CCM yavunja rekodi Mkutano wa kufunga Kampeni Migoli Isimani

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ismani Emmanuela Mtatifikolo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amehitimisha mikutano ya kampeni za Uchaguzi Mdogo katika Kata ya Idodi kwa kuwaomba wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi kupiga kura za Ndiyo kwa CCM katika uchaguzi utakaofanyika Juni Mosi, 2026 ili kumpa nafasi ya kuyatekeleza kwa vitendo yote aliyowaahidi wananchi wa Ismani katika kata zote 13.

Mkutano huo wa Kampeni umehidhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa Ndugu. Issa Ussi Gavu ambao wote kwa pamoja walitumia nafasi hiyo kumuombea kura za Ndiyo Mgombea wa Ubunge Emmanuela Mtatifikolo.

Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la a Ismani zilizinduliwa rasmi Mei 11, 2026 ambapo Vyama takribani 17 vilijitokeza kushiriki na kuhitimishwa rasmi Mei 31,2026.
 
Duuh maskini CCM!
 
Tanzanians loves CCM than any political party within the country.

Kila la kheri mgombea ubunge wa CCM Emmanuela,

Nakutakia ushindi wa kishindo kikuu πŸ‘ŠπŸ‘Š
 
Viva CCM Viva
 

Chaguzi zenyewe fake matokeo tayari yameshapagwa wajinga jinga wengi sana πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hiyo rekodi iliyovunjwa imelinganishwa na rekodi ipi,ya lini,wapi na ilihusu nini?Acha utapeli wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…