2030, imekoleza vuguvugu la kutaka demokrasia ya ushindani ipate nafasi.

Samuel Paul, mmoja wa makada wa CCM, aliliambia Mwananchi kuwa ni dhahiri kuwa CCM, kimefunga milango kwa makada wake wenye ndoto ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu 2025 kwa kusema Rais Samia Suluhu na Dk Husein Mwinyi watahudumu hadi 2030.

Alisema ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na ile ya CCM ya mwaka 1977 zinatambua urais ni miaka mitano mitano, lakini CCM kina utamaduni iliyojiwekea wa Rais kuhudumu kwa vipindi viwili mfululizo (miaka mitano mitano).

Vikao vya juu vya CCM kuanzia Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na mkutano mkuu kila baada ya miaka mitano hupitisha jina la mgombea wa kiti cha urais lakini utamaduni kuachiana ndio hushika hatamu.

Ni kutokana na utamaduni huo, anapojitokeza kada wa CCM kutaka kushindana na Rais aliye madarakani anayepaswa kumalizia kipindi cha pili, huonekana ni msaliti anayetaka kuvuruga chama hivyo hutakiwa kuliondoa jina lake katika mchuano.

Kada wa CCM, Benard Membe ni miongoni mwa walioonja shubiri ya kufukuzwa chama baada ya kutangaza kutaka kuomba fomu za kuwania urais kukabiliana na aliyekuwa Rais John Magufuli.

John Shibuba naye alikabiliana na joto kali la kusakamwa baada ya mwaka 2010, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo akikabiliana na Jakaya Kikwete.

Hata hivyo Shibuda hakuirejesha fomu hiyo licha ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa ikiwemo kusaka wadhamini.

Kitendo hicho kilionekana kukaidi utamaduni wa chama hicho hivyo Shibuda, aliangushwa kwenye kura za maoni alipokuwa akiomba uteuzi wa kutetea kiti cha ubunge wa Maswa Mashariki, alichokuwa akikishikilia na hivyo kuhapia Chadema alikowania kiti hicho na kushinda ubunge.

Samson Njaidi, mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, alisema utamaduni wa CCM unaondoa dhana nzima ya demokrasia kwa hasa kwa kuwa chama hicho ni kioo na kiongozi kwa vingine

Alisema kama Rais aliyepo madarakani akishindanishwa itaongeza umakini na chachu ya kinyang’anyiro husika.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanaiona kauli ya Shaka ni ishara ya uwepo wa moto unaofukuta chini kwa chini ndani ya CCM kuelekea 2025 na wapo makada wanaojiimarisha kugombea nafasi hizo.

Kauli ya Rais Samia, aliyoitoa akiwa Ikulu Januari 4, 2022 wapo watu ambao hakuwataja majina, wanapanga safu za uongozi kuelekea 2025 na kusema ni ‘stress’ (msongo) na kutaka wasamehewe kwa kuwa wana homa ya uchaguzi.

Shaka alivyofunga mlango

Akizungumza katika kongamano la kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo zinazofanywa na Rais Samia lililofanyika mkoa wa Unguja Kaskazini huko Zanzibar, Shaka aliwaambia wanachama wa CCM kuwa watamalizana na Rais Samia 2030.

“Kwa kazi nzuri aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwaheshimisha Watanzania, ya kuheshimisha Afrika, Rais Samia tutamalizana naye 2030, penye uhai Mungu atupe uhai,” alisema Shaka katika kongamano hilo.

Msimamo huo huo akauelekeza kwa Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi akisema naye watamalizana naye 2030 na kusisitiza kama kuna mtu (mwana CCM) ana ndoto za kuchukua fomu 2025 kuwania nafasi hizo basi waziweke pembeni.

“Chama hiki hakijawahi kucheza bahati nasibu kweye kupata viongozi wa kuwakabidhi dhamana ya kulivusha taifa hili,” alisisitiza Shaka na kusema katika eneo ambalo chama hicho kiko makini, ni eneo la kuwapata viongozi.

Lakini kauli hii ya Shaka inaonekana kama ni mkakati mahsusi ndani ya CCM, kwani hata katika mikutano ya kiserikali, hakutakosekana kiongozi atakayemnadi Rais Samia kuelekea 2025 na hii ni kuanzia Waziri mkuu hadi mawaziri na Naibu.

Walichokisema wasomi

Akizungumzia jambo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Bob Wangwe alisema aliyetoa maneno hayo ni kiongozi wa CCM na chama hicho kina katiba, miongozo na miiko ambayo haiku kwenye katiba au kanuni zake.

Alisema kitu alichokisema Shaka ni jambo linalofanyika ndani ya chama hicho kwa sababu imezoeleka Rais anapomaliza kipindi kimoja, anaachiwa kipindi cha pili ili akamilishe miaka 10 kwa mujibu wa katiba ya nchi nay a chama.

“Ukija kwenye dhana ya demokrasia, nafikiri hapo kutakuwa na maswali, kwamba demokrasia inahitaji watu washiriki kwenye uchaguzi ndani ya chama au nje ya chama. Mwisho wa siku wanaoamua hilo ni walewale ndani ya CCM ambayo of course ni demokrasia.

“Lakini ukiangalia kwenye katiba, inaelekeza kwamba kila baada ya miaka mitano, kutakuwa na uchaguzi wamchague kiongozi. Sasa wamefutaje kwenye vyama yao, wataangalia miongozo inawa-govern namna gani,” alisema Wangwe.

Chanzo: Mwananchi
Mbona kipindi cha JPM walioanza kuonesha dalili za kutaka kuwania nafasi hiyo walikuwa wanawang'ong'a ikiwa pamoja na huyo anayetoa tahadhari kwa sasa?

Zamu hii hakuna atakayekubali, utamaduni sio sheria ni mazoea yasiyokuwa na tija na hasa panapokuwepo hakuna mtu makini wa usimamizi wa haki.Aliyepo anatosha kula embe alilookota lakini kuongezewa na akilazimisha yeye ndio atalazimishwa kuondoka kwa aibu na wananchi ambao hawathaminiwi
 
Mbona kipindi cha JPM walioanza kuonesha dalili za kutaka kuwania nafasi hiyo walikuwa wanawang'ong'a ikiwa pamoja na huyo anayetoa tahadhari kwa sasa?

Zamu hii hakuna atakayekubali, utamaduni sio sheria ni mazoea yasiyokuwa na tija na hasa panapokuwepo hakuna mtu makini wa usimamizi wa haki.Aliyepo anatosha kula embe alilookota lakini kuongezewa na akilazimisha yeye ndio atalazimishwa kuondoka kwa aibu na wananchi ambao hawathaminiwi
Mimi nimekuelewa, kama HAKUBALIKI Kwa wananchi, BUSARA itumike kumwambia YATOSHA!!!!
 
Mimi binafsi namuunga mkono Mama Samia kwa Urais 2025 amefanya mandeleo mengi sana kwa kipindi kifupi
 
Mimi binafsi namuunga mkono Mama Samia kwa Urais 2025 amefanya mandeleo mengi sana kwa kipindi kifupi
Maendeleo gani au wewe ndiye ulirudi na kuanza kuporomosha majumba ya kifahari kwa kasi hapo Mikocheni TPDC ndio unaona uamefanya maendeleo?
 
Waanze kummulika rais wa mawe. Ndio maana ana mkwamisha Mama.
 
Yes. Tuendelee kusukuma ajenda ya katiba mpya ili walau 2025 iwe imepatikana na na ikibidi itumike kuandaa tume ya uchaguzi
Narudia kusema tena hapa JF, hayo ni mawazo na mtizamo wa Mwenyezi shaka,pengine ndio msimamo wake ktk chama lakini ni dhahiri Ccm utamaduni uliopo au sheria,kanuni,miongozo au katiba yenyewe ya kumwachia mgombea urais kumaliza kipindi cha pili si kwa namna Rais aliyepo madaraka alivyopata nafasi hiyo.
Ikumbukwe wazi, Rais Samia mbali na nafasi hiyo, amerithi kutoka nafasi hiyo baada ya dhoruba kubwa iliyotokea ktk Taifa ya kuondokewa na hayati Magufuli ambaye ndiye chama kilikuwa kimemuidhinisha katika nafasi ya uraisi kama ulivyo utamaduni wa chama ya kutoruhusu mgombea mwingine kuchukua fomu ya nafasi hiyo. Hivyo Mwenyezi Shaka binafsi naona anayeeleza bila kusema aliyepo madaraka alipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais au alilitishwa kama makamu wa Rais akitokea Zanzibar kama ilivyo hada?
Binafsi nashauri tumwache Rais afanye majukumu yake maana 2025 bado mbali sana ila uhuru utamalaki.
 
Kumbukeni mkiendelea kurumbana kumbukeni mungu nae yupo na pia nae anayo maamuzi yake tena Yana nguvu kuwazidi nyie binadamu haya shauli yenu.
 
tunataka demokrasia ndani ya chama huo utamaduni wa muendelezo hautakiwi unaiangamiza nchi kiuchumi,kiutamaduni na kisiasa.

wacha wanachama washindane kwa uhuru sababu hakuna mwenye hati miliki ya kuongoza nchi kwa miaka kumi.waachieni wananchi uhuru wa kuchagua wanaowapenda.

Tatizo lako litakuwa Ni uelewa wa mambo haya ya Siasa. Toa mfano chama gani na katika Nchi gani hiyo ilibadilisha mgombea muhula mmoja ? Trump mwenyewe na ujinga Wake wote RP walimpa kama chama. Akapigwaaa na wananchi na wanazengo.
 
Back
Top Bottom