Nchi inaongozwa kwa sheria na sio kwa maamuzi binafsi, watanzania wengi hawana kawaida ya kufanya maamuzi ndani ya sheria na ya kisomi kwa kuwa vitu hivi vililetwa na wazungu kwetu, havikuibikia africa. Siamini kwamba tindu lissu, mabere na huyo dr ndiyo wasomi wakuu wa sheria, tupo kwenye century ya 21, kila kitu kipo wazi kwenye mtandao na kimaandishi, tunauwezo wa kuzisoma na kuvielewa na kufanya maamuzi sahihi. Kivyovyote vile, chadema wanafanya maamuzi ndani ya sheria zilizopo, wanajua, wakizivunja wanalo.
Naamini, kuwa ni busara kuita press conference na kufanya informed decision ndani ya sheria. Sio kukurupuka na kuacha vitabu pembeni na kufanya maamuzi, kila siku utachekwa kwa ufinyu wa akili zako iwapo unataka kuendesha nchi, taasisi, chama, au kampuni kwa kutokea kijiweni,( aristottle na wenzake ndo walileta elimu hii ya kisasa duniani kutokea greece, sasa watanzania hatutaki kutumia, kuamini kwamba, ni kwa usomi na science ndipo tutaweza kuiendesha nchi, siamini kuwa mtu akiwa anaumri mkubwa na ana phd ndo anajua kila kitu, ni lazima usome kila siku kujua, dunia iko wapi na imetoka wapi).