CCM yatamba haiogopi mafisadi!

CCM yatamba haiogopi mafisadi!

Mbatia: Mabadiliko CCM hayataondoa umaskini


*Asema ni majigambo ya kisiasa yasiyo na manufaa
*Mukama asisitiza walichofanya si nguvu ya soda


Na Grace Michael

MABADILIKO ya kujivua gamba yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuibua mjadala katika jamii na
vyombo vya habari yameelezwa kutokuwa na maana kwa kuwa hayana mkakati wowote wa kuondoa umasikini unaowakabili wananchi kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, CCM kimetakiwa kuachana na majigambo ya kisiasa na badala yake kije na mkakati wa kuwaondoa wananchi katika ugumu wa maisha unaowakabili kwa sasa.

CCM kilifanya mabadiliko ya uongozi wake wa ngazi ya juu ambayo ilitanguliwa na kujiuzulu kwa sekretarieti nzima ya chama hicho na Kamati Kuu na kuteua wajumbe wengine, akiwamo Katibu Mkuu mpya, Bw. Wilson Mukama.

Pamoja na kufanyika kwa mabadiliko hayo ambayo wana-CCM wanaeleza kwamba yatasaidia kurejesha heshima ya chama hicho kwa jamii na kutoa tambo kwa vyama vya upinzani kuwa kimejipanga upya kupambana nao baada ya kuwatoa wale kinaodai ni mafisadi.

Hata hivyo, kadri siku zinavyokwenda, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameanza kuukosoa mkakati huo, wakisema unatakimaliza zaidi kwa kuwa kitakuwa na mgawanyiko mkubwa huku Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia akisema wazi kuwa hayana tija kwa kuwa wananchi wako katika hali ngumu kimaisha.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Mbatia alisema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kujadili namna ya kuwaondoa wananchi katika umaskini mkubwa unaowakabili na si mambo ya kutambiana au kukabiliana kisiasa.

"Jamani namuomba Mukama ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM na vyama vyote vya siasa kuachana na malumbano ya kisiasa na badala yake tujadili mambo yanayowakabili wananchi...daraja la wenye nacho na wasio nacho limekuwa kubwa, mifumko ya bei, maisha yamekuwa magumu kwa wananchi hivyo mambo ya kujigamba kuikabili CHADEMA au wapinzani, hayana tija tuangalie namna ya kuwakomboa wananchi hapa walipo," alisema Bw. Mbatia.

Alisema kuwa nchi ina mambo mengi ya kujadili ili kukabiliana na umasikini unaoongezeka kila kukicha ambapo shilingi ya Tanzania nayo inazidi kushuka thamani yake dhidi ya dola, hivyo CCM badala ya kujigamba kuvua magamba wanatakiwa kuja na mkakati wa kumaliza matatizo hayo ambayo ndiyo kero kubwa kwa wananchi.

Kutokana na hayo, Bw. Mbatia alisema kuwa hoja zote zinazotolewa na viongozi wapya wa CCM akiwemo Bw. Mukama ambaye ameweka wazi msimamo wake kuwa mabadiliko hayo si nguvu ya soda, ni hoja nyepesi zisizo na mashiko kwa kuwa haziwasaidii wananchi kuondokana na umaskini.

"Mwaka 2015 Tanzania tutahukumiwa na malengo ya milenia kwa kuwa tutatakiwa kueleza tumeyatekelezaje na malengo hayo ni kuondokana na umasikini, elimu kwa wote, usawa wa kijinsia na kuwawezesha akina mama, kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini miaka mitano na vifo vya akina mama wajawazito, kupambana na UKIMWI na ushirikishanaji," alisema Bw. Mbatia.

Kuvua gamba si nguvu ya soda

Katika hatua nyingine, Mwajuma Juma anaripoti kutoka Zanzibar kuwa Bw. Mukama amesema kuwa moto uliowashwa na chama hicho hivi karibuni kuhusiana na mafisadi ndani yake umelenga katika kurejesha imani kwa wananchi wakione kuwa ni chama bora na sio nguvu ya soda.

Kauli hiyo ameitowa huko katika Ofisi Kuu ya Chama hicho Kisiwandui mjini Unguja wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wazee, ikiwa ni mfululizo wa utambulisho wa wajumbe wa Sekretarieti mpya iliyoteuliwa baada ya ile ya awali kujiuzulu.

Alisema kuwa moto huo haukuwa nguvu za soda na wala hautazimika hadi pale wananchi watakapokiamini na kuona kuwa ndio chama pekee ambacho kitakuwa ni kimbilio la wanyonge badala ya kuwa matajiri.

Alifahamisha kuwa ili kufikia azma hiyo chama hicho kwa sasa kimejipanga vizuri kwa kubuni mbinu mbalimbali na mikakati madhubuti, ambayo itasaidia kurejesha haiba yake iliyopotea miongoni mwa wananchi.

“Moto uliowashwa ndani ya chama hichi siyo nguvu za soda na hautazimika hadi imani ya wananchi dhidi ya chama iweze kurejea kwa Watanzania wote,” alisema.

Katika kikao hicho, wazee hao walitoa shukrani zao kwa viongozi hao kwa hatua waliyofikia na kuwataka viongozi wa mikoa hadi taifa kuungana ili agizo la katibu huyo liweze kufikiwa.

Bw. Mukama yupo Zanzibar kwa ajili ya kuwatambulisha wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, tangu Aprili 17, mwaka huu.

Ripoti ya CAG na NCCR

Bw. Mbatia alitumia mwanya huo kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. John Tendwa kukisafisha chama hicho na tuhuma za kushindwa kuwasilisha hesabu za matumizi ya fedha za ruzuku kwa madai kuwa NCCR-Mageuzi kimewasilisha ripoti ya ukaguzi katika ofisi yake.

Bw. Mbatia alisema kuwa chama chake kimekuwa kikitekeleza sheria ya vyama vya siasa inayotaka kukaguliwa kwa fedha zake kila mwaka ambapo alionesha ripoti ya ukaguzi kuanzia mwaka 2005 hadi sasa.

Alisema kuwa ni haki ya wananchi kujua namna ya fedha za ruzuku zinavyotumika na ndio maana chama hicho kinatekeleza sheria hiyo kwa kukaguliwa fedha za ruzuku pamoja na fedha za vyanzo vingine kama ada za wanachama.

"Hizi taarifa za ufisadi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa zimeleta mtafaruku mkubwa kwa kuwa wanachama wengi wanapiga simu wakihoji kuhusu suala hili na wanafanya hivyo kwa kuwa chama kimeweka utaratibu wa kuweka wazi mapato na matumizi, hivyo tunamwomba msajili atusafishe kwa kuwa nakala ya ripoti ya ukaguzi anayo," alisema Bw. Mbatia.

Alisema NCCR-Mageuzi hakiko kwenye kundi la ufisadi wa fedha za walipa kodi kwa kuwa kila mwaka hukaguliwa na ripoti kuwasilishwa katika mamlaka husika.
 
4 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Bravoo Mbatia,malumbano hayasaidii,wananchi wanateseka wao wanasiasa wananeemeka
April 20, 2011 12:46 AM
blank.gif

Anonymous said... Mukama mbona hatujasikia mkitaja majina ya mafisadi kama mna nia kweli ya kupambana na ufisadi ndani ya chama tajeni majina ya hao mafisadi hadharani. vinginevyo ni usanii mtupu.
April 20, 2011 2:41 AM
blank.gif

Anonymous said... ccm mmekuwa wasaanii, mnapiga kelele ili msikike lakini mkisikika hamna cha maana kinaeleweka kutoka kwenu. Kama wajasiri kweli mnashindwa nini kuwataja hao mafisadi? Wenzenu mbona wanataja? Mkama na genge lako mtajikuta mnashindwa kujibu maswali ya wananchi mkiendelea na kelele zenu.

Cha msingi kaeni chini mje na mpango mkakati wa kuwapa vijana ajira, kuwa na mipango ya kuzuia wageni kupora ajira za vijana kwa kuwabana wageni watoe ujuzi na kuondoka sio kufanya hata na kazi za uhasibu. Wageni wamejaa humu nchini wanachukua ajira zetu mnasikiaaaaaaaaaaaaaaaa
April 20, 2011 3:26 AM
blank.gif

Anonymous said... Huu wa CCM ni usanii mtupu. Wananchi tunataka mabadiliko ya kweli haswa hali ya maisha. Inashangaza hawa wakina Nape wanazunguka na kufanya mikutano ya hadhara hawasemi mikakati ya kumkomboa Mtanzania ni ipi maana wao ndio wanajisifia CCM imejivua gamba. Mbona mapambano yao ni dhidi ya CHADEMA tu sisi hayo yanatusaidia nini jamani? Inaelekea hofu yao ni kupata madaraka ili waidhibiti CHADEMA na sio kuwasaidia walalahoi. Hawatafanya lolote la maana sana sana wanazidisha mpasuko ndani ya CCM na kujijengea maadui.
April 20, 2011 5:12 AM

Post a Comment
 
Nnauye anavaa gamba lililovuliwa na wazee!
ban.blank.jpg


Barnabas Maro​

amka2.gif
"WALA watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka , divai ikamwagika, na viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote" (Mt. 9:17).
Kijana wangu aitwaye Nape Nnauye ambaye sasa amepewa wadhifa wa kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, anasema orodha mpya ya mafisadi iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa mjini Tabora majuzi ni ‘sawa na mchezo wa kuigiza'. Nimtahadharishe Nnauye kuwa akiingilia lisilomhusu atapata lisilomridhi; tena maji asiyoyafika hajui kina chake.
Mwaka 2007 wakati Dk. Willibrod Slaa alipotangaza orodha ya mafisadi 11 pale Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam, CCM wakiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wao, Yusuf Makamba, waliibeza orodha ile wakimwambia Slaa aende polisi kama ana ushahidi.
Ngoma ileile aliyocheza Makamba ndiyo anayocheza sasa Nnauye; ila anajikanganya kwa kukataa na wakati huohuo anakubali asemayo Slaa.
Nnauye anasema tangazo la Slaa halina lolote katika mchakato wa kuwang'oa mafisadi ndani ya CCM na kwamba wanachofanya (CHADEMA) ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli. Akaendelea: "Tunajua mipango yao ya kujaribu kufanya kampeni za kuchafua watu wasafi ndani ya CCM akiwamo rais na familia yake".
Kwa kuwa Nnauye amevishwa ‘gamba' la wazee, naye ghafla amezeeka hata kumbukumbu zimemtoka kwa kudai eti CHADEMA wamepanga kutumia baadhi ya vyama vya upinzani, viongozi wa dini na baadhi ya vyombo vya habari na waandishi ili kuwachafua makada wa CCM, Rais Kikwete na familia yake.
Eti mkakati huo hautaweza kuidhuru CCM wala kuifanya iachane na mchakato wa kuwashughulikia mafisadi ndani ya CCM. Anakataa nini na anakubali nini?
Kuhusu madai yake kwamba CHADEMA inavitumia vyama vingine vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi, Nnauye amesahau ndoa ya CCM na CUF? Barazani CUF ni serikali na uani ni ‘wapinzani'. Yawezekana kuchanganya sukari na magadi katika chai na ikafaa kunywewa? Ni siri gani itakayozungumzwa na wapinzani isiifikie CCM?
Mara ngapi Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ameshirikiana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia kuishambulia CHADEMA na viongozi wake? Mara ngapi viongozi wa dini nao wameingizwa kwenye mkumbo wa kuishambulia CHADEMA wakidai kuwa eti maandamano na mikutano yake inahatarisha amani ya nchi?
Nnauye anasahau kuwa hivi karibuni vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM vilifanya mageuzi ya uongozi na kupitisha maazimio yenye lengo la kuwaondoa wenye tuhuma nzito za ufisadi na ukosefu wa maadili ili kujivua ‘gamba'.
Katika orodha mpya ya viongozi, Nnauye ni Katibu wa Uenezi na Itikadi, hivyo kavishwa ‘gamba' lililoachwa na wazee wake!
Tangu mwaka 2007 viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiilaumu CCM kwa kuwakumbatia mafisadi. Ingawa watuhumiwa walikanusha kwa mapana na marefu, sasa ndio walio mahakamani, wamejiuzulu na wengine (wanaofahamika lakini hawatajwi), wamepewa miezi mitatu wajiondoe wenyewe katika chama. Isijekuwa kisu kibutu hakichinji kuku!
Kwa upande wake, Dk. Slaa amemwambia Rais Kikwete kwamba kama watuhumiwa hao watatajwa na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuondolewa kwenye nafasi zao za uongozi, katika chama na ubunge, ndipo dhana ya kujivua ‘gamba' itakapokuwa na mantiki, vinginevyo ni usanii mwingine.
Dk. Slaa anasema Watanzania wanataka kuona fedha zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na wahusika wafikishwe mahakamani badala ya kushikilia maneno matupu ya chama kujivua ‘gamba'.
Zi'wapi fedha za EPA, Kagoda, Benki Kuu ya Tanzania, Meremeta na Tangold?
Mbona mpaka sasa serikali inashindwa kuchukua uamuzi dhidi ya wahusika? Je, waliorejesha fedha za EPA ni kina nani na kwa nini inakuwa ‘haramu' kuwataja; tena hawajafikishwa mbele ya sheria?
Si kweli kwamba miongoni mwao ni viongozi wakuu wa serikali? Kama ni hivyo, basi CCM kujivua ‘gamba' hakutoshi kwani kinachotakiwa ni kufyonzwa damu yote na kuwekewa nyingine isiyokuwa na virusi vya ufisadi na kiwewe cha kutotaka kuwaachia wengine (wapinzani) madaraka.
Usanii uliofanywa na NEC na Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma ni sawa na "kutia kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu, maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi." (Mt. 9:16).
Nape Nnauye ni kiraka cha nguo mpya katika nguo mbovu; tena ni divai mpya katika kiriba kilichochoka. Amesahau alivyosakamwa na baadhi ya viongozi alipozungumzia ufisadi wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM?
Hakumbuki jinsi mmoja wa watuhumiwa alivyokataa kuupokea mkono wake na kumtamkia wazi kuwa "kijana wewe nakuchukia!" Kama Nnauye anadhani amesimama, aangalie asianguke!



h.sep3.gif

marobarnabas@yahoo.com
0784/0715 33 40 84 na 0756 85 53 14
 
Idd Azzan atishiwa kunyanganywa kadi


Na Anneth Kagenda

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, Bw. Idd Azzan amelalamika kuwa kuna watu ndani ya chama hicho mkoa wa Dar es Salaam wamemtishia kumnyanganya kadi
yake uanachama, jambo ambalo halimtishi.

"Kuna mtu mmoja aliniambia kwamba tutakunyanganya kadi yako ya uanachama kwa madai kuwa ninataka Sekretarieti ya CCM Mkoa na Kamati ya Siasa ijivue gamba, hata wakiitaka leo nitawapa lakini ni lazima tuseme ukweli ili kukinusuru chama chetu," alisema.

Hayo aliyasema Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya kuweka msisitizo kwamba hababaishwi na maneno ya baadhi ya watu pale anapotaka kusema ukweli ndani ya CCM kwa nia ya kukinusuru chama.

Alisisitiza kwamba Sekretarieti ya Mkoa na Kamati ya Siasa lazima ijiuzulu ili chama kiweze kujipanga na kujiwekea mikakati endelevu ya kushika dola bila kukumbwa na kashfa za hapa na pale zinazoendelea ndani na nje ya chama.

"Sekretarieti ya Mkoa inanitisha eti kwanini nilisema wajivue magamba, wananiambia watanionyesha, lakini mimi ninachoamini ni kwamba pale ukweli unaposemwa wazi wazi bila kificho huwa unauma lakini lazima tuuseme kila wakati.

"Viongozi wa Mkoa wamegawanyika katika makundi mawili ambayo yamechangia kwa asilimia kubwa kukidhorotesha chama tangu mwaka 2007. Yaliwaengua madiwani wa Kata na wale wa viti maalumu waliokuwa wakipendwa na wananchi, na kusababisha wananchi kuvipigia kura vyama vya pinzani," alisema.

Aidha alisema kuwa Aprili 14, mwaka huu Katibu wa CCM Mkoa, Bw. Kilumbe Ng'enda aliitisha kikao cha makatibu kata na madiwani na kuwaambia kwamba hajivui magamba ng'o na kusema kuwa alitakiwa kujibu kwa hoja siyo blabla.

Bw. Azzan aliongeza kwamba nia yake ya kutaka sekretarieti hizo zijiuzulu ni kutokana na kwamba kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kimakosa ikiwa ni pamoja na viongozi hao kutotaka kuitisha mikutano ambayo watu watatoa dukuduku zao za namna ya kuboresha na kukiendesha chama.

"Tulikuwa tunatakiwa kufanya vikao tangu Novemba au Desemba lakini cha kushangaza mpaka leo hatujafanya kikao chochote, je, ni kwanini hawataki vikao hivyo vifanyike?.

"Sasa mimi ninasema kwamba wasipofanya vikao hivyo ndani ya mwezi huu ili viongozi watoe dukuduku lao juu ya kilichosababisha CCM kushindwa kufanya vizuri kwenye uchaguzi uliopita, nitaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuyaanika yale yote waliyoyafanya mpaka chama kikapoteza majimbo mawili na kata nyingi," alisema.
 
4 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Sema IDD AZZAN wananchi tunasubiri magamba ya CCM tuyaone.
April 19, 2011 9:44 PM
blank.gif

Anonymous said... CCM JIDHIBINI KUKIMBILIA VYOMBO VYA HABARI.MALUMBANO HAYAWASAIDII KITU ZAIDI YA KUKIDHOOFISHA CHAMA.CHAMA CHENU KIMEKUWA HAKINA NIDHAMU KUTOKANA NA KUPOKEA VIONGOZI/WANACHAMA NDANI YA CHAMA KWA NJIA ZISIZO SAHIHI NA WASO NA SIFA
April 20, 2011 12:56 AM
blank.gif

Anonymous said... Njoo CUF! wasikuzingue.
April 20, 2011 3:00 AM
blank.gif

Anonymous said... Sekretariati ya DSM, hiyo jeuri ya kung'ang'ania gamba wamepewa na mapacha watatu. Ila wanacheza makida makida, waendelee na kidali poo...HAWAONI SABABU YA UFISAFI..WAMECHAFUKA HADI DAMUNI
April 20, 2011 7:54 AM
 
Kajivua gamba lakini chatu yule yule
ban.kalamu.jpg


Samson Mwigamba​

amka2.gif
NILIVUTIWA sana na mnyama huyu mpaka nikaamua kumfuatilia kwa wataalamu wa wanyamapori baada ya kuponea chupu chupu kuuawa na mnyama huyu wa ajabu.
Nilikwenda porini alasiri ili kuchukua zamu ya kuchunga ng'ombe na kumpa nafasi babu yangu kwenda kufanya mambo mengine.
Ilikuwa ni Jumapili lakini sikumbuki tarehe wala mwezi wala mwaka ila nakumbua nilikuwa bado mdogo pengine nikiwa darasa la nne ama la tano hivi.
‘Nikapanda' ndege. Ilikuwa ikitokea ukaona kiota cha ndege tena mara nyingi chenye mayai (kuonyesha kwamba bado ndege huyo anaishi humo), unasema ume-pena.
Na mimi siku hiyo nikapena. Kazi iliyofuata ilikuwa ni kutafuta kimti chenye matawi ili hatimaye nitengeneze mtego wa kumnasa ndege wangu.
Nikatembea hadi chini ya mti uliokuwa kati kati ya nyasi ndefu kiasi tu, huku macho yangu yakiwa yameelekezwa juu ya mti kutafuta tawi lenye herufi Y kwa ajili ya kutegea ndege. Pale nilipoangalia sikuona, hivyo nikalazimika kutembea mbele ili niangalie upande wa pili wa mti ule.
Mwanzoni nilitaka kutembea tu macho yangu yakiwa yanaendelea kuangalia juu ya mti kadiri ninavyouzunguka nikitafuta hilo tawi. Baadaye mawazo yakanituma tu kuangalia kwanza chini kabla sijasonga mbele. Hamad! Nikakuta mzee chatu kajituliza vizuri kimya akiwa amejinyoosha kweli kweli tayari akisubiria niingie kwenye kumi na nane zake.
Niliruka na kupiga kelele ambayo sikuwahi kuitoa maishani mwangu. Babu alikuwa hajafika mbali akarudi kukata fimbo na kumchapa yule chatu akakimbia. Kimsingi kwenye ukoo wetu kwa mujibu wa tamaduni haturuhusiwi kumuua chatu.
Kama mimi nikimuua inabidi mtoto wangu atakayefuata aitwe jina lake mfano akiwa mwanamume ataitwa ‘Lusato' na akiwa msichana ataitwa ‘Nyasatu'. Vinginevyo kila mtoto atakayezaliwa atakufa. Hayo ni mambo ya mila na tamaduni tuachane nayo.
Ni baada ya hapo nililazimika kutafuta wataalamu wanieleze kidogo habari za chatu. Wakaniambia ni mnyama anayeishi kwa kumeza wanyama wenzake wadogo wadogo wakiwemo mbwa, mbuzi, swala, na wengineo akiwemo mwanadamu.
Ameumbwa kipekee sana maana akikukamata anaviringisha mkia wake kukuzunguka mithili ya mtu azungushiavyo kamba mzingo wake. Mwishoni kabisa mwa mkia wake kuna kifundo kigumu sana kiasi kwamba huweza kuufunga mkia wake kwenye mti ama kwenye kitu kingine chochote na hatimaye anaanza kuukaza kama unavyokaza kamba.
Kutokana na nguvu alizonazo, huweza kuvunja vunja mbavu na hatimaye kumuua kiumbe aliyemkamata. Baada ya kujihakikisha kwamba kiumbe kimekufa huweza kufyonza damu kutokea kwenye pua ya mzoga huo na kisha huanza kuulamba lamba mzoga na kwa mate yake kila kitu huteleza na hatimaye kuumeza mzoga huo mzima mzima.
Tumboni mwake ameumbwa na mimeng'enyo ya ajabu. Kila kiingiacho tumboni mwake huweza kuyeyuka na hakuna mfupa, nguo, jino, ama chochote kilicho kwenye mwili wa mzoga aliyemezwa na chatu ambacho hakitayeyuka.
Lakini je, akikutana na mnyama mwenye pembe kama swala, impala, ama nyumbu, hufanyaje? Katika mdomo wa chatu huweza kutoka dawa ambayo huitema pale zilipoota pembe na baada ya muda pembe huoza na kuanguka zenyewe huku chatu akiendelea na kazi ya kumeza mzoga wake. Lakini pia ana sifa nyingine.
Chatu hana masikio. Anasikia kupitia magamba yake yaliyo mwilini, hasa upande wa tumboni ambao ndio hukaa ardhini. Kinachotokea ni kwamba anasikia kwa mitetemo (vibrations).
Kwamba akiwa amejilaza mahali kama pale porini siku ile alipotaka kunimeza, kitu chochote kinachopita maeneo hayo mshindo wake husafiri kwa mitetemo kupitia ardhini na mitetemo ile hufika kwenye magamba ya chatu na yeye huweza kutafsiri ukubwa wa kiumbe anayepita.
Kwa hiyo akipita tembo huweza kujua kabisa kwamba hicho ni kishindo cha tembo na kwa kuwa hana uwezo wa kumkabili tembo, hukimbia asije akakanyagwa na kufa. Lakini akipita mbwa huweza kujua kwamba hicho ni kishindo cha mbwa na hatimaye kujiweka sawa ili kumnasa.
Na kwa wale waliowahi kuishi maeneo ya vijijini sana ama kupita pita maporini ambako kuna chatu, wamewahi kupita sehemu wakati fulani wakasikia harufu nzuri ya wali.
Huyo ni chatu. Akihisi anayepita ni mbwa na kwa kujua kwamba mbwa anapenda sana kula kula, basi huachama mdomo wake ambao hutoa harufu nzuri ya wali unaonukia.
Mbwa huweza kusogea mahali pale na hata anapoona kwamba kuna hatari ya chatu haamini kwamba sehemu yenye harufu nzuri kama hiyo inaweza isiwe jikoni bali machinjioni. Mbwa hushindwa kuamini hilo na kuendelea kusogea hatimaye kunaswa.
Sifa nyingine ya chatu ni kwamba akisha kula na kushiba huweza kuishi hata miezi bila kula tena. Kimsingi kama amemeza mbuzi mkubwa ama swala mkubwa anaweza kukaa hata miezi mitatu wanasema, bila kulazimika kutafuta chakula kingine.
Kuna suala moja ambalo sikuambiwa na wataalamu ila niliambiwa na wazee wa kijijini kwamba kuna wakati kama kameza ng'ombe mkubwa anaweza akabaki hapo mpaka mchwa wakajenga nyumba zao juu yake na wakasema mtu anaweza kumwona kama gogo lililokatwa muda mrefu.
Ni kutokana na hali hii kwamba chatu hufikia mahali ngozi yake ya juu ikazeeka na kuchakaa sana.
Anachokifanya chatu kama nyoka wengine ni kujivua gamba lake la juu na kumfanya ngozi yake imeremete tena katika rangi yake ya asili. Lakini jambo la mwisho kuhusu chatu ni hili: Chatu aliyejivua gamba ni mbaya zaidi kuliko mwenye gamba la zamani. Nitaeleza. Chatu mwenye gamba lililochakaa inawezekana alimeza mzoga mkubwa na sasa kalemewa na shibe mpaka amechakaa hapo alipo. Hajiwezi wala hawezi hata kukimbia. Ni rahisi kwetu wanadamu kumkamata na kumuua ili shibe yake itakapoisha asirejee kuua wanyama wengine wakiwemo wanadamu.
Lakini chatu aliyejivua gamba ni chatu ambaye huko nyuma alishakula tena vingi tu. Lakini labda mara hii akala mzoga mkubwa zaidi. Akashiba akalewa akabweteka hapo chini mpaka wanadamu wakamkuta.
Wakiwa hawajui kama ni chatu ama ni gogo wakaliwashie moto liteketee, wakiwa wanaligeuza geuza hilo ambalo wanadhani ni gogo, shibe ikaisha. Chatu akashtuka! Akakimbia mbio na akaenda kupita sehemu finyu sana na hatimaye akajivua gamba na kurudia ngozi yake ya zamani.
Anapojiangalia anajikuta bado ni yule yule tena mara hii ni mwepesi kuliko hapo nyuma kidogo maana chakula kimeisha tumboni. Sasa anaweza kukaa mahali akafunua tena kinywa ili kuwakamata mbwa kwa kuwadanganya na harufu nzuri ya wali.
Sasa ni mwepesi kuliko hapo zamani, anaweza kukimbia vishindo vya tembo lakini anaweza kujifunga mahali na kuwanasa mbuzi kwa urahisi kwa kuwaviringishia mkia na kuwabana mbavu.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejivua gamba. Kitendo cha mwenyekiti wake wa taifa kudai chama kimezeeka kinahitaji kujivua gamba ili kurudia upya kilinifanya nimkumbuke chatu na sifa zake kama nilivyoelezewa na wataalamu.
Wataalamu wanatofautiana na labda wataalamu wengine wa wanyama watasema baadhi ya sifa nimezikosea kidogo. Hilo halitanishangaza sana maana mimi si mtaalamu wa wanyama na nimefanya kuelezwa na kuna uwezekano mengine nimesahau ama kuyawasilisha isivyo.
Muhimu kwangu nataka uchukue ujumbe wangu nilionao kwako Mtanzania mwenzangu.
Chatu wetu mkubwa aitwae CCM amekula mizoga mingi aliyoitengeneza mwenyewe. Amemeza IPTL 1994 akashiba na kubweteka. Mwaka 1995 shibe ikawa imeisha akajivua gamba na kuonekana akimeremeta tena pale alipovaa ngozi ya ‘Mr. Clean'. Tukaambiwa sasa chatu kawa mpya tena na mwepesi zaidi.
Tukaambiwa tutarajie umezaji mpya hata wa swala na impala wenye pembe zilizojisokota. Kweli tulishuhudia umezaji mpya wa Deep Green Finance, Meremeta, Kagoda, EPA na kadhalika.
Kilichotushangaza wakati ule ni jinsi chatu wetu alivyokuwa akimeza na kukaa na mzoga tumboni siku chache tu anasikia tena njaa na kwenda kukamata mnyamna mwingine. Hata hivyo baada ya kuwameza wengi akaanza kuchakaa.
Ilifikia wakati mpaka tukadhani sasa 2005 chatu huyu mkubwa tunamkamata akiwa ameshiba mizoga yote hiyo na kumtupa nje (hatutaki kumuua).
Akashtuka, akajivua gamba. Akaja na "Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya". Akajivua na kumeremeta tena.
Walaku kama mbwa wakasikia harufu nzuri ya wali wakamsogelea chatu wakitikisa mikia na kubembeleza wapewe chochote. Ndio wakati tuliposikia maneno kama ‘Chaguo la Mungu'. Niliwahi kugusia hapa jinsi binti mmoja mwanahabari mwenzetu (jina nalihifadhi) alivyoandika makala akisema eti ‘CCM kwa kumpitisha Kikwete kugombea wamelamba dume'.
Kichekesho ni sababu alizozitoa. Akadai eti Kikwete ni rafiki wa waandishi wa habari. Eti hata usiku ukimpigia anapokea simu na kuongea na wewe kwa unyenyekevu. Akaenda mbali zaidi na kusema eti hata ukimbeep ama ukimwandikia sms kwamba ni mwandishi naitwa mfano, Amina, nina shida ya kuongea na wewe, basi Kikwete atachukua simu na kukupigia. Hizo ndizo sifa za rais bora kwa mujibu wa mwandishi yule.
Niambieni kama huyu si aina ya wale mbwa wanaovutiwa na harufu ya wali na kujipeleka kwa chatu. Sidhani kama Watanzania walikuwa wanataka rais ambaye atakuwa anatumiwa sms usiku na waandishi wa habari halafu ndo tumwone anafaa.
Gamba alilojivua chatu wetu 2005 lilikuwa ni zito mno na lilimweka chini akabweteka kwa muda mrefu sana ndiyo maana alipojivua akawa kama kawekwa huru na kuwa na ari mpya, na hiyo ikampa nguvu mpya na hatimaye kwa wepesi wa kuachana na gamba zito akawa kasi mpya!
Ni ari hiyo mpya, nguvu hiyo mpya, na kasi mpya iliyompelekea chatu wetu kushindwa kutambua vizuri vishindo vya wanyama wanaopita. Akajikuta anatafsiri vibaya kishindo cha Richmond/Dowans akadhani ni viswala kama Meremeta kumbe alikuwa ni tembo.
Hata hivyo kutokana na nguvu mpya aliyopata baada ya kujivua gamba lake, chatu wetu aliweza kummeza tembo. Lakini kwa kweli amechakaa haijapata kutokea.
Hakuna wakati CCM ilichuja kama wakati huu baada ya kummeza tembo Richmond/Dowans. Imechakaa mpaka watoto wa darasa la kwanza wanajua kwamba ni gogo. Mtoto wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anayesoma darasa la kwanza kaleta kizaazaa shuleni. Mwalimu aliingia darasani akiwa amevaa mavazi ya kijani, rangi ya CCM. Mtoto akapiga kelele akisema mwalimu kumbe na wewe ni fisadi!?
Mwalimu alipojaribu kujitetea mtoto akasema mbona umevaa nguo za mafisadi? Mimi sitaki kufundishwa na wewe, siwezi kufundishwa na mwalimu fisadi.
Si maneno yangu wala si maneno ya Mbunge Lema. Ni maneno ya mtoto wa darasa la kwanza aliyomwambia mwalimu mbele ya wanafunzi wenzake.
Akachukuliwa mpaka ofisi ya walimu akayarudia bila kukosea wala kumng'unya maneno. Chatu wetu amechakaa vilivyo. Kwa nini mwaka jana wanadamu (Watanzania) hawakumtupa nje ya pori? Ni swali letu sote. Lakini muhimu ni kwamba alitumia maarifa yake kuyeyusha kila kitu. Sasa anajivua gamba.
Kuna wasomi wakubwa wameshatoa maoni yao. Mara zote huwa napingana na mbwembwe nyingi zinazofanywa na CCM kuwahadaa ‘mbwa walaku' na mwishowe mnakuja kukubaliana nami. Nilieleza hapa pale mliposhangilia sana akina Anna Kilango waliposema wanapigana na mafisadi ndani ya chama chao na si kazi hiyo kufanywa na kina Zitto.
Leo mnakubali wenyewe walikuwa wanajivua gamba tu lakini chatu ni yule yule.
Wito kwa Watanzania wenzangu, chatu aliyejivua gamba ni mbaya zaidi kuliko aliyechakaa. Tumkatae, tumchape kwa fimbo nyembamba inayouma sana mpaka akimbie na tumtupe nje ya pori (tumng'oe madarakani).
Hatutamuua tusije tukalazimika kuwaita wanetu majina kama ‘dikteta' kama ambavyo Wajita hulazimika kuwaita Nyasatu. Hata hivyo tukimkosesha mizoga (ufisadi) atajifia mwenyewe.
Katika makala hii ukisahau yote kumbuka tu kwamba kajivua gamba lakini chatu ni yule yule. Tusimpe nafasi ya kutuhadaa mwaka 2015 kwa harufu za wali!
 
Hatari ya nyoka si gamba lake, ni sumu yake
ban.rais.jpg


Paschally Mayega​

amka2.gif
RAIS wangu, kuyaandika haya tunayoyaandika hatushawishiwi na chochote wala na yeyote, bali mapenzi mema kwa wananchi wenzetu, nchi yetu, kwa ajili yako rais wetu na kwa ajili yetu sisi wenyewe.
Hatumchukii mtu na wala hatumpendi mtu. Tumekosa faragha nawe, hii ndiyo faragha tuliyojaliwa.
Iko hadithi katika vitabu vitakatifu inayosema kuwa kundi la watu walimfumania mwanamke akifanya uzinzi. Wakamkamata wakampeleka kwa Bwana Yesu, wakisema, "Mwalimu huyu mwanamke tumemtoa sasa hivi katika uzinzi, unasemaje juu yake?" Bwana Yesu akawauliza, "Kwani sheria yenu inasemaje kwa mwanamke mzinzi?" Wakamjibu, "Anapigwa mawe hadi kufa."
Tunasoma kuwa Bwana Yesu aliinama chini akaandika, "Basi na asiye na dhambi kati yenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe!" Kila aliyeyasoma maandiko yale aliondoka zake taratibu. Bwana Yesu alipoinuka akamkuta yule mwanamke mzinzi amesimama peke yake. Akamuuliza, "Wako wapi wale waliokuleta?" Mwanamke mzinzi akajibu, "Wamekwishaondoka." Bwana Yesu akamwambia, "Basi na mimi sikuhukumu. Nenda zako lakini usifanye uzinzi tena!."
Wasiopenda kufikiri sana wanaweza kumwona Bwana Yesu kama anatetea wazinzi. Nimeuleta mfano huu hapa kwa sababu katika maandiko ya leo napinga mafisadi kuwapeleka mafisadi wenzao kwa wananchi ili wananchi wawahukumu.
Wasiopenda kufikiri sana wanaweza kudhani natetea ufisadi.
Rais wangu ni bahati mbaya sana kuwa hatujawahi kumuuliza nyoka kwa nini huwa anavua gamba lake. Anavua kwa sababu linakuwa limechakaa au hufika mahali likaanza kumwasha? Au ni utaratibu aliojipangia kuwa kila baada ya muda fulani anajivua gamba. Vyote iwavyo nyoka akijivua gamba hubaki nyoka yuleyule! Kama unadhani anakuwa tofauti akijivua gamba kamshike uone!
Hatari ya nyoka ni sumu yake si gamba lake.
Ndugu Rais, wakati mnavua gamba kule Dodoma ulisema, "Tumeanza kuchukua hatua na huu ni mwendelezo, tunaowatambua tuwabane kwa kuwataka wajiuzulu na pale wanapokataa tusichelee kuwawajibisha na hakuna tena sababu ya chama kusubiri ushahidi kama ilivyokuwa mwanzo."
Hivi kweli nchi inayoongozwa na utawala wa sheria mwananchi anaweza kuhukumiwa kwa kutuhumiwa tu bila ushahidi? Mmekuwa na mafisadi kwa zaidi ya miaka minne sasa. CCM ina serikali nayo serikali ina Jeshi la Polisi. Ina TAKUKURU. Ina Usalama wa Taifa. Ina Tume ya Maadili ya Viongozi.
Imeshindikana vipi kuwapeleka hawa watu mahakamani? Mnataka kutumia njia za majungu, ili kuficha nini?
Kama kweli sasa CCM imedhamiria kuwashughulikia mafisadi basi ianze na wale waliomo katika orodha ya aibu iliyotolewa Mwembeyanga na Dk. Willibrod Slaa, maana kuna ushahidi.
Kukukumbusha tu ndugu Rais, majina yaliyotajwa kwenye ile orodha ya aibu ambayo sasa CCM inakubaliana nayo ni marehemu Daud Balali, Basil Mramba, Gray Mgonja, Nazir Karamagi, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nimrod Mkono, Patrick Rutabanzibwa, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Edward Lowassa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
CHADEMA ina ushahidi dhidi yao itakaoutoa mahakamani kuthibitisha ufisadi wao. Katika hawa hakuna mwenye haki wala udhu wa kuwataka wenzake wajiuzulu nyadhifa zao au waondoke katika chama. Kulinda heshima yake awe wa kwanza kuondoka. Hakuna mtuhumiwa wa ufisadi atakayekubali kuondoka awaache wenzake.
Kutatokea mtafaruku mkubwa utakaokigharimu chama. Chama Cha Mapinduzi ni Chama tawala na kikubwa. Kikikatika na kugawanyika, nchi inaweza kukatika na kugawanyika. Baba unawapeleka wapi Watanzania?
Wakati yanatamkwa haya Dodoma huku kwingine wananchi wanaambiwa vingine kuwa akiwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Kikwete tarehe 10 Aprili,1990 aliingia mkataba wa madini na Kampuni ya SAMAX Ltd ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu wilayani Nzega, mkoani Tabora.
Maelfu ya wachimbaji wadogo wadogo waliondolewa kwa nguvu na FFU bila ya fidia yoyote. SAMAX Ltd waliuza eneo hilo kwa Kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana ambao nao waliiuzia Resolute Ltd ya Australia ambao ndio wenye mgodi ujulikanao kama Golden Pride.
Wanaendelea kuwahabarisha wananchi kuwa, Mheshimiwa Kikwete aliingia tena mkataba wa madini na Kampuni ya Kahama Mining Corporation Ltd, kampuni tanzu ya Kampuni ya Sutton Resources ya Canada ambayo ilivamia eneo la Bulyanhulu na kuwatimua wakazi wapatao laki nne. Sutton Resources iliwauzia Barrick Gold Corporation ya Toronto Canada Kwa dola za Marekani milioni 280.
Pamoja na kwamba Bulyanhulu ni moja kati ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika, lakini kutokana na mikataba mibovu ambayo Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja kuisaini, taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Tuhuma hizi nazo hazihitaji kusubiri ushahidi kweli?
Rais wangu, kama katika vichwa vya viongozi wapya wa CCM, ufisadi kwao ni Richmond, Dowans na Chenge pekee, na wala si pamoja na EPA, Kagoda, Deepgreen, Meremeta, IPTL, Loliondo na waliotumia fedha za walipa kodi kifisadi kama kujenga jengo la spika mahali pasipokuwa na spika na kuchukua posho na masurufu kwa mamilioni kwenda kutafuta ukweli na kisha kuficha nusu, basi CCM wanacheza mchezo wa patapotea. Na tayari wamekwisha pata, potea!
Ndugu Rais katika dhehebu langu muumini akifanya ufisadi kwa kuvunja amri za Mungu kuna kitu tunaita ‘kitubio'. Ni mahali fisadi (mkosefu) anakwenda, anatubu na kujutia yote aliyoyafanya na kuahidi kutorudia tena. Anapewa malipizi (adhabu) ya kufanya.
Kama aliiba anarudisha alichoiba. Akimaliza kufanya hayo yote anarudi kundini kumsujudia Mwenyezi Mungu pamoja na waumini wengine kwa upendo kama zamani, kanisa linasonga mbele. Wangekuwa wanatimuana kama CCM mnavyotaka kufanya, labda mpaka sasa kanisa lingebaki na Baba Mtakatifu peke yake.
Mnaowatuhumu, mmewapa nafasi ya kujutia makosa yao na kutubu? Waondoke waende wapi? Wakaanzishe mapambano sehemu nyingine? Nchi itabaki katika amani! Busara isipotumika tunaikaribisha vurugu.
Ndugu Wilson Mukama, Katibu Mkuu mpya wa CCM ana histroria ya kupelekwa pale paliposhindikana na akapanyosha. Anasema, "CCM inatakiwa kujengwa upya kabisa na ili hayo yaweze kufanikiwa kuna kila sababu za kuwa na watu safi, hivyo mimi nawataka ndugu zangu wasimame katika misingi ya zamani tuliyokuwa nayo katika chama chetu!"
Kauli yake hii inaleta faraja na matumaini mapya. Misingi ya zamani anayoisema katibu mkuu mpya, CCM mliiacha Zanzibar pamoja na Azimio la Arusha. Mlipoliacha Azimio la Arusha na miiko yake ya uongozi na kuasisi Azimio la Zanzibar ndipo mlipotenda dhambi ya mauti ambayo laana yake sasa inawarudi. Hakuna nchi yoyote duniani inaweza kuwa na uongozi bora bila kuwa na miiko ya uongozi.
Laiti kama Rais wangu angekuwa aliisikia sauti niliyoitoa katika makala ya BUTIAMA KUNA KABURI na kuchukua hatua muafaka, CCM leo isingefika hapa!
Niliandika nikiikumbuka siku Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa akizindua kitabu chake cha ‘Majukumu ya nchi za Kusini.' Nilipata bahati ya kualikwa nyumbani kwake Msasani. Akiongea kwa hisia kali, Mwalimu aliwalaumu na kuwashutumu waziwazi hadharani tena kwa maneno makali, waasisi wa Azimio la Zanzibar ambao wengi wao walikuwamo katika mkutano wa majuzi kule Dodoma.
Baada ya kuwatolea hizaya watu hao Mwalimu alionya, "....Najua mmekwishaiacha siasa ya ujamaa na kujitegemea na mtu kutaka kuisemea sasa itakulazimu uwe na moyo mkubwa kama wa mwendawazimu...Lakini ‘Paolo, Paolo' (Mwalimu aliita mara mbili kwa msisitizo)...na wengine, nawaambieni, mkilifuta kabisa Azimio la Arusha mtakuja kupata shida sana baadaye." Baba wa Taifa aliapiza!
CCM mmelifuta kabisa Azimio la Arusha, hofu imewasonga mpaka nafsini mwenu, mkondo wa maji unawasukumiza na laana juu yenu inakamilika! Ndugu Rais, mlitaka CCM mlaaniwe namna gani?
Niliyaunganisha maneno hayo na yale yaliyoandikwa ukurasa wa 80 katika kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu yasomekayo kuwa, "...Nayakumbuka vizuri sasa, maneno ya Mwalimu wangu aliyepata kusema, mkilifuta kabisa Azimio la Kijenge, mtakuja kupata taabu sana baadaye. Mwalimu aliona mbele na sasa yanatimia. Natamani angerudi ili airekebishe hali hii, maana pamoja na kwamba utawala wetu umefika ukomo lakini mwisho wake unakuwa mchungu kama shubiri. Mwisho wa maisha yetu ni mashaka matupu. Kwa hakika waasisi wa Azimio la mji Mkongwe watalaumiwa na vizazi vingi vijavyo kama vile waasisi wa Azimio la Kijenge watakavyotukuzwa milele."
Ole wake mtu yule atakayeenda Butiama bila udhu. Mwenye heri atakapojibu, Chama Cha Mapinduzi kitakohoa kutaka kutoa golegole la mafisadi lakini hakitaweza, hivyo kitagotea milele hadi kaburini. Na hapo ndipo waliyoyasema wahenga yatakapotimia, ‘kilichopatikana kwa hila kitaondoka kwa hila!'.
Ndugu Rais, baada ya kuliua Azimio la Arusha viongozi wetu mlianza mara moja kushirikiana na wafanyabiashara matajiri.
Mioyo yenu ikajaa tamaa ya mali. Kazi yenu kubwa ikawa kujikusanyia mali nyingi iwezekanavyo. Wakulima na wafanyakazi katika maudhui ya Chama Cha Mapinduzi wakawekwa kando.
Baadaye wafanyabiashara wakaacha kuwatumia nyinyi kama mawakala wakaingia wenyewe katika uongozi wa chama na serikalini. Chama kikabinafsishwa na kuwa mali ya wafanyabiashara matajiri na viongozi matajiri.
Mkawa wote mafisadi! Mkaikamilisha ile dhambi kubwa, kupanua zaidi pengo kati ya walionacho na wasionacho. Na kwakufanya hivyo mkaistahili laana!
Baba Kikwete ni nani aliye msafi ndani ya CCM wa kustahili kuwahukumu wengine? Mwalimu Mkuu wa Watu uk. 61 tunasoma, "Waziri mkuu alifikia mahali akawa hajiwezi tena, akalia kwa sauti akisema, "Ee, Baba uliyewatuma manabii na mitume wako nasi tukawapuuza, kama hutatusamehe, ukatuhesabia makosa yetu yote, kati yetu sisi nani atasimama?" Wakuiona pepo watakuwa wachache!" Busara ni maridhiano. Kutangaza vita nyakati zetu hizi ni upunguani.
Rais wangu mwombeni Mwenyekiti wenu wa CCM wa wakati ule, Ali Hassan Mwinyi, awarudishe Zanzibar akingali hai, mkalichukue Azimio la Arusha mlikolitelekeza na miiko yake ya uongozi. Katika kufanya hivyo mtakuwa mnamsaidia na yeye mwenyewe kuwa na cha kumjibu Muumba wake siku yake ya kusimama mbele ya haki itakapofika. Lazima ataulizwa kwa nini alilifungua fundo lililokuwa limewaunganisha waja wake!
Tunachoshuhudia leo ni viongozi wa CCM kuanza kuhubiri chuki ndani ya chama chao badala ya upendo. Wanaunda mfarakano badala ya mshikamano. Undugu kati yao aliowaachia Mwalimu Nyerere umepotea! Uchungu wa muasisi huko alikolala unawatafuna nao wanatafunana. Wanatangaza vita badala ya amani. Wamesahau kuwa vita haijawahi kuwa suluhisho la amani hata siku moja popote duniani!
Wakati CCM mmeanza kugombana CHADEMA wanashika kasi. Alipohutubia mkutano wa hadhara mkoani Kilimanjaro wakati wa kampeni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alinukuliwa akisema, "Hawakuwaahidi kuiba bilioni 40 kupitia kampuni yao ya Kagoda lakini wameiba. Ushahidi tunao…na ndio maana Kikwete hachukui hatua. Kikwete atapata wapi ujasiri wa kutueleza wezi wetu wakati fedha hizo walizoiba Benki Kuu ndizo zilizomwingiza Ikulu?"
Rais wangu huoni kuwa vita inayotangazwa ndani ya CCM itawaathiri zaidi wanaoitangaza kuliko wanaolengwa? Baba itawezekana vipi mfanye juhudi pamoja mpaka muichukue nchi halafu msishirikiane kurudisha nguvu zenu na kufanya mipango ya kujiletea hali bora zaidi huku mkiufaidi utawala wa nchi mlioupata kwa nguvu zenu kwa pamoja? Watanzania wa leo ni waelewa! Lazima mtoke wote. Mmoja mmoja hatoki mtu labda kama walivyosema wabunge wetu kule Dodoma, ‘fungeni milango mpigane'. Watawala wetu ndio chimbuko la ufisadi. Kuwaondoa mafisadi lazima kwanza uondoe muhimili wa ufisadi ambao ni serikali.
Ndugu Rais, kwa kuwa binadamu uhesabiwa kwa vichwa vyao, kichwa cha serikali ni rais. Je, ni kweli watu wako tuwaache waamini kuwa rais wao ndiye chimbuko na muhimili wa ufisadi katika nchi yao? Baba kwa nini usinipatie faragha tukaliweka hili jambo sawa sawa pamoja kwa kauli tu! Mmejaribu kuanzisha vita hewa ya udini mmeshindwa.
Sasa mmeikarabati vita hewa ileile iliyoshindwa dhidi ya ufisadi. Lini wananchi wataachwa wafanye kazi za kuwaletea maendeleo? CCM mkianza kugombana nchi itaingia katika machafuko. Watakaoumia zaidi ni wananchi!



h.sep3.gif

Simu: 0713334239
 
Mbatia: Malumbano yasipewe nafasi


na Irene Mark


amka2.gif
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewashauri wanasiasa kuacha malumbano yasiyo na tija, badala yake kujadili sababu za umaskini wa Watanzania na jinsi ya kuondokana nao.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mbatia alisema malumbano ya kuua vyama ama kashfa zenye lengo la kudhoofisha nguvu za wanasiasa sio ajenda muhimu itakayowasaidia wananchi badala yake washirikiane kupunguza pengo kati ya tajiri na fukara.
Katika mazungumzo hayo, mwenyekiti huyo aliyekuwa mgombea ubunge wa Kawe, alitaka siasa za kuchafuana ziwekwe kando ili kupisha muda wa kujadili hoja za msingi za kuwanasua wananchi kwenye lindi la umaskini na ufukara.
“Nawaomba wanasiasa wenzangu wa vyama vyote bila kujali awe Katibu Mkuu wa CCM Willson Mukama au CHADEMA kuachana na malumbano; umefika wakati wa kujadili mambo yanayowakabili wananchi hususan umaskini.
“...Hivi sasa ukitizama daraja la wenye nacho na wasio nacho limekuwa kubwa mno, mfumko ya bei kila siku, maisha yamekuwa magumu kwa wananchi hivyo mambo ya kujigamba eti wanasema wamekuja kuua upinzani hayana tija. Tuangalie namna ya kulikomboa taifa hili tuumizwe na umaskini wa watu wetu,” alisema Mbatia.
Mwenyekiti huyo pia alisema taifa linakabiliwa na changamoto nyingi za malengo nane ya milenia likiwemo umaskini ambapo hivi sasa fedha ya Tanzania inashuka thamani ikilinganishwa na dola ya Marekani.
 
CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan Send to a friend Thursday, 21 April 2011 08:17

Geofrey Nyang'oro, Singida
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi.

Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake.

Dk Slaa alisema chama chake kina shaka na wingi wa fedha alizonazo kijana huyo na kwamba atahakikisha kwamba kigogo huyo anaiambia Chadema na Watanzania alipozipata.

Alisema kijana huyo alimaliza masomo yake muda mfupi uliopita, lakini tayari amekuwa bilionea akisisitiza kuwa chama chake kitahoji alipopata mabilioni hayo.

"Ninajua kwamba ana fedha nyingi, lakini huyu alikuwa mtoto wa shule juzi tu. Leo amekuwa bilionea! Atatuambia amepata wapi hizo fedha, Chadema tutahoji ni wapi amezipata," alisema Dk Slaa.

Dk Slaa pia alizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi na kusema watahakikisha halali.

Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alitoa kauli hiyo alipozungumzia ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema umeimarisha ngome ya upinzani bungeni.

"Rais Kikwete alisema kelele za upinzani hazimnyimi usingizi, lakini kwa kumchagua Lissu mmeongeza nguvu ya upinzani na sasa hatalala," alisema na kuongeza:

"Ujumbe wangu kwenu ni kwamba sasa mmemchagua mbunge jasiri anayeweza kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbele ya Waziri Mkuu kuwa amekuwa mvivu kusoma."

Alisema kutokana na ujasiri huo wa Lissu sasa miswada mibovu haitapelekwa bungeni.

Awali, akizungumza katika mkutano huo, Lissu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo akisema kuwa ni mara ya kwanza fedha hizo kutengwa huku akijigamba kwamba ni kutokana na wapinzani kubana mianya ya wizi.
 
Nape: Vita ya mafisadi sasa inahamia kwa vigogo serikalini Send to a friend Thursday, 21 April 2011 08:54

*Asema ni pamoja na mawaziri wasiotekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo
Tumaini Msowoya, Iringa

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema vita dhidi ya ufisadi sasa inahamia kwa watendaji wa Serikali wakiwamo mawaziri ambao watashindwa kutekeleza Ilani ya chama hicho kwa vitendo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema mkakati wa chama sasa ni hakuhakikisha kuwa mafisadi hawana nafasi tena kwenye chama hicho na Serikali yake.

"Tumekuwa tukisema kwamba vita ya ufisadi haitaishia kwa watendaji wa chama tu. Itakwenda hata kwa watekelezaji wa Ilani ya CCM. Tutahakikisha kila anayepewa jukumu la kutekeleza ilani yetu, anawajibika," alisema Nnauye.

Alipotakiwa kufafanua aina ya watendaji anaowalenga katika vita hiyo, Nape alijibu: " Nasema wote, hata kama ni mawaziri au wakuu wa mikoa kwa sababu tunapoingia kwenye uchaguzi, siyo wao wanaokinadi chama. Huu ni wajibu wa kuhakikisha ilani yake inatekelezeka ili tunapokuja kwenye chaguzi kisipate pingamizi."

Kauli hiyo ya Nape ni msisitizo wa kile alichokisema juzi kwenye mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Ofisi za Chama hicho, mkoani Iringa.

Katika mkutano huo, Nape alisema baada ya kumaliza vita dhidi ya mafisadi walioko ndani ya CCM, hatua inayofuata ni kwa viongozi wa Serikali wa ngazi zote ambao wamekuwa wakikisaliti chama hicho kwa kujifanya miungu watu.

Nnauye alisema suala la kujivua magamba linapaswa kuanza kufanyiwa kazi katika ngazi za wilaya na kwamba, ikiwa viongozi hao hawataamua kujiondoa wenyewe, wataondolewa kwa nguvu.

"Hatua inayofuata ni ya viongozi wa Serikali ambao ni wasaliti, wale ambao badala ya kutekeleza ilani ya chama chetu wanatekeleza ilani za matumbo yao. Hatutakubaliana na jambo hilo na hili lazima lifanyika kabla ya mwaka 2015," alisema Nnauye.

Alisema wanachama pia watapatiwa nafasi ya kuwataja watu ambao wamekuwa wakichangia kukiangamiza chama hicho, wakiwemo mafisadi na wala rushwa.

Aliwataka viongozi wa CCM, kuanzia ngazi za mikoa, wilaya, kata na matawi kujitathmini wenyewe na hatimaye kujivua madaraka ikiwa wamekuwa wakitajwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi ambazo ndizo zilizokibebesha chama hicho mzigo mkubwa.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati alisema chama hicho kimetambua kuwa kilifanya makosa na hivyo kimejirekebisha ili kurudisha hadhi yake kwa wananchama.

"Kuna watu wameibebesha CCM mzigo mkubwa ambao umekigharimu, sasa hivi tunarejesha chama kipya ambacho kigezo cha uongozi au ujumbe wa NEC hakitakuwa fedha tena...." alisema Chiligati.

Katika mkutano huo wa Iringa Mjini, zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu mbalimbali mkoani hapa walijiunga na CCM kwa madai ya kufurahishwa na hatua ya kukibadilisha chama hicho na baadhi ya viongozi wa juu kujivua gamba.

Wakizungumza baada ya kupokea kadi za chama hicho, wanafunzi hao walisema walikasirishwa na baadhi ya vitendo vilivyokuwa vikifanywa na watu wachache ndani ya chama hicho, ndiyo maana waliamua kupigia debe vyama vya upinzani.

Walisema wana uhakika kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa ndiyo sababu kubwa ya kulipoteza Jimbo la Iringa Mjini ambalo hivi sasa linaongozwa na Mbunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Comments




0 #7 SOSTENES GALUS MITTI 2011-04-21 10:17 Kaka yangu NAPE, hata UKIFA au KUACHA siasa umesha tuonyesha WATANZANIA kuwa VIJANA TUNAWEZA nasi tunajivuna kuwa nawe, kwani HAUOGOPI VITISHO vya hao MAFISADI na MAWAKARA wao, mungu akuzishie nguvu na HEKIMA na pia MOYO WA UPENDO KWA WATANZANIA WENGI WETU TULIO MASIKINI.......KAZA BUTI USIMWANGALIE MTU USONI
Quote









0 #6 mkereketwa 2011-04-21 10:10 kwani huyu RIDHIWANI anayemiliki mabilionea wakati amemaliza chuo hivi karibuni amepata wapi huo utajiri mkubwa namna hiyo ,si ni mwanachama wa ccm,si ni mtoto wa kikwete.sasa vita dhidi ya mafisadi iko wapi hapo.mnajiosha au mnazidi kujichafua zaidi.mimi nafikiri mgeanza na Jk.
Quote









0 #5 mkereketwa 2011-04-21 10:10 kwani huyu RIDHIWANI anayemiliki mabilionea wakati amemaliza chuo hivi karibuni amepata wapi huo utajiri mkubwa namna hiyo ,si ni mwanachama wa ccm,si ni mtoto wa kikwete.sasa vita dhidi ya mafisadi iko wapi hapo.mnajiosha au mnazidi kujichafua zaidi.mimi nafikiri mgeanza na Jk.
Quote









0 #4 Amini 2011-04-21 10:09 Nnauye na viongozi wangu wapya wa ccm,itabidi mfanye kazi kubwa na ziada kwani katika kukisafisha chama mtakutana na Visiki na Vigogo ambavyo msipokua navyo makini katika kuving'oa mnaweza mkajikuta vinang'oka na ninyi!,sifa mbaya ya mti mkubwa unapoanguka huangukia miti mingine mingi midogomidogo.
Quote









0 #3 Vincent A 2011-04-21 10:08 Ugawaji wa viwanja katika Halmashauri ya Arusha hususani vile vya BURKA uligubikwa na kiwango cha juu cha rushwa na wananchi tunaona kama vile tulitapeliwa. CCM ikirekebisha hili tutarudisha imani kwao
Quote









0 #2 mbiligi 2011-04-21 09:52 matendo ndio tunayasubiri, tumechoshwa na ahadi.
Nape punguza domo, utaumbuka kama yatashindikana
Quote









0 #1 abdalah 2011-04-21 09:22 Pole Tanzania yangu. Bado utaendelea kuwa shamba la Bibi sijui mpaka lini?
Quote







Refresh comments list

Add comment
 
Dk. Slaa afichua mabilioni ya Rostam
• Asema anapokea bil. 280/- kwa mwaka, ataka akamatwe

na Joseph Senga


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mapato ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kwa kile alichodai yana uhusiano mkubwa na ufisadi.
Dk. Slaa aliyasema hayo juzi jioni katika mkutano wake mjini Igunga, mkoani Tabora katika mwendelezo wa ziara zake.
Alisema mapato ya Rostam kwa mwaka yanafikia sh bilioni 280, hivyo TAKUKURU haina budi kumkamata na kumchunguza kwani aliwahi kutangaza kuwa hana shida ya kuwa kiongozi au kung'ang'ania madaraka yoyote, kwani pesa alizonazo zinamtosha.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa TAKUKURU haitamchukulia hatua Rostam, atawashawishi wananchi kutotoa ushirikiano wowote kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwazomea maofisa wake kila wanapowaona.
Akifafanua tuhuma hizo za ufisadi, alisema kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
Alisema kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa na nia ya kweli angemshirikisha kuwakamata mafisadi badala ya kuwapa siku 90 kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, ikiwa Kikwete amewapa mafisadi hao siku hizo kuondoka ndani ya chama pamoja na kuachia ubunge, naye hana budi kujipa siku hizo, kwani naye ni fisadi.
Alisema kujitokeza kwa mmiliki wa Dowans Brigedia Jenerali (mstaafu), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ulikuwa ni usanii wa picha ya Rostam kwani baadaye ndiye atakayelipwa fedha hizo za Dowans.
Alisema CHADEMA haitakubali fedha hizo zilipwe na kwamba itaitisha maandamano nchi nzima kupinga.
Dk. Slaa alisema ufisadi mwingine wa serikali katika sakata hilo la Dowans ni serikali kuweka mawakili watatu kinyemela na kupanga kuwalipa sh bilioni tano.
"Nilimtaja Rostam kuwa ni mmoja wa mafisadi kule Mwembeyanga, naye alinitumia vitisho kwa ujumbe mfupi kuwa nina sekunde chache za kuishi hivyo nipige magoti, nisali. Nilimjibu na nasema …nilizaliwa siku moja na nitakufa siku moja, sitaogopa kusema ukweli," alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema moto uliowashwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) umeifanya serikali ya CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kushindwa kulala.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungi katika Jimbo la Singida Mashariki jana aliposimama kuwasalimia wakati akitokea Singida kuelekea Dar es Salaam, Dk. Slaa alisema Lissu ni mbunge jasiri katika Bunge ambaye amediriki kumnyooshea kidole hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.
Katika hotuba yake hiyo alisema wananchi hawana imani tena na serikali ya Jakaya Kikwete na kama atafanya mchezo hataweza kurudisha imani hiyo wala kumaliza kipindi chake cha utawala.
Alisema mambo mengi yamejitokeza ambayo yamesababisha wananchi kukosa imani naye, yakiwamo ya ufisadi unaofanywa na yeye mwenyewe pamoja na watu walio karibu naye.
"Wananchi wanaona yanayofanyika, mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete, amemaliza shule hivi karibuni lakini leo ni bilionea. Haya yote hayawezi kuvumilika hata kidogo."
Akiwashukuru wananchi wa kijiji hicho, Dk. Slaa alisema si tu kwamba wamemchagua mbunge wa Jimbo la Singida, bali ni mbunge wa nchi nzima na kwamba ni nyundo itakayotumika kuwaponda CCM.
Akizungumzia suala la CCM kujivua gamba, alisema neno fisadi alilianzisha yeye na chama chake na kwamba anayepaswa kujivua gamba hilo ni Kikwete halafu awavue wengine.
 
Mali za CCM zazua balaa Moshi


na Grace Macha


amka2.gif
MGOGORO wa kugombea mali za Halmashauri ya Moshi zinazodaiwa kumilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana ulichukua sura mpya baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadette Kinabo, kususia ajenda hiyo na kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi wakati wa kikao hicho maalumu na kuwalazimu madiwani wa CHADEMA kumchagua katibu wa muda wa kuendesha kikao hicho.
Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya halmashauri, nje ya eneo hilo na mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi polisi waliweka ulinzi mkali na kufunga barabara kwa kile kilichoelezwa kuwa walihofia vurugu zingetokea.
Kikao hicho awali kilikuwa kifanyike Machi 31 mwaka huu lakini kilishindikana baada ya Mkurugenzi huyo kukiahirisha kwa kile alichoeleza kuwa kungeweza kutokea kwa vurugu.
Mkurugenzi huyo ambaye ni katibu wa kikao hicho alitoka wakati walipokuwa wakithibitisha ajenda za kikao hicho ambapo alitaka ajenga namba 7 iliyokuwa inahusu kujadili majengo ya manispaa hiyo yanayokaliwa na CCM isijadiliwe kwani tayari alikuwa na maagizo ya mahakama (court order).
Kinabo alisema barua hiyo ya mahakama aliipokea siku iliyopita saa tisa alasiri, hivyo akataka kikao hicho kisijadili hoja hiyo, ambapo Meya wa manispaa hiyo, Jafar Michael, aliyekuwa akiendesha kikao hicho aliamua kusikiliza maoni ya madiwani.
Mwanasheria wa halmashauri hiyo ambaye ni mgeni aliyetambulishwa kwenye kikao hicho, Deograsius Nyoni, aliwasomea madiwani ‘oder' hiyo iliyoweka zuio la kuhamisha au kuharibu mali kwenye viwanja namba 54 Block BBB na namba 19 Block B, ambavyo vinakaliwa na CCM.
Alisema shauri hilo linalosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Stella Mgasha, lilifunguliwa Aprili 13 mwaka huu na bodi ya wadhamini wa CCM kupitia mwanasheria wao, Beth Minde, ambapo mshitakiwa pekee kwenye shauri hilo ni mkurugenzi wa halmashauri.
Alifafanua kuwa CCM iliomba malalamiko yao kusikilizwa kwa shauri hilo kwa hati ya dharura ambapo mahakama iliyasikiliza Aprili 14, mwaka huu sasa 8 mchana lakini usikilizwaji huo ulifanyika kwa upande mmoja.
Alisema kuwa maombi hayo ya CCM yaliyowasilishwa mahakamani yalilazimika kusikilizwa kwa haraka kuhofia maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Moshi kilichokaa jana Aprili 20, huku mwanasheria akitaka kutojadiliwa kwa ‘oder' hiyo ya mahakama.
Mwanasheria huyo alifafanua kuwa ‘oder' hiyo inaelekeza kutofanyika kwa shughuli yoyote kwenye viwanja hivyo ambavyo kesi ipo mahakamani.
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi, madiwani walitakiwa wajadili kwa pamoja juu ya kuondolewa kwa hoja namba 7 kwenye kikao hicho, hali ambayo ilikuwa vigumu kwa madiwani wa CHADEMA kukubali maamuzi hayo ya mkurugenzi ya kuondolewa kwa hoja hiyo huku wakitaka badala ya kujadili ajenda hiyo basi wajadili ‘order' iliyotolewa na mahakama ili waone namna watakavyokabiliana na kesi hiyo.
Pia madiwani walihoji juu ya kutopatiwa ‘oder' hiyo siku iliyopita kwani walikuwa kwenye kikao cha awali cha baraza la madiwani ambacho kilidumu mpaka saa 12 jioni kama kweli mkurugenzi alipata barua hiyo saa 9 alasiri.
Baada ya kutoa maelezo ya kuondolewa kwa hoja namba 7, mkurugenzi huyo alisema kuwa yeye ndiye mtendaji wa serikali na anachotaka ni vikao hivyo vifuate utaratibu na hatimaye kunyanyuka na kutoka nje ya kikao.
Baada ya mkurugenzi kutoka nje na kufuatiwa na wataalamu wa halmashauri na madiwani wa CCM, madiwani wa CHADEMA waliendelea kukaa ndani ya ukumbi huo wakijadiliana ni nini kifanyike ili waweze kuendelea na kikao.
Baada ya kujadiliana walikubaliana kuahirisha kikao kwa muda ili wamwandikie barua mkuu wa mkoa aweze kuwapatia katibu atakayeweza kuendelea na kikao. Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita waliingia kwenye ukumbi majira ya saa saba mchana na kuendelea na kikao.
Meya huyo alisema baada ya kupitia kanuni za kudumu za halmashauri hiyo walibaini kuwa wanaweza kuendelea na kikao kwa kuchagua katibu wa muda baada ya kubaini kuwa hakuna kifungu kinachowazuia kumchagua katibu au kutomchagua.
Alisema kuwa madiwani ndio wenye maamuzi ya kuweka hoja na kuiondoa na katika kikao cha baraza walitaka kupitisha maazimio ya kufuta maazimio ya awali yaliyotolewa ya kuwamilikisha CCM majengo ya halmashauri.
Hoja iliyotakiwa kuondolewa ni ile ya kujadili viwanja viwili, kiwanja chenye namba 056038/94 ilipo ofisi ya wilaya ya CCM na namba 15686 ilipo ofisi ya UVCCM mkoa.
"Lengo la Mkurugenzi kutoka nje ya kikao ni kutaka CHADEMA waonekane kuwa wana vurugu na sisi hili tutaliepuka, na baada ya hapo endapo akifanikiwa kwa kisngizio hicho basi baraza hili la CHADEMA livunjwe ...lakini CHADEMA kwa hili hatupo tayari," alisisitiza Jafari.
Katika kikao hicho ambacho walimchagua Diwani wa Kata ya Longuo B, Raymond Mboya, kuwa katibu wa muda, walipitisha maazimio matatu, ikiwemo madiwani kuwa sehemu ya kesi iliyofunguliwa na CCM dhidi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Diwani wa Kata ya Bondeni, Abdulrahman Sharif, alisema lengo ni kumdhibiti mkurugenzi kwa kuhofia kufikishwa mahakamani na kukubali kuwa mali hizo ni za CCM pamoja na kumtafuta wakili kwa ajili ya kesi hiyo.
Azimio jingine walilolipitisha ni la kumpeleka mkurugenzi kwenye kamati ya maadili kwa kile walichoeleza kuwa ni kudharau kikao kwa kutoka na watendaji na kumuacha mweyekiti huku kikao kikiwa bado kinaendelea, ambacho kitakuwa na wajibu wa kupeleka mapendekezo kwa mwajiri wake au waziri mwenye dhamana kwa ajili ya utekelezaji.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, alisema mkurugenzi huyo alitoka nje kwa hoja kuwa ‘order' ya mahakama haipaswi kujadiliwa lakini maelezo hayo hayana hoja, kwa sababu kilichotaka kufanywa si kujadili ‘order' bali kujadili jinsi ya kukabiliana na kesi hiyo.
Ndesamburo alisema kulikuwa na haja ya kujadili juu ya kuweka wakili kwenye kesi hiyo ambayo walisema hawataki kutumika kwa mwanasheria wa halmashauri hiyo, ambaye ndiye kwanza wamemuona jana pamoja na kumuweka kando mkurugenzi kwenye suala hilo baada ya kuonekana kuwa na masilahi binafsi.
Polisi wengi wenye silaha walionekana maeneo ya kuzunguka halmashauri hiyo huku Barabara ya Florida inayotumiwa kuingia kwenye jengo la mkuu wa mkoa, manispaa na kituo cha uwekezaji nchini (TIC) zikiwa zimefungwa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 8:30 mchana.
Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kuwa barabara hiyo inatumika kuelekea maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na viunga vyake.
Kwa upande wake, Kinabo akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baadaye, alisema kuwa aliamua kutoka kwenye kikao hicho baada ya kuona hapewi nafasi ya kuongea pamoja na madiwani wa CHADEMA kuamua kujadili ‘oder' ambayo kisheria hairuhusiwi kujadiliwa.
 
Rostam, Ridhiwan wachunguzwe

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
MOJA ya habari za gazeti hili leo, inahusu taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kuhusu mapato makubwa anayodai kuyapata Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, mbunge huyo anapata mapato ya takriban sh bilioni 280 kwa mwaka.
Katika tamko lake alilolitoa akihutubia wananchi jimboni kwa mbunge huyo Igunga Tabora, Dk. Slaa ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ichunguze mapato ya mbunge huyo, kwani yana uhusiano mkubwa na ufisadi.
Itiliwe maanani kuwa Dk. Slaa alitoa hoja na angalizo hilo, akirejea kauli ya Rostam mwenyewe aliyowahi kuitoa akisema hana shida ya kuwa kiongozi au kung'ang'ania madaraka yoyote kwani pesa alizonazo zinamtosha.
Izingatiwe kuwa katika maelezo yake hayo, Dk. Slaa alibainisha kuwa kati ya makampuni 17 yanayosemekana kuwa ni ya Rostam hakuna jina lake hata moja.
Kwa hiyo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapaswa kumkamata mbunge huyo na kumchunguza kwani kiwango na uhalali wa mapato yake vinatia shaka.
Kwetu mtazamo wetu, tamko na hoja za Dk. Slaa zinapaswa kufanyiwa kazi na TAKUKURU kwani ni moja ya majukumu yao kufanyia kazi taarifa mbalimbali zinazohusiana na rushwa au ufisadi.
Tuhuma hizo ni nzito hasa tukirejea tuhuma nyingine mbalimbali ambazo mbunge huyo amekuwa akihusishwa nazo, ikiwa ni pamoja na zile za Kampuni hewa ya Kagoda, EPA, Dowans na nyinginezo.
Tunaona TAKUKURU ina kila sababu ya kuzifuatilia tuhuma hizo kwani hata mbunge huyo ametajwa kuwa mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi waliokichafua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kukipotezea imani kwa wananchi.
Tunaishangaa taasisi hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua zilizo ndani ya majukumu yake ilhali mtuhumiwa huyo na wengineo wameshatolewa maelezo ya kutosha hata kufikia hatua ya kuonekana kuwa ni tatizo ndani ya chama chao cha siasa.
Aidha, tuhuma nyingine nzito iliyotolewa na Dk. Slaa ni ile inayohusu utajiri wa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete aitwaye Ridhawan Kikwete, kwamba hivi sasa mtoto huyo ni bilionea wakati ni juzi juzi tu alitoka shule.
Sawa na Rostam na watuhumiwa wengine wote wa aina hiyo, tunaitaka TAKUKURU na vyombo vingine vyote vinavyohusika kumchunguza Ridhiwan Kikwete bila kujali kuwa ni mtoto wa Kiongozi Mkuu wa nchi, kwani huenda mapato yake makubwa (kama ilivyoelezwa) yamepatikana kwa rushwa na ufisadi.
Ieleweke kuwa tunaposema watuhumiwa hao wachunguzwe tunamaanisha kuwa uchunguzi huo pia uhusu taarifa zenyewe zilizotolewa na Dk. Slaa na kisha kuchukua hatua zaidi kuhusiana na taarifa hizo.
Tunasisitiza kuwa tuhuma zote hizo ni nzito, zichunguzwe kwa masilahi ya taifa.
 
Kiongozi UVCCM ataka mafisadi wafilisiwe


Na Martha Fataely, Moshi

SERIKALI imeombwa kwenda mbali zaidi katika vita dhidi ya ufisadi kwa kuhakikisha inawadhiti, kuwafilisi na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wanaotajwa kwani ni
sawa na wahujumu uchumi.

Mjumbe wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Paul Makonda aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo pia alitaka utajiri wa wanachama wa CCM wahojiwe jinsi ambavyo wamepata mali hizo.

Madai ya Bw. Makonda yamekuja siku chache baada ya viongozi wa CCM kutoa taarifa zinazotatanisha, baadhi wakidai kuwa kwenye vikao vyake watu watatu walitajwa kuhusishwa na ufisadi na kupewa siku 90 kupima wenyewe na kuachia nyadhifa zao, huku wengine wakisema hayakutajwa majina wala orodha ya watuhumiwa hao

Bw. Makonda katika taarifa yake aliomba serikali iwahoji aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Mwasheria Mkuu wa Serikali, Bw Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Azaz ili kujua wamepata wapi utajiri walionao.

Bw. Makonda alisema watuhumiwa wote waliotajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya nchi,wafilisiwe ili kuhakikisha rasilimali walizopora watanzania zinarejshwa.

Alisema pamoja na Kamati Kuu ya CCM kutoa muda wa siku 90 kwa watuhumiwa wenyewe kujivua nyadhfa zao lakini, ni vyema kwa serikali ikawafilisi ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu ya kujilimbikizia mali.

“Hawa wote wamechafuka na wananchi wanawatuhumu wanapaswa kufukuzwa CCM ikiwa ni pamoja na hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa dhidi yao kwani wao ni majeruhi,” alisema.

Alisema wapo baadhi ya vigogo ambao wana utajiri wa kutisha hapa nchini wakati waliwahi kushika nyazifa mbalimbali hapa nchini lakini pia wamekuwa wakihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

“Tunaomba watu hawa wafilisiwe, utajiri wao uhojiwe kwani wameweza kuliingiza taifa katika mikataba feki mbalimbali wakati wakiwa na nyazifa za uongozi serikalini,” alisema.

Aidha Bw. Makonda ameendelea kutoa madai mazito kwa viongozi
wa UVCCM, Mwenyekiti Beno Malisa, James Millya, Hussen Bashe na Martine
Shighela, ambao alidai ni vibaraka wa watuhumiwa hao.

Bw. Makonda aliongeza kuwa iwapo Bw. Lowassa aliwahi kujiuzulu katika kashfa ya Richmond, mapema wakati bunge likiendelea na mjadala, basi anatakiwa kufanya vivyo hivyo katika hatua hii, pamoja na watuhumiwa wengine wote.

Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa UVCCM, Bw. Beno Malisa, alipohojiwa alisema masuala ambayo yanaigusa taasisi yatajibiwa na taasisi husika na mengine anayozungumzia vijana Bw Makonda atajibiwa na vijana wa saizi yake.

“Ah sasa tusipoteze muda, huyo kama amezungumza hivyo,subiri atajibiwa na taasisi anazozitaja….mengine pia atajibiwa na vijana wa saizi yake, we chukua hilo ndiyo jibu sasa, au unataka jibu unalotaka wewe?" alihoji.
 
7 Maoni:


franco said... BONGO BWANA DOWANS NDIO TATIZO NA NI LAZIMA LILIPWE KWA SABABU MKATABA UPO NA YOTE HAYO NI MATUNDA YA CCM,MHASIBU WAO MKUU ALITUMIA PESA YAKE KWA PILAU NA POSHO SASA NDIYO MATUNDA YAKE.
HIVI DUNIANI KUNA MTU ANAYETOA PESA BILA KUPATA FAIDA SASA CCM MJUE WALE WALIOWAPA PESA ZA UFADHILI NDIO WANAZIRUDISHA.
TUNASUBIRI TUONE MATOKEO YA KUWANYANG'ANYA MALI ZAO HAYA WEEE
May 6, 2011 12:07 AM
blank.gif

Anonymous said... Kweli hii ni bongo,Mkama alisema hawana orodha ya mafisadi, sasa wewe uvccm unajifanya kutoa tamko ili watu wakuone wamaana, huna lolote songi ni lilelile tulilolizoea, mafisadi wakubwa mnawajua na hamuwezi wafanya kitu chochote, unajing'atng'ata hapo, una meno ya kuwala mafisadi.

jitokeze basi umtaje hata mmoja tuone ujasiri wako ukowapi!!!

tetetetetete, humndanganyi mtu, tetetete,
May 6, 2011 1:03 AM
blank.gif

Anonymous said... Matamko ya CCM na wanaCCM hayasadikiki, hayatoki moyoni, hayana dhamira ya kuleta mabadiliko. si ajabu huyo kijana Makonda kesho akakanusha katakata kuwa hajawahi kusema hayo aliyoyasema. inasikitisha kwakuwa inaoneshajinsi tunavyopoteza mwelekeo sahihi kilakukicha.Hatahivyo ikosiku wenye dhamira yakweli wahanga wa ufisadi huu tutasema tusikike na tutasimamia tunachokisema huo ndio utakuwamwisho wa waongo na hao wanajiona miungu watu. Ulemwisho wao wenyewe umekaribia. Mungu yu pamoja nasi hatutahofia wauwaji mafisadi.
May 6, 2011 1:32 AM
blank.gif

Anonymous said... Hii ngonjera ya CCM kujivua gamba, na mafisadi kupewa siku 90 inafaa kupelekwa katika mashindano - "is a good fiction"!
May 6, 2011 3:40 AM
blank.gif

Anonymous said... Mwadhani CCM inao ubavu wa kuwanyoshea kidole mafisadi? Wanalindana na hakuna chochote watakachotendewa; yote muyaonayo ni kiini macho tu. CCM inajifanya imeondoa gamba, lakini sumu ni ile ile, tena imezidi kuwa kali. Ona walivyoanza kusuasua na hizo barua walizokuwa wanatamba nazo akina Nape. Wangekuwa na ubavu mbona wasizisambaze? Ni usanii mtupu. Na mabaradhuli tu ndio watakaotazamia mafisadi kushughulikiwa. Ni nani katika viongozi waliopo atathubutu? Ni nani kati yao aliye msafi?
May 6, 2011 3:45 AM
blank.gif

Anonymous said... CCM haina orodha ya mafisadi! wewe unasemaje wafilisiwe? Huna akili?
May 6, 2011 4:21 AM
blank.gif

Anonymous said... Mimi nashauri suala hili la ufisadi tumeshachoka kulisikia. Nina hakika hawatafanywa kitu chochote kwani wao ndio CCM yenyewe. Bila wao CCM haina uhai. Ninasema hivi kwa sababu watu hawa ni wafadhali wakubwa wa CCM. Pia wana siri kubwa wanayoijua juu ya serikali iliyoko madarakani kwa hiyo Mkuu wetu hayuko tayari kuwaudhi hawa kwani watamuumbua. Kwa hiyo sisi walalahoi tunateseka mioyo yetu bure mafisadi CCM hawataisha kwani wanaotajwa ni mapacha watatu tu je hao wengine vipi? Watalindana kama walivyozoea. Mwenyekiti wa taifa CCM alitamka jukwaani kuwa amewapa siku 90 wajiondoe lakini nina hakika siku 90 zitaisha bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi yao. Sababu ni hizi kauli zinazopingana za kina Nape na Mukama kuanza kusema hawajapewa siku 90. Wameona maji yako shingoni watanzania wako makini sana zikiisha siku 90 sijui watapita barabara gani.
May 6, 2011 5:14 AM

Post a Comment



Links to this post

Create a Link


Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

HABARI ZA KANDA

Majira Kagera Majira Morogoro Majira Kilimanjaro Majira Ruvuma Majira Dodoma Majira Zanzibar

ZA LEO!!!:

**Marekani yashinikizwa kuonessha picha za Osama**Osama MAswali mengi kuliko majibu**Samatta agoma kwenda Ulaya**

Zilizopendwa






TAFUTA HABARI



poweredby_999999.gif

Custom Search



PATA HABARI

Majira Business Times Dar Leo Spoti Starehe

JITANGAZE:

b2.jpg



Jazz & Blues Bar Saturday night...

Joett released a Valentine's Day music video created especially for YouTube. In this
unique concept Joett and his crew hit Dar es salaam's largest shopping mall,
Milimani City, to invite passersby to scribble the name of the one they love on a
placard above the title of his new single "I Could Never Live (Without Your Love)"
... so their messages of love can appear on the new Joett music video. The video was
uploaded to YouTube just before the 14th of February 2011.

The Harbour View Suites' New Orleans style Jazz & Blues Bar, located on the 9th
floor atop Harbour View Towers (formerly JM Mall) on Samora Avenue, is a fabulous
venue with a magnificent view of the harbour where, as of Saturday March 12th (and
every Saturday), Joett will perform a live one hour jazz set singing classics from
Frank Sinatra to Ella Fitzgerald, Luther Vandross to Barbra Streisand to name but a
few. The idea behind this jazz entertainment event is to offer corporate executives
and business entrepreneurs a laid back and informal environment to socialize and
network; and Saturday night revelers a hip pre-party venue to kick-start their Saturday night. Jazz & Blues Bar Saturday night events are sponsored by Business
Times, Times 100.5 FM, Harbour View Suites, Advertising Dar, Island Def Jam Digital
Distribution (USA), Joett Music and DarCity Promotion
 
7 Maoni:


franco said... BONGO BWANA DOWANS NDIO TATIZO NA NI LAZIMA LILIPWE KWA SABABU MKATABA UPO NA YOTE HAYO NI MATUNDA YA CCM,MHASIBU WAO MKUU ALITUMIA PESA YAKE KWA PILAU NA POSHO SASA NDIYO MATUNDA YAKE.
HIVI DUNIANI KUNA MTU ANAYETOA PESA BILA KUPATA FAIDA SASA CCM MJUE WALE WALIOWAPA PESA ZA UFADHILI NDIO WANAZIRUDISHA.
TUNASUBIRI TUONE MATOKEO YA KUWANYANG'ANYA MALI ZAO HAYA WEEE
May 6, 2011 12:07 AM
blank.gif

Anonymous said... Kweli hii ni bongo,Mkama alisema hawana orodha ya mafisadi, sasa wewe uvccm unajifanya kutoa tamko ili watu wakuone wamaana, huna lolote songi ni lilelile tulilolizoea, mafisadi wakubwa mnawajua na hamuwezi wafanya kitu chochote, unajing'atng'ata hapo, una meno ya kuwala mafisadi.

jitokeze basi umtaje hata mmoja tuone ujasiri wako ukowapi!!!

tetetetetete, humndanganyi mtu, tetetete,
May 6, 2011 1:03 AM
blank.gif

Anonymous said... Matamko ya CCM na wanaCCM hayasadikiki, hayatoki moyoni, hayana dhamira ya kuleta mabadiliko. si ajabu huyo kijana Makonda kesho akakanusha katakata kuwa hajawahi kusema hayo aliyoyasema. inasikitisha kwakuwa inaoneshajinsi tunavyopoteza mwelekeo sahihi kilakukicha.Hatahivyo ikosiku wenye dhamira yakweli wahanga wa ufisadi huu tutasema tusikike na tutasimamia tunachokisema huo ndio utakuwamwisho wa waongo na hao wanajiona miungu watu. Ulemwisho wao wenyewe umekaribia. Mungu yu pamoja nasi hatutahofia wauwaji mafisadi.
May 6, 2011 1:32 AM
blank.gif

Anonymous said... Hii ngonjera ya CCM kujivua gamba, na mafisadi kupewa siku 90 inafaa kupelekwa katika mashindano - "is a good fiction"!
May 6, 2011 3:40 AM
blank.gif

Anonymous said... Mwadhani CCM inao ubavu wa kuwanyoshea kidole mafisadi? Wanalindana na hakuna chochote watakachotendewa; yote muyaonayo ni kiini macho tu. CCM inajifanya imeondoa gamba, lakini sumu ni ile ile, tena imezidi kuwa kali. Ona walivyoanza kusuasua na hizo barua walizokuwa wanatamba nazo akina Nape. Wangekuwa na ubavu mbona wasizisambaze? Ni usanii mtupu. Na mabaradhuli tu ndio watakaotazamia mafisadi kushughulikiwa. Ni nani katika viongozi waliopo atathubutu? Ni nani kati yao aliye msafi?
May 6, 2011 3:45 AM
blank.gif

Anonymous said... CCM haina orodha ya mafisadi! wewe unasemaje wafilisiwe? Huna akili?
May 6, 2011 4:21 AM
blank.gif

Anonymous said... Mimi nashauri suala hili la ufisadi tumeshachoka kulisikia. Nina hakika hawatafanywa kitu chochote kwani wao ndio CCM yenyewe. Bila wao CCM haina uhai. Ninasema hivi kwa sababu watu hawa ni wafadhali wakubwa wa CCM. Pia wana siri kubwa wanayoijua juu ya serikali iliyoko madarakani kwa hiyo Mkuu wetu hayuko tayari kuwaudhi hawa kwani watamuumbua. Kwa hiyo sisi walalahoi tunateseka mioyo yetu bure mafisadi CCM hawataisha kwani wanaotajwa ni mapacha watatu tu je hao wengine vipi? Watalindana kama walivyozoea. Mwenyekiti wa taifa CCM alitamka jukwaani kuwa amewapa siku 90 wajiondoe lakini nina hakika siku 90 zitaisha bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi yao. Sababu ni hizi kauli zinazopingana za kina Nape na Mukama kuanza kusema hawajapewa siku 90. Wameona maji yako shingoni watanzania wako makini sana zikiisha siku 90 sijui watapita barabara gani.
May 6, 2011 5:14 AM

Post a Comment



Links to this post

Create a Link


Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

HABARI ZA KANDA

Majira Kagera Majira Morogoro Majira Kilimanjaro Majira Ruvuma Majira Dodoma Majira Zanzibar

ZA LEO!!!:

**Marekani yashinikizwa kuonessha picha za Osama**Osama MAswali mengi kuliko majibu**Samatta agoma kwenda Ulaya**

Zilizopendwa






TAFUTA HABARI



poweredby_999999.gif

Custom Search



PATA HABARI

Majira Business Times Dar Leo Spoti Starehe

JITANGAZE:

b2.jpg



Jazz & Blues Bar Saturday night...

Joett released a Valentine’s Day music video created especially for YouTube. In this
unique concept Joett and his crew hit Dar es salaam’s largest shopping mall,
Milimani City, to invite passersby to scribble the name of the one they love on a
placard above the title of his new single “I Could Never Live (Without Your Love)”
... so their messages of love can appear on the new Joett music video. The video was
uploaded to YouTube just before the 14th of February 2011.

The Harbour View Suites' New Orleans style Jazz & Blues Bar, located on the 9th
floor atop Harbour View Towers (formerly JM Mall) on Samora Avenue, is a fabulous
venue with a magnificent view of the harbour where, as of Saturday March 12th (and
every Saturday), Joett will perform a live one hour jazz set singing classics from
Frank Sinatra to Ella Fitzgerald, Luther Vandross to Barbra Streisand to name but a
few.The idea behind this jazz entertainment event is to offer corporate executives
and business entrepreneurs a laid back and informal environment to socialize and
network; and Saturday night revelers a hip pre-party venue to kick-start their Saturday night. Jazz & Blues Bar Saturday night events are sponsored by Business
Times, Times 100.5 FM, Harbour View Suites, Advertising Dar, Island Def Jam Digital
Distribution (USA), Joett Music and DarCity Promotion
 
Je lowasa akipitishwa Nape atampigia kampeni?
 
Back
Top Bottom