Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeonya watendaji na viongozi wake wanaohujumu mchakato wa kura za maoni za kupata wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Dk Mohamed Said Dimwa ametoa onyo hilo alipozungumza na wajumbe wa kamati za siasa za matawi, wadi na majimbo katika Wilaya ya Mkoani, Pemba.
Dk Dimwa alisema CCM itawasimamisha kazi na kuwapeleka katika kamati za usalama na maadili watendaji na viongozi watakaohujumu mchakato huo.
Alisema chama hicho kitaanza kufanya usafi wa ndani kwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watendaji wanaofanya udalali wa kisiasa kwa masilahi yao na wanaotumiwa na watia nia kuvunja taratibu na miongozo ya CCM.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Dkt. Dimwa alisema usafi huo utakuwa ni maandalizi ya kupata wagombea wasio na chembechembe za rushwa, wenye utu na uzalendo wa kusimamia na kuleta maendeleo ya wananchi.
"Natumia ziara hii kutoa onyo kwa watendaji wote na viongozi waliopo katika usimamizi ya chama kuacha tabia ya kutumiwa na watu kuharibu utaratibu na kanuni za chama, hatuwezi kuacha vitendo hivi viendelee; tunataka kupata wagombea safi watakaouzika na kukubalika uchaguzi ujao," alisema.
Aliongeza: "Lazima chama kirudi kwa wanachama wenyewe, hiki si chama cha wapiga deal (wababaishaji) bali ni chama cha kijamaa yaani wakwezi, wakulima na wafanyakazi, ni lazima tulinde misingi ya ASP na Tanu".
Alisema kupitia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliofanyika Januari 18-19, mwaka huu yamefanya mabadiliko ya Katiba yake ya 1977 toleo la 2022 kwa kuongeza idadi ya wapigakura katika mchakato wa ndani wa kura za maoni ili kuongeza upana wa uwazi, uhuru na demokrasia ndani ya chama.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Zanzibar, Abdi Mahmoud Abdi alisema kundi la vijana wa chama hicho linatakiwa kuwa mfano bora wa kuipigania CCM ishinde na kupata viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo.
Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya Organaizesheni CCM Zanzibar, Ibrahim Omar Kilupi alisihi wajumbe hao wafanye uamuzi sahihi ili wagombea wanaowateua katika kura za maoni wawe wanakubalika na kuchagulika.