Tetesi: CCM yapanga kufanya mkutano eneo ambalo CHADEMA walipanga kufanya mkutano huko Singida Magharibi

12STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
1,189
Reaction score
407
Serikali inajipiga kifua kwamba katika Uongozi wa MAMA SAMIA RAIS WA JMT ,Demokrasia imestawi.

Kiukweli usawa wa uendeshaji wa shughuli za kisiasa unabinywa chini kwa chini karibia kila Kona ya Nchi yetu.

Kesho Jumanne Tarehe 11/6/2024 kutakuwa na Mkutano wa MHESHIMIWA TUNDU LISSU (MAKAMU/KITI CHADEMA TAIFA) Katika KATA YA MTUNDURU,,Kijiji Cha MTUNDURU.

Baada ya kusikia Tundu Lissu Atakuwa na Mkutano Kijiji na Kara hio ya MTUNDURU, CHAMA TAWALA CCM Kwa uongo wao nao wamedai kufanya Mkutano eneo Hilo Hilo katika Kijiji hicho hicho Cha MTUNDURU.

Kwa habari nilizo nazo kwenye chanzo sahihi kilicho huru kisichofungamana na upande wowote wa chama Cha kisiasa iwe CHADEMA ama CCM;Chama Cha tawala kimeingiwa na kiwewe maana CHADEMA imeshika KASI huko SINGIDA mpaka vijijini,huenda baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa tukaona MABADILIKO MAKUBWA ya VIJIJI NA MITAA mingi Sana NCHINI kuingozwa na chama kikuu Cha upinzani CHADEMA.

Kwa kawaida wakati WOOTE wakiwa na mikutano Yao kwenye Kijiji hicho Cha MTUNDURU hufanya mikutano Yao kwenye viwanja vyao vya ofisi za CCM kijijini hapo.Iwe nikutano wa Mbunge au mkubwa yeyote mikutano Yao huishia kufanya huko.

Kwa vile TUNDU LISSU anakuja wameogopa mno,
1).Na wao wanatoka kufanya Mkutano eneo la madukani.

2).Wakati wanajua TUNEU LISSU Ana Mkutano kesho Tarehe 11/6)2024 na wao wameamua kufanya Mkutano kesho iyo hio na Tarehe iyo hiyo.

2).Wamepanga kufanya Mkutano kwenye eneo Lilo Hilo ambalo CHADEMA wanafanyia mkutano.------ hii sio sawa Ni vurugu hizo.

3).CCM na Uongozi wa shule ya msingi MTUNDURU wamekaa kikao hapi shuleni na kupiga marufuku chadema wasifanyia Mkutano hata kwenye uwanja wa shule ya msingi MTUNDURU.

CCM acheni uoga waacheni chadema wafanye mikutano kila chama kipewa jukwaa sawa la kueleza Sera zao Mwisho wa siku Wananchi waamua Nani wa kuongoza Kijiji au Jimbo ama NCHI.
 
Tundu Lisu ahirishe tu, nyita yake inang'aa asishindane nao... Biblia imesema usishindane na mtu MUOVU.
 
..wafanye mkutano wa pamoja.
inabidi Tundu Lissu aanze kutembea na mark 🖊 pen na ubao wa kueleza wananchi wa vijijini ni kwa namna gani wanaumia kulima, huku wakiwa na huduma mbovu za maji, umeme, huduma za afya na ufukara sababu ya CCM kuwanyonya pesa zao wanazopata kwa shida na kwenda kununua bodaboda, vitenge, kofia ili waje kuwahadaa.
Mavuno ni mengi ila watenda kazi wachache Lissu sauti yake inasikika sana. Kinachotakiwa ni kuondoa ujinga wa watu wa vijijini huo ndio mtaji wa CCM
 
inabidi Tundu Lissu aanze kutembea na mark [emoji996] pen na ubao wa kueleza wananchi wa vijijini ni kwa namna gani wanaumia kulima, huku wakiwa na huduma mbovu za maji, umeme, huduma za afya na ufukara sababu ya CCM kuwanyonya pesa zao wanazopata kwa shida na kwenda kununua bodaboda, vitenge, kofia ili waje kuwahadaa.
Mavuno ni mengi ila watenda kazi wachache Lissu sauti yake inasikika sana. Kinachotakiwa ni kuondoa ujinga wa watu wa vijijini huo ndio mtaji wa CCM
Unanena ujumbe wa nguvu sana
 
CCM wanataka kuleta vurugu.
si mara ya kwanza

2183704_IMG_1183.jpg
 
Ccm bila kuamrisha watoto wa shule na watumishi hawapati watu
Na hivi shule zimefungwa huu si muda muafaka ccm kufanya mikutano
Umesema ukweli kabisa mwamba! Labda wabebe na malori Toka sehemu nyingine!
 
M
Serikali inajipiga kifua kwamba katika Uongozi wa MAMA SAMIA RAIS WA JMT ,Demokrasia imestawi.

Kiukweli usawa wa uendeshaji wa shughuli za kisiasa unabinywa chini kwa chini karibia kila Kona ya Nchi yetu.

Kesho Jumanne Tarehe 11/6/2024 kutakuwa na Mkutano wa MHESHIMIWA TUNDU LISSU (MAKAMU/KITI CHADEMA TAIFA) Katika KATA YA MTUNDURU,,Kijiji Cha MTUNDURU.

Baada ya kusikia Tundu Lissu Atakuwa na Mkutano Kijiji na Kara hio ya MTUNDURU, CHAMA TAWALA CCM Kwa uongo wao nao wamedai kufanya Mkutano eneo Hilo Hilo katika Kijiji hicho hicho Cha MTUNDURU.

Kwa habari nilizo nazo kwenye chanzo sahihi kilicho huru kisichofungamana na upande wowote wa chama Cha kisiasa iwe CHADEMA ama CCM;Chama Cha tawala kimeingiwa na kiwewe maana CHADEMA imeshika KASI huko SINGIDA mpaka vijijini,huenda baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa tukaona MABADILIKO MAKUBWA ya VIJIJI NA MITAA mingi Sana NCHINI kuingozwa na chama kikuu Cha upinzani CHADEMA.

Kwa kawaida wakati WOOTE wakiwa na mikutano Yao kwenye Kijiji hicho Cha MTUNDURU hufanya mikutano Yao kwenye viwanja vyao vya ofisi za CCM kijijini hapo.Iwe nikutano wa Mbunge au mkubwa yeyote mikutano Yao huishia kufanya huko.

Kwa vile TUNDU LISSU anakuja wameogopa mno,
1).Na wao wanatoka kufanya Mkutano eneo la madukani.

2).Wakati wanajua TUNEU LISSU Ana Mkutano kesho Tarehe 11/6)2024 na wao wameamua kufanya Mkutano kesho iyo hio na Tarehe iyo hiyo.

2).Wamepanga kufanya Mkutano kwenye eneo Lilo Hilo ambalo CHADEMA wanafanyia mkutano.------ hii sio sawa Ni vurugu hizo.

3).CCM na Uongozi wa shule ya msingi MTUNDURU wamekaa kikao hapi shuleni na kupiga marufuku chadema wasifanyia Mkutano hata kwenye uwanja wa shule ya msingi MTUNDURU.

CCM acheni uoga waacheni chadema wafanye mikutano kila chama kipewa jukwaa sawa la kueleza Sera zao Mwisho wa siku Wananchi waamua Nani wa kuongoza Kijiji au Jimbo ama NCHI.
Mwisho watasema ardhi yote ni mali ya CCM, Chadema watafute ardhi yao. Wanatia huruma, wanasikitisha wameshikwa vibaya!
 
Mimi sijaona tatizo hapo...

Kila chama kifanye mkutano wake. Na kwa maoni yangu, huo ndio utakuwa wakati mzuri wa kupima nani anasikilizwa na kukubalika kijijini hapo, yaani CHADEMA au CCM...?

Waacheni wala msigombane nao. Mnachotakiwa kufanya ni hiki;

Kama wao CCM watafanyia mkutano wao viwanja vya madukani, nyie CHADEMA nendeni mkafanyie mkutano wenu kwenye viwanja vyao vya CCM ambavyo wao ndipo hufanyia mikutano yao!

Acheni kulialia. Tundu Lissu ameshawaambia, kuweni ngangari. Mambo yasiyokuwapo kisheria yakataeni na wakilazimisha wapigeni makofi wote wanaokuja kuwasumbua..!
 
Ccm wasichojua ni kwamba confrontational politics ndiyo huwa zinampa milage Tundu Lisu, na anazitaka sana maana anaziweza.
Wajinga, hawajui hilo..

Tukumbuke tukio la kule Ngorongoro. Hiyo confrontation ya jamaa kuongoza timu yake kuacha magari yao pembeni na wao kukaa barabarani (highway road) na kuzuia kila gari ktk njia ile haikuwa ya kitoto eti maana ilibidi polisi yote mkoa wa Arusha impigie magoti kumwomba aachie njia..

Eti walijidai kumfungulia kesi. Hiyo kesi nadhani ilishajifia yenyewe huko maana haisikiki tena!

Sasa sembuse hao wa kijijini, wanawezaje kuzuia mkutano wa Tundu Lissu kwa mfano?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom