Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikishinda ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, chama hicho kimeshindwa katika viti vya udiwani katika Kata za Machinjioni Kigoma Ujiji Kigoma na Mnyawa Tandahimba mkoani Mtwara.
Aidha, chama hicho tawala kimeshinda katika Kata ya Kati Manispaa ya Arusha na Kata ya Mkundi pia Tandahimba katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita. Katika Kata ya Mnyawa, mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Nalinga Basha ameibuka mshindi kwa kuwashinda wagombea wenzake akiwamo wa CCM.
Basha anakuwa diwani wa kwanza kuandika historia kwa Mkoa wa Mtwara kushika nafasi hiyo ya uongozi kupitia chama cha upinzani tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.
Katika uchaguzi huo, Basha alishinda kwa kishindo baada ya kupata kura 2,352 dhidi ya mpinzani wake, Njayo Abdul wa CCM aliyepata kura 1,508 na hivyo kushinda kwa tofauti ya kura 844.
Katika Kata ya Mkundi, mgombea wa CCM, Nilinga Shaweje, alishinda kwa kura 1,154 na kuwabwaga wapinzani wake wa CUF, Maundo Omari aliyepata kura 1,098 na Rashidi Matumla wa Chadema aliyeambulia kura 127.
Aidha, CCM imeshinda katika Kata ya Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa, baada ya mgombea wake, Nelson Mpalala kupata kura 1,312 sawa na asilimia 61 ya kura 2,159 zilizopigwa wakati mgombea wa Chadema, Sadick Nyambo alipata kura 817 sawa na asilimia 30.
Mkoani Kigoma, CCM imeshindwa katika Kata ya Machinjioni katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, baada ya mgombea wake, Yahaya Akilimali kupata kura 398 dhidi ya kura 448 za mgombea wa Chadema, Ahmad Singwa. Wagombea wengine ni Jumanne Fumawicha wa TADEA aliyepata kura mbili, Ahmad Digio wa DP na Mandela Mandela wa Jahazi Asili hawakupata kitu.