Hio ndio hali halisi. CCM inajaribu kuhadaa umma eti kwamba Dr Mwinyi yuko tayari kwa maridhiano, sio kweli.
Tokea kumaliza kwa uchaguzi wa 2020 ulioacha machungu, simanzi, vilio na dhulma za wazi kile kinachoitwa maridhiano wala hakipo hadi sasa. Hakikuwepo mwanzo na hakuna dalili.
Kumeendelea kufanywa hadaa na kuwaaminisha watu eti Dr Mwinyi ameonesha moyo wa Maridhiano ukiuliza unaambiwa eti kwa kuiandikia barua ACT kuwasilisha majina ya Makamo wa kwanza wa Raisi na pili kuwaachia ACT nafasi mbili za Uwaziri.
Haya sio maridhiano, haya ni matakwa ya kikatiba. Wanaposahau na kujitoa fahamu ni pale wanaposhindwa na kupotezea kuwa tayari Katiba ya Zanzibar walishaivunja.
Wanapotezea kuwa Katiba inataka kuwe na Haki katika chaguzi, na ni wazi uchaguzi ulivurugwa na mamlaka na kufanya ghiliba za kiwango kikubwa kuanzia mwanzo hadi mwisho
Watu wameuliwa na kuonewa vya kutosha, kuteswa, kunyanyaswa na kupigwa mno. Kuna vilema, kuna majeruhi, kuna waliokamatwa na kutupwa misituni,kuna wajane, mayatima na kuna waliouawa kinyama na mengi maovu. Jamii imegawanyika na kuumizwa mno. Hakuna Katiba na Sheria iliyofuatwa na kutiwa maanani wakati na baada ya Uchaguzi zaidi ya vitisho na ubabe wa Dola.
Hakujafanyika uchunguzi wa maridhiano na waliotenda haya hawajashughulikiwa hadi sasa. Kukimbilia kuunda serikali ya SUK bila kufanyika makubaliano ya namna ya kutatua changamoto hizi na kuzungumzwa kiini cha haya ni kujipotosha kusema eti unataka maridhiano kwa sababu tu umeandika barua ya kuomba majina ya mawaziri wawili au Makamo wa Raisi.
Hayo sio maridhiano, hicho ni kichaka cha kujificha na kuficha maovu. CCM walishakataliwa Zanzibar wamelazimisha kupendwa, lengo ikiwa ni kutawala kwanza mengine baadae.
ACT wana hiyari ya kushiriki au la baada ya kujiridhisha kwa upande wao na wanachama wao. Kushiriki kwao kama watakubali sio kwa sababu ya maridhiano hapana ni kwa sababu za kikatiba na kuangalia hatma ya mapambano.
ACT haiwezi kufungwa kuendelea kudai haki zao kwa sababu eti watakuwa ndani ya SUK ikiwa wataamua kuingia. Hawafungiki na maovu ya wengine waliovunja sheria na kamwe haitahusika kubeba msalaba wa wengine na kamwe haistahiki kulaumiwa na wabia wao pale watakapoamua kuchanja mbuga kupata haki zao iwe ndani au nje ya serikali kwa sababu kuu moja kwamba hakuna Maridhiano. CCM imekataa maridhiano.
CCM IMEKATAA MARIDHIANO TAYARI
Ndio CCM imeshakataa maridhiano tayari. Kitendo cha kusonga mbele na teuzi za viongozi na serikali kuanza kufanya kazi bila ya ushiriki wa SUK tayari ni kukataa maridhiano kwa vitendo. Mpaka muda huu hakuna MOU yoyote ya utekelezaji kuhusu kilichotokea kwenye uchaguzi uliopita wa 2020 na tunaona hadaa za maigizo za maendeleo na za kutenda haki katika mazingira yale yale.
Wafanyaji na wanaoshutumiwa kutenda makosa wapo na hakuna dalili za kushughulikiwa. Hadi hapo picha iko wazi kuwa hakuna Maridhiano.
Waliouwa wapo, waliotesa wapo na waliovunja sheria wapo hakuna hatua za wazi au dalili ya kupewa uzito madai ya Upinzani kwenye kadhia ya Zanzibar. Madai ya Upinzani yako wazi na ushahidi upo.
Kamwe dhana ya Maridhiano isichanganywe na hadaa za uwepo wa Serikali ya kitaifa. CCM Zanzibar acheni hadaa kwa maslahi ya wote.
Kishada