CCM yawatakia waislamu heri ya mwaka mpya wa Kiislamu 1447 Muharram

CCM yawatakia waislamu heri ya mwaka mpya wa Kiislamu 1447 Muharram

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Haya mambo CCM wameanza lini? Mbona ni kujipendekeza sana kuelekea mwaka huu wa chaguzi kutafuta kura kwa namna na kujionyesha wao ni wema sana
=====================

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa salamu za heri na baraka kwa Waislamu wote nchini Tanzania na duniani kote katika kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Muharram.

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amesema mwaka mpya wa Kiislamu ni fursa adhimu ya kutafakari maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W), hususan ujasiri wake, uvumilivu, na moyo wake wa kujitolea kwa ajili ya kuleta haki, amani na mshikamano wa kijamii.

“Kwa niaba ya CCM na kwa niaba yangu binafsi, nawatakia Waislamu wote mwaka mpya uliojaa mafanikio, afya njema, amani na mshikamano. Tunathamini sana mchango wa jamii ya Waislamu katika kujenga taifa letu, kukuza maadili, kuimarisha uzalendo, na kudumisha umoja wa kitaifa,”
amesema Katibu Mkuu.
snapins-ai_3663636362957170653.jpg
 
Back
Top Bottom