Pre GE2025 CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heshimuni katiba jmn waafrika sisi bora tungeendelea kutawaliwa na wazungu huenda tungekuwa mbali mno!Afrika hatuna akili ya kujiongoza zaidi ya kutanguliza matumbo mbele.Huyo Mzanzibar akipewa miaka miwili itamsaidia nini kama kwenye mitano ameshindwa.Sultani go bhna utaanza kuchosha watu muda si mrefu
 
Balaa kwa nchi yetu! Sasa kilichobaki, "if you can't fight them, join them, " But kill them slowly from inside"!
TZ imekuwa shamba LA chama tawala,ukitaka Mambo yako yaende, ama Uwe mfanyabiashara, usidungamane na upande, au, chukua kadi ya CCM, piga pesa
 
Kama wameridhishwa na utendaji wake wamchague tena mwakani lakini siyo kubadili kipindi kimoja kuwa miaka saba. Wacha wamchurie shauri yao,CCM wana upuuzi mwingi sana
Hutaki chura apige miaka 7❓
 
Hata huku tunaomba iwe hivyo,sio mitano tena kwa mama bali ni mikumi kabisa,nitapeleka hoja hii bungeni ijadiliwe kwa kina.

Mikumi tena kwa mama samia
 
Ndio inavyopaswa kuwa, labda useme kuna elimu inayosomewa ili kuwa rais.
Nachojua mimi hata ikiwepo mifumo ila bado kutakuwa na athari katika masuala ya uongozi wa nchi kutokana na aina ya rais aliyepo madarakani. Sasa hauwezi kusema yeyote tu anaweza kuwa rais.
 
Nasema yoyote anaweza, kwa maana hakuna mtu amezaliwa special wa kazi ya urais. Mifumo itamshepu atakayepata nafasi hiyo ili atakeleze majukumu yake kwa usahihi.
 
Mifumo haimgeuzi mtu kuwa robot, ndio maana nasema pamoja na mifumo ila bado athari ya uongozi kutokana na aina ya rais aliyekuwepo madarakani lazima iwepo. Huko kwa wenzetu wana mifumo ila bado wakiona kiongozi wao anafanya wasiyotaka wanampiga chini na kuweka mwengine.
 
Sijawahi kuamini wazenji wana akili, unaswali sala tano mji mkongwe na kuchapa bakora makobe halafu mtu huyo huyo unaenda hoteli ya kitalii pwani mchangani kuwakaangia watalii wazungu nguruwe na kuserve whisky! huu ni ushahidi tosha.

Miaka mitano inatosha na kama Rais akitoboa uchaguzi anapewa mitano mingine na kutoka kumuachia mwingine ambae anaweza kuwa bora zaidi. Je rais alietoka angekaa madarakani miaka 7 times 2 = 14 huyu aliepo angepataje nafasi?

Katika miaka kumi ya urais huwa kuna makundi ya watu huwa yamebanwa kiuchumi , Rais akitoka akaja mwingine inakuwa zamu yao kula keki. Yaani huyu aliesema Rais aongezewe muda hataki uhondo, halua na tende viishe upande wake na wengine wapate kula!!

Kuruhusu jambo hilo ni mwanzo wa kuvuruga katiba na kitakachotokea ni fujo na vurugu maana sasa itakuwa kila Rais mzenji wa bara au visiwani anajiamulia atawale kama Mugabe hadi afie madarakani!!
 
Mifumo haimgeuzi mtu kuwa robot, ndio maana nasema pamoja na mifumo ila bado athari ya uongozi kutokana na aina ya rais aliyekuwepo madarakani lazima iwepo. Huko kwa wenzetu wana mifumo ila bado wakiona kiongozi wao anafanya wasiyotaka wanampiga chini na kuweka mwengine.
Ndio maana nasema mifumo ndio inaamua kiongozi aweje, na akishindwa kwenda na mifumo anapigwa chini.
 
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa
wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya Dimami kichama Zanzibar uliofanyika Ofisi za Wilaya hiyo Kiembesamaki.

Dk Dimwa amesema uamuzi wa kumuongezea muda wa kuongoza Dk Mwinyi unatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa tangu aingie madarakani.

Katika maelezo yake, Dk Dimwa amesema CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kuwa ni wananchi wanahitaji maendeleo endelevu, hivyo Rais Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe nchi ya visiwa iliyoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika mashariki.

"Wajumbe wa sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Mwinyi, tukajiridhisha hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” amesema Dk Dimwa.
Naunga mkono uamuzi huo.Mwinyi yuko vizuri sana
 
Rais Hussein Mwinyi ni kijana anayeheshimika sana kwa utendaji na hata kwa maadili tena ni kwa watanzania wote kwa asilimia kubwa.Sidhani kama ataendekeza upuuzi na ujinga huu wa chawa wa CCM wa kuvunja katiba.Kwa maadili yake mema,AWAKEMEE HARAKA.Na Mwinyi asije akadhani wanampenda kwani zinaonekana ni mbinu za kumuangusha.Wajinga hawa wanajua hili litaleta tafrani na kumfanya adharaulike kupitia migongo yao.Sio watu hao Rais Mwinnyi.Wanavaa kijani tu lakini ni sawa sawa na wachawi tu.
 
Ndio maana nasema mifumo ndio inaamua kiongozi aweje, na akishindwa kwenda na mifumo anapigwa chini.
Kwahiyo tuseme uongozi wa Obama ulikuwa sawa tu na Trump naye Trump uongozi wake ulikuwa sawa tu na Biden?
 
Back
Top Bottom