- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Baada ya mipango yao ya kuandikisha watoto kufeli leo Chama cha Mapinduzi kimesema kinahujumiwa na viongozi na mawakala wao na watendaji wa serikali za mitaa.
- Tunachokijua
- Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala ambacho kilianza rasmi Februari 5, 1977 kutokana na kuunganishwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amaan Abeid Karume.
Kuelekea uchaguzi wa serikaliza mitaa utakaofanyika mwezi Novemba 2024, CCM ni moja kati ya vyama vingi ambavyo vitashiriki uchaguzi huo huku kadri siku zinapokwenda kumekuwepo na taarifa nyingi zinazohusiana na uchaguzi huo ambapo pamoja na uwepo wa taarifa za kweli lakini kuwekuwepo na taarifa nyingi zisizo za kweli na zenye lengo la kupotosha.
Kumekuwepo na barua ambayo imekuwa ikisambaa mtandaoni na kudaiwa kuwa imetolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), barua ambayo inahusishwa na harakati za kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Uhalisia wa barua kutolewa na CCM upoje?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli na haijatolewa na Chama Cha Mapinduzi CCM kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya CCM.
Aidha JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa barua hiyo barua hiyo haijatolewa na CCM, Moja ya mapungufu hayo ni kutofautiana kwa mwandiko (fonts) ambapo barua hiyo imeandikwa kwa mwandiko tofauti na ule ambao umekuwa ukitumiwa na CCM katika barua zake rasmi.
Aidha kupitia kurasa wake wa mtandao wa X CCM imeikanusha barua hiyo na kwamba si ya kweli na kuutaka umma kuipuuza barua hiyo.
Barua hiyo imehifadhiwa hapa na hapa.