Pre GE2025 CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

Pre GE2025 CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mabadiliko haya ni ya kikatiba.

Ibara ya 28 (2) ya katiba ya Zanzibar imeweka muda wa urais Zanzibar kuwa ni miaka mitano.

Huwezi kubadilisha hili bila mabadiliko ya kikatiba.

Kama hoja ni kutumia vizuri pesa za umma, ingependeza kama mabadiliko mengine yote ya kikatiba yakafanyika mara moja.
 
Ni mbinu nzuri ya kupishanisha uchaguzi wa Bara na Visiwani.

Hata hivyo Mwinyi angeendelea tu hata miaka 20 huko.

Lakini kwa huku Bara, hapa kwa kweli. Tulipaswa kuwa na rais mwingine kabisa Ikulu tangu ile 2021 Machi ya majonzi.
 
Ni mawazo mazuri hata huku bara iwe hivo miaka mitano ni michache na ni usumbufu tu
 

Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa
wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya Dimami kichama Zanzibar uliofanyika Ofisi za Wilaya hiyo Kiembesamaki.

Dk Dimwa amesema uamuzi wa kumuongezea muda wa kuongoza Dk Mwinyi unatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa tangu aingie madarakani.

Katika maelezo yake, Dk Dimwa amesema CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kuwa ni wananchi wanahitaji maendeleo endelevu, hivyo Rais Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe nchi ya visiwa iliyoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika mashariki.

"Wajumbe wa sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Mwinyi, tukajiridhisha hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” amesema Dk Dimwa.
Naunga mkono hoja.
 
Wajumbe wa Sekretarieti ya kamati maalum ya chama cha Mapinduzi Zanzibar wamependekeza kuongezeka Kwa kipindi cha utawala kwa Kwa Rais Hussein Mwinyi kutoka miaka mitano mpaka saba.
Je Kuna ubaya au inafaa?
Ewe mjenga nchi tiririsha maoni yako
Kitendo Cha kupendekeza kihivyo tu! WAMEVUNJA KATIBA!
Wanasheria Tenda hiyo....
 
Kwani ndio utakua uchaguzi w kwanza kwao? Mpk iwe loss.





KAZI ni kipimo cha UTU
 
Huu ulikuwa ni mpango wa dhalimu magu kabla Mungu hajaingilia kati, lakini mbegu matamanio yake imebaki hivyo inafanyiwa kazi.
chuki dhidi ya MAGU,katibu kasema ameridhishwa na utendaji wa Mwinyi we unaleta hasira za vyeti feki hapa,mpango wenyewe hauendi kokote labda kama Mwinyi ndo anausimamia.
 
Nitamlumu mzilankende siku zote kwa huu ujinga kwa sababu yeye ndio alikuwa mwanzilishi wa huu upumbavu uliopo sasa na kulikuwa na fununu alikuwa anataka kutawala milele.Haya ndio matunda aliyotuachia na sisi tunasema asante.Ndugu zangu ukimaliza muda wako just go!unachosha watu mwili na roho maana hii nchi inataka kugeuka kuwa ya kifalme!
 
Halafu mtu anajiita Dr.kwa ujinga huu. Wakati Rais Mandera anamaliza muda wake wa urais ambapo aliongoza kwa miaka kwa miaka mitano tu,alikuwa Tanzania kuaga wakati huo na kipindi hicho aliyekuwa Rais wa Zanzibar alikuwa Dr. Salmin Amour, na yeye alijaribisha mchezo huu wa kutaka kubadili katiba na angefanikiwa sijui huyu Mwinyi kama angekuwa hapo leo.
Kwenye hotuba ya kumkaribisha na kumpongeza Mandera, Mwalimu alisema term limit iliwekwa kwa ajili ya popular president na siyo unpopular maana kwenye uchaguzi ukiwa huru na haki ataondolewa kwenye kura kama ilivyotokea kwa Trump.
Sasa hawa wanabadili katiba kwa ajili ya huyu Rais aliyepo. Sasa fikiria akiingia Rais mwizi atatumia katiba hiyo hiyo iliyobadilishwa kuiharibu nchi.
Gharama za demokrasia hazipaswi kuangalia gharama.
 
Ngoja afariki kwanza ndio watakoma na kimbelembele chao hawajajifunza kwa marehemu jiwe na wapambe wao.
Kwanza nyie vichwa flat screen rais wenu anateuliwa dodoma kaeni kimya na flatscreen head zenu
Jiwe angekuwepo angeendelea kutawala milele alishaanza harakati za kubadilisha katiba hata wabunge wa upinzani alikuwa hataki kabisa.Hii nchi ilikuwa inaelekea kuwa ya kifalme wakati ule,ule mshale tukaukwepa now umerudi kwa namna nyingine!
 
Back
Top Bottom