Ndugu zangu watanzania,
Ukisikia na kuambiwa kuwa CCM ni chama kiongozi Barani Afrika,uwe una elewa maana yake.ujuwe ni chama kinachoendeshwa kitaasisi na chenye kuongozwa kwa misingi ya katiba ,kanuni , taratibu na miongozo mbalimbali.
Ambapo ukikiuka misingi hiyo ya kikatiba kwa maslahi yako binafsi na kwa tamaa zako binafsi ,ni lazima ichukuliwe hatua kali bila kujali cheo chako na jina lako.ndio sababu ya CCM kuendelea kutawala na kuongoza Taifa hili mpaka leo hii.kwa sababu ya kutamalaki kwa nidhamu na maadili ndani ya chama.
Sasa leo kikao cha kamati kikuu kimefanya maamuzi mazito ya kuwavua uongozi wafu watatu baada ya kubainika na kukutwa makosa mbalimbali.hilo ni onyo tu maana yake wakiendelea makosa yaliyowafanya wakavuliwa uongozi ,wanaweza kufukuzwa hata uwanachama wao ili waende huko kwa vyama vinavyoendeshwa kama Sacco's au kipofu gizani kama ilivyo CHADEMA ambako kila mtu ni kama Kambare au Beberu mwenye ndevu.
View attachment 3084596
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.