CCM yatoa maagizo waliotajwa ripoti za CAG, Takukuru

Intelejensia inaonyesha wahusika wengi wameshakimbilia kwa waganga wa jadi kupooza pooza wasidhuriwe pamoja na wizi wao,
NB,
wezi wote rudisheni fedha magagula hayatafanya lolote katika awamu hii ya sita!, Rudisheni fedha za umma,haraka.

Taabu kusikia kwao kama masikio ya kenge
 
Chama tawala nao wamesema:

View attachment 2573826

Hiki angalau kimtindo, kitakuwa kimeumana.

Ngoja tuone.
-----

Chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuwachukulia hatua kwa waliohusika kwenye ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Chama hicho kimetoa wito huo leo Jumamosi, Aprili 1, 2023 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Ripoti hizo za CAG na Takukuru ziliwasilishwa Ikulu, Dar es Salaam, Machi 29, 2023 na kubainisha ubadhirifu wa fedha katika maeneo mbalimbali serikalini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jioni, ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Sophia Mjema amesema kamati kuu imesikitishwa na kuwepo baadhi ya maeneo mengine ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa upungufu, udhaifu uliobainishwa, ikiwa ni pamoja na mifumo ya malipo na ukusanyaji wa mapato kutokusomana.

Amesema kuwepo kwa baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu, hali inayosababisha serikali kukosa mapato na kupata hasara, uwepo wa mashirika ya umma yanayojiendesha kwa hasara na vitendo vya ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma, kama vile kuongeza bei za manunuzi ya Serikali.

“Kamati Kuu imeielekeza Serikali kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliobainika kuhusika katika ukiukaji wa sheria na kusababisha ubadhirifu wa mali na rasilimali za nchi,” alisema Mjema na kuongeza:

“…imetoa maelekezo kwa Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana za uongozi vibaya na kushindwa kuweka maslahi ya nchi na uzalendo mbele katika nafasi walizoaminiwa kutumikia watu, badala yake wanaweka maslahi binafsi.”

Mjema amesema kamati kuu ya CCM, imeipongeza Serikali kwa kuratibu na kufanikisha vema ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris aliyetembelea nchi yetu kwa siku tatu kuanzia Machi 29 hadi 31, 2023.

Amesema ziara hiyo imeongeza uimara wa ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kufungua milango zaidi ya mahusiano yenye faida kwa maendeleo na ustawi kwa pande zote mbili, hususan katika maeneo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, kukabiliana na magonjwa, uchumi, uwekezaji na ajira.

Mjema amesema kamati kuu imezipongeza Serikali zote mbili za CCM ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Samia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais Hussen Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa vitendo, kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania wote.

Chanzo: Mwanannchi
Mwenyekiti wa CCM Taifa anaongoza kikao cha kuiagiza serikali

Mwenyekiti wa CCM Taifa ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Uchawi hautaisha Afrika
 
Kwa hivyo Mama hana mamlaka ya kuchukua hatua hadi aende huko kwenye mavikao mambuzini kuomba ruhusa?!.
 
Tatizo wenye nchi tumelala. Watu kama Raila ni kina Lipumba. Wahamasishaji watu wako wapi?
 
Ruto afanyeje kama Raila akichagua kuwa kama hawa wa kwetu?
 
Tatizo wenye nchi tumelala. Watu kama Raila ni kina Lipumba. Wahamasishaji watu wako wapi?
Raia wsnaosubiri kuhamasishwa ili wajue haki zao ni raia waliokufa mioyo.

Mungu atashusha ghadhabu yake soon
 
Hamasa inataka mtu kuijenga na kuiongoza haiwezi kunyesha kama mvua. Ndiyo maana jumatatu na alhamisi ni rasmi. Kwa nini siyo jumatano au jumamosi?

Baba akiweka manyanga chini mambo ya kufungua server yanaishia hapo.

Kukwepa jukumu la kuwahamasisha watu ni kutaka kuwatumia tu kama ngazi.
 
Hapo tutawatoa madarakani ila wataenda na fedha sisi tunataka fedha zetu ata wasipotolewa kwenye vyeo vyao au kazi zao
Watolewe madarakani na wawajibishwe kwa ubadhirifu walioufanya. Ifikie kipindi Tanzania iwe kama China katika swala la kuwashugurikia mafisadi kwa mustakabali wa nchi yetu.
Mpaka lini tutaendelea kujitoa kuitumikia nchi yetu kwa moyo wote wakati kuna watu wanajinufaisha kivyao.....
Hatuwezi kuendelea kuteseka na uananchi wetu kisa watu wachache......
 
Kufikia yenyewe kama China haiwezekani. Wenye kuifikisha huko ni sisi. Hapo itabidi kujizatiti kweli kweli.
 
Raia wsnaosubiri kuhamasishwa ili wajue haki zao ni raia waliokufa mioyo.

Mungu atashusha ghadhabu yake soon
Je hao wanaotoa hamasa wana mioyo ya aina gani? % ya watanzania wameshajikatia tamaa either kwakujua au kwa kutokujua haki zao, wanaishi ilimradi jua limezama na kesho limekuchwa na mahangaiko ya kutafuta ugali ni juu yao bila kutambua kuwa serikali iko pale kwaajiri ya kurahisisha mazingira ya utafurahi wao wa ugali.
Ujinga ni juu ya watanzania kutokujua haki zao, wachache wananjitokeza kuwaeleza na kuwaelimisha lakini mwisho wa siku wanawadharau wale wanaowafundisha.......
We Tanzanians are stupid creatures in the world
 
Kwani watanzania wa enzi za Dk. Slaa walitokea wapi? Au hawa:

Ya nini kutoliita koleo kwa jina lake? Viongozi wetu ni madhubuti wa aina ya Maalim, Odinga, Mtikila, Nyerere, Mandela, Tutu, Malema na wa namma hiyo?

Au viongozi wetu ni wa aina ya kina Lipumba na kina Cheyo?

Isije kuwa tunasubiria dodo kwenye minazi. Waliopo ilikuwa muhimu kujipima kama wanatosha. Kama vipi kuachia ngazi nayo ni option.

Inafahamika ikifikia hapa wengi huingiwa kigugumizi maungo huona woga wakaomba kikombe hicho kiwahusu wengine isipokuwa wao.
 
Sasa unautenganisha vipi CCM na seeikali, ni sawa na kusema baba wa familia amtaka mama wa familia awachukulie hatua watoto wao wa kuwazaa ndani ya nyumba yao, kama sio usanii ni kitu Gani.
 
Chama tawala nao wamesema:

View attachment 2573826

Hiki angalau kimtindo, kitakuwa kimeumana.

Ngoja tuone.
-----

Chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuwachukulia hatua kwa waliohusika kwenye ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Chama hicho kimetoa wito huo leo Jumamosi, Aprili 1, 2023 mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan.

Ripoti hizo za CAG na Takukuru ziliwasilishwa Ikulu, Dar es Salaam, Machi 29, 2023 na kubainisha ubadhirifu wa fedha katika maeneo mbalimbali serikalini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jioni, ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Sophia Mjema amesema kamati kuu imesikitishwa na kuwepo baadhi ya maeneo mengine ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa upungufu, udhaifu uliobainishwa, ikiwa ni pamoja na mifumo ya malipo na ukusanyaji wa mapato kutokusomana.

Amesema kuwepo kwa baadhi ya watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu, hali inayosababisha serikali kukosa mapato na kupata hasara, uwepo wa mashirika ya umma yanayojiendesha kwa hasara na vitendo vya ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma, kama vile kuongeza bei za manunuzi ya Serikali.

“Kamati Kuu imeielekeza Serikali kuchukua hatua thabiti kwa wahusika wote waliobainika kuhusika katika ukiukaji wa sheria na kusababisha ubadhirifu wa mali na rasilimali za nchi,” alisema Mjema na kuongeza:

“…imetoa maelekezo kwa Serikali kuwafuatilia watu wote wanaotumia dhamana za uongozi vibaya na kushindwa kuweka maslahi ya nchi na uzalendo mbele katika nafasi walizoaminiwa kutumikia watu, badala yake wanaweka maslahi binafsi.”

Mjema amesema kamati kuu ya CCM, imeipongeza Serikali kwa kuratibu na kufanikisha vema ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris aliyetembelea nchi yetu kwa siku tatu kuanzia Machi 29 hadi 31, 2023.

Amesema ziara hiyo imeongeza uimara wa ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kufungua milango zaidi ya mahusiano yenye faida kwa maendeleo na ustawi kwa pande zote mbili, hususan katika maeneo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, kukabiliana na magonjwa, uchumi, uwekezaji na ajira.

Mjema amesema kamati kuu imezipongeza Serikali zote mbili za CCM ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Samia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais Hussen Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa vitendo, kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania wote.

Chanzo: Mwanannchi
Mh huu utaratib tangu lini ukawa activated? Na kamwe hauwez kua activated ✔️!! Haujatokea utawala wa kuwawajibisha mafisadi na wabadhirifu ndan ya huu utawala wa CCM!! NB; Huo sio utamaduni wao!!
 
Tunahitaji wenye mioyo ya chuma kubadirisha upepo wa watanzania waoga kuzijua haki zao na maendeleo thabiti ya taifa lao.
 
Mh huu utaratib tangu lini ukawa activated? Na kamwe hauwez kua activated ✔️!! Haujatokea utawala wa kuwawajibisha mafisadi na wabadhirifu ndan ya huu utawala wa CCM!! NB; Huo sio utamaduni wao!!

Weka suluhu mkuu. Tunafanya je kutoka hapo?
 
Back
Top Bottom