CCM yatoa maagizo waliotajwa ripoti za CAG, Takukuru

Intelejensia inaonyesha wahusika wengi wameshakimbilia kwa waganga wa jadi kupooza pooza wasidhuriwe pamoja na wizi wao,
NB,
wezi wote rudisheni fedha magagula hayatafanya lolote katika awamu hii ya sita!, Rudisheni fedha za umma,haraka.
Mimi sirudishi, nimekula kwa urefu wa kamba yangu , shida nini
 
Sophia! Huu ni ukakasi!
Mnashangaa na kushtushwaje!?
Wakati huu ndio mchezo mchafu wa CCM yeyote awapo madarakani! Huu mtindo haujaanza Leo. Na ndio maana pale Arusha kongamano la viongozi hata mkuu alikiri kutoelewana na hii ni Kwa sababa ya ulaku wa pesa za kazi na miradi wanazopewa.
Walioko juu wakivutana Kwa mgawanyi kwanza.
Hata Halmashauri pesa nyingi sana zinaliwa na wenyewe ambaonwasimamizi.wakuu ni ninyi wenyewe.
Usilidanganye Taifa.

Huku kubadiliashana vyeo nafasi na Teuzi ni ujinga.

Kama wahusika wanaisimamia kazi na Fedha za umma na walipa Kodi wapo Kuna shida gani aitwe mbele ya kadamnasi ajieleze na mwisho apishe nafasi hiyo.
(Mtindo wa JPM) tumbua papo hapo.
 
Tuamue Sasa, je tuko tayari kama wananchi?
Mimi na wewe tunaweza kuwa tayari. Wawili sisi hatutoshi. Hapa ndipo wito wa kuzigeuza nyomi kutoka kwenye kuuza sura unapokuja. Nani atakamatwa katikati ya nyomi hizi:

Your browser is not able to display this video.



Hakuna watu 10,000 Hapo.
 
Huyu mama nae ni msaniii,sasa anampa maagizo nani?,yeye ndio Raisi na mwenyekiti wa chama,chama kinaipa maagizo serikali!!,serikali ambsyo yeye ndio boss!!sasa anajipa maagizo mwenyewe!!!??
Badala ya kutekeleza anazinguka zunguka tu kwa upuuzi!!yeye ndio mkuu wa serikali na chama,wote waliopo serikalini na chamani wapo chini yake?!!sasa Kuna haja gani ya kuludia rudia matamko ya kujiambia
 
Kwa ushauri wangu, ni muhimu sana kwa Serikali kuchukua hatua zaidi ya kuwatoa tu kwenye madaraka watu waliobainika kufanya ubadhilifu wa fedha. Ni muhimu pia kurudisha fedha hizo ili kuirejesha serikali kwenye hali nzuri ya kiuchumi na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma muhimu. Ni muhimu pia kwa Serikali kuwachukulia hatua kali watu wote wanaohusika na vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na kuhakikisha kuwa haki inatendeka. Hii itasaidia kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao na kuhakikisha kuwa nchi inaelekea kwenye maendeleo endelevu.
 

Mkuu wadhani hawayajui hayo? Au kuwa itafika siku moja wataona wayafanye hayo ghafla kwa kujisikia kwao?
 
Hao wakugenzi wa wilaya ni makada wa ccm, wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wote ni makada badala ya kuajiri watu kwa professional zao.
Wataachaje kugawana asali ya hazina ya nchi ukizingatia chama kile wote ni ukoo wa panya?
Baba ana ndevu, mama ana ndevu na matoto nao wana ndevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…