PreGE2025 CCM yazindua rasmi Ilani yake ya 2025. Yaweka Katiba Mpya kama mojawapo ya agenda watakazozitekeleza!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu akishiriki Mkutano Mkuu Chama cha Mapinduzi CCM siku ya pili Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Dodoma, leo tarehe 30 Mei, 2025.

Soma hapa Ilani > Ilani ya CCM 2025-2030


View: https://www.youtube.com/watch?v=yXnzuEg-DLk
====================================================

Your browser is not able to display this video.



​
Prof Kitila Alexander Mkumbo, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 akizungumza wakati akiwasillisha Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, Ijumaa tarehe 30 Mei 2025, Dodoma alisema:

β€œSehemu kubwa ya maudhui ya Ilani hii yametokana na maoni ya wanachama wa CCM, wananchi na wadau mbalimbali. Kwa mfano: Vijana wetu wa UVCCM waliandaa makongamano mbalimbali kutoka pande zote za Tanzania na kutoa maoni yao.

Msisitizo wao mkubwa ulikuwa ni kwamba Ilani ije na suluhu ya ajira kwa vijana. Tulikutana na Mabaraza ya Wazee, wanawake na makundi mbalimbali maalum. Kwa umuhimu wa pekee, nitambue mchango uliotolewa na Asasi za Kiraia (AZAKI). Tumekutana nao mara tatu, tukawasikiliza kwa umakini mkubwa, tukahojiana nao na walitupatia nakala ya Ilani yao. Tumezingatia maoni ya wadau wote”

"Sehemu kubwa ya maudhui ya Ilani hii yametokana na maoni ya wanachama wa CCM, wananchi na wadau mbalimbali. Kwa mfano: Vijana wetu wa UVCCM waliandaa makongamano mbalimbali kutoka pande zote za Tanzania na kutoa maoni yao.

"Msisitizo wao mkubwa ulikuwa ni kwamba Ilani ije na suluhu ya ajira kwa vijana. Tulikutana na Mabaraza ya Wazee, wanawake na makundi mbalimbali maalum. Kwa umuhimu wa pekee, nitambue mchango uliotolewa na Asasi za Kiraia (AZAKI). Tumekutana nao mara tatu, tukawasikiliza kwa umakini mkubwa, tukahojiana nao na walitupatia nakala ya Ilani yao. Tumezingatia maoni ya wadau wote"

Yaliyomo kwenye ilani kuhusu sekta ya Madini

"CM inatambua kuwa sekta ya madini ina nafasi ya kipekee katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Katika kuhakikisha sekta hiyo inaongeza mchango katika ukuaji wa uchumi, kipaumbele kitawekwa katika kuongeza thamani ya madini nchini kabla ya kusafirishwa nje, kuwezesha uchimbaji wa madini wenye tija, uendelezaji wa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kunufaika na ushiriki wao katika shughuli za madini, na kuimarisha usimamizi wa mapato yatokanayo na biashara ya madini.

Ili kufikia azma hiyo Chama kitaielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo: Kufanya utafiti zaidi wa maeneo yenye madini na kuongeza eneo lililopimwa na kufanyiwa utafiti kutoka asilimia 16 ya sasa hadi kufikia asilimia angalau 50 ifikapo mwaka 2030 ili kuhamasisha uwekezaji hususan wa madini muhimu na ya kimkakati;

Kutokana na umuhimu na nafasi yake katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla, Serikali itaweka mazingira maalumu ya kisera na kisheria yatakayohakikisha kuwa madini adimu na ya kimkakati (strategic mineral resources and rare earth elements) yanachimbwa na Watanzania na/au Watanzania kwa ubia na wawekezaji kutoka nje. Aidha, Serikali itaweka sera, sheria na kanuni zitakazohakikisha kuwa madini haya hayasafirishwi nje bila kuongezewa thamani nchini”,

Yaliyomo kwenye ilani kuhusu sekta ya kilimo

"Kwa kutambua nafasi ya kilimo katika usalama wa nchi, ujenzi wa uchumi na kukuza kipato cha wananchi, CCM itaendelea kusimamia mapinduzi katika sekta ya kilimo ili kukifanya kuwa cha kisasa na chenye tija. Lengo ni kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa chakula, kuongeza kipato cha wakulima, kukuza Pato La Taifa, kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda, na kuongeza ajira. Katika miaka mitano ijayo, CCM inaweka shabaha ya kuona kuwa sekta ya kilimo inakua kutoka asilimia 4.6 mwaka 2025 hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 kwa kuchukua hatua zifuatazo:

i) Kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora na kwa bei nafuu;
ii) Kuendelea kutoa ruzuku ya pembejeo mbalimbali kwa wakulima ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija;
iii) Kuboresha na kuongeza miundombinu ya umwagiliaji itakayoongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 983,466.06 mwaka 2024 hadi kufikia hekta 5,000,000 mwaka 2030 ili kupunguza utegemezi wa mvua kwenye kilimo;
iv) Kuimarisha upatikanaji wa zana za kisasa za kilimo, ikiwemo kununua na kusambaza matrekta 10,000 kwa wakulima; na
v) Kuanzisha mfuko wa dhamana kupitia Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo na Benki ya Ushirika ili kuwawezesha wakulima na wananchi wengine wanaojishughulisha na uongezaji wa thamani kwa mazao ya kilimo, mifugo na samaki kukopa katika taasisi za fedha kwa riba ndogo”
 

Attachments

Your browser is not able to display this video.


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeweka ajenda ya Katiba katika ilayani yake ya uchaguzi ya mwaka 2025-2030, kikisema kuwa kinaamini kuwa misingi imara ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria ni muhimu katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kama msingi mama wa shughuli za maendeleo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Kuu ya Kuandaa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Profesa Kitila Mkumbo leo Mei 30 jijini Dodoma, akisema kuwa chama hicho kinatambua mchango wa falsafa ya uongozi wa 4R katika kudumisha maelewano, mshikamano na umoja miongoni mwa wadau wa maendeleo nchini.

Katika kutekeleza hayo, amesema Chama kitaielekeza Serikali kuimarisha misingi ya demokrasia kwa kuboresha mazingira wezeshi ya wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

β€œKuweka mfumo wa kisheria katika kutekeleza falsafa ya uongozi ya 4R; Kuhuisha na kukamilisha mchakato wa katiba mpya; Kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi kwa kuzuia na kudhibiti vitendo vya rushwa na kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu dhidi ya viongozi na watumishi wa umma watakaojihusisha na vitendo hivyo.

β€œKuendelea kuimarisha Serikali za Mitaa kama nyenzo ya demokrasia na maendeleo ya wananchi kwa kuandaa na kutekeleza sera ya taifa ya ugatuzi; Kuendelea kuimarisha uhuru wa asasi za kiraia na vyombo vya habari kama taasisi muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na sauti ya wananchi; na Kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Haki Jinai kama sehemu ya kuimarisha mnyororo wa hakijinai” amesema Profesa Mkumbo.
 
Ilani imeweka namna ya kuzuia wizi wa kura na tutakavyopata katiba mpya?

Maana CCM mmebadili katiba yenu ila katiba ya nchi kubadilishwa mnachora mstari.
 
Sisi kama Deep State hayo hayatuhusu, nchi ni mali yetu, hatuwezi kufuata katiba yoyote.
 
Tena wangesema anawakilisha kundi la '' LGBTQ''. Leo Msajili wa 'si hasa'' angemaliza Ink cartridge kwa barua za kujieleza. Afande J4 naye ungemsikia wanafuatilia wengine walioficha mtaa wa Ufipa.
Bilionea Wambui angetoa onyo kali.
 
Wakuu mama kizimkazi katoa speech yake karusha dongo kwa bishop
Moja kwa moja nimegundua ni dhaifu saaana yn hana sifa ya kuwa kiongoz na hyo weakness ndo wanaitumia wapiga dili sasa
Mzee baba kule tocha alikopumzika lazma anajuta moja ya kosa alofanya ni kubalance gender
Bc wapiga dili waneshangilia walivosikia dongo la bishop😁😁😁😁😁
 
Welcome to the club, umechelewa kufaham hili
 
Mwanamke anabaki kuwa mwanamke tu.
Wazanzibari waliligungua hilo siku nyingi na wanaiheshimu Qoran: nyinyi wabara hamuheshimu dini za wenzenu ndio maan mkamtawaza mwanamke awatawale : hiyo ni haram!! Matokeo yake nchi inateseka kutokana na Ufisadi wake huyu bibi kizimkazi.
 
Ilani ya CCM ya mwaka 2015 ndani yake kulikuwa na kipengele cha "kukamilisha" mchakato wa katiba mpya, kilichofuata baada ya hapo ni Rais aliyenadi Ilani hiyo kupuuza kipengele hicho.

Kwa CCM ilani ni kipande cha karatasi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…