"Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona harakaβ-Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM CCM Humphrey Polepole ameandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya kuripotiwa kuwa wasanii watatu wamepata ajali hii leo wakitokea mkoani Iringa.
Habari Star TV Tanzania
Kutumia Ajali za Watu kama tiketi yako ya 'Kujiimarisha' zaidi 'Kisiasa' inaweza ikawa ni sehemu Kuu ya Kuonyesha 'Udhaifu' wako wa Kifikra kuliko ambavyo pengine umetegemea. Je, kwa mfano Watu wakisema kuwa hiyo Ajali 'imetengenezwa' nanyi 'Kiuchawi' ili mjipatie 'Political Mileage' katika Kipindi hiki cha Kampeni mtawalaumu?
Sasa kwakuwa mmeonyesha Upendo kwa hawa 'Wasanii' nawaombeni ili niamini mna Upendo kwa Watanzania hebu 'Kalipieni' upesi sana 'Bills' za 'Wagonjwa wote wasio na Uwezo wa 'Kulipia' katika Hospitali zetu Kubwa nchini Tanzania. Mkimaliza hapo lipieni pia na 'Bills' za walioshindwa 'Kulipia' Maiti zao Hospitalini nchi nzima.
Najua na nina Uhakika 'Nitachukiwa' sana tu ila mtanisamehe katika Maisha yangu 'Msamiati' wa 'Unafiki' na 'Kujipendekeza' haupo. Tuvumiliane tu!