Mwiba naamini umekosea kichwa cha habari, inabidi kisomeke.
" CCM yatoa mkong'oto kwa wananchi TANGANYIKA ."
Kwani wao ndio waliofanya maamuzi kwa kupigia upinzani kwa madiwani, wabunge na raisi wa upinzani na CCM ikawapora ushindi wao. Fikirisha kidogo tu kichwa chako, pale Arusha wakati wa kudai vurugu au pale Loyola kituoni-Ubungo, Mwanza kwenye jimbo la Ihemela,n.k waliokesha kituoni kulinda kura na baadae kudai haki yao hadi kupigwa mabomu si Dr.Slaa, si Freeman Mbowe, si Zitto Kabwe, si Wenje, si Mnyika bali ni wananchi.
Ama kwa hakika CCM imewapa mkong'oto wananchi wa Tanzania. Ningekuwa mimi ndie moderator wa hii forum, nadhani ningebadilisha kichwa cha habari kisomeke hivyo!