Elections 2010 CCM Zanzibar wataka Mbowe aombe radhi

Joshi Kanji

Member
Joined
Mar 1, 2008
Posts
75
Reaction score
43
Kufuatia kauli yake kuwa Marehemu Idris Abdul wakil alikuwa darasa la saba..

Zanzibar yambana Mbowe awaombe radhi

Mwinyi Sadallah

  • Ni kwa kauli Rais mstaafu darasa la saba

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametakiwa kuomba radhi kufuatia kauli yake kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, marehemu Idrisa Abdulwakil, alishika nafasi hiyo akiwa na elimu ya darasa la saba.

Kauli hiyo ilitolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar jana kupitia Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai.

Vuai alisema kauli ya Mbowe ni upotoshaji kwa Watanzania kwani Rais huyo mstaafu alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri aliyepata Shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Alisema CCM imeshitushwa na kauli hiyo na kumtaka Mbowe awaombe radhi Watanzania na wanafamilia kwa vile kiongozi huyo alikuwa ni wa kitaifa.

Hata hivyo, alisema CCM haifikirii kuchukua hatua zozote za kisheria, lakini kiungwana lazima wahusika wakubali wamefanya makosa kutangaza jambo kinyume na ukweli wake.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za chama hicho wiki iliyopita katika viwanja vya Jangwani, Mbowe alisema marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya darasa la saba lakini aliweza kumudu vyema uongozi kwa vile ni hekima na busara.

Mbowe aliyasema hayo baada ya wanachama wa CCM kudai kwamba mgombea mwenza wa urais wa Muungano kupitia Chadema ana elimu ya darasa la saba.

Hatahivyo, Mbowe akizungumzia suala hilo alisema anatafakari hatua hiyo ya CCM na kama itathibitika marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya chuo kikuu sio makosa kwa yeye kuomba radhi.

"Hilo nalitafakari na kama kweli ikithibitika kiungwana sio makosa kuomba radhi", alisema
 
Labda Mbowe alichanganya majina. Hivi Mzee Karume (RIP) alikuwa wa darasa la ngapi? Mbona naye alikuwa kiongozi mzuri tu aliyetuletea Muungano na kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo yaliyolenga watu kwa kuwajengea nyumba za kisasa? Wakati mwingine hicho kigezo cha elimu wala si hoja kwa sababu jitu linaweza kuwa na MaPhd kibao lakini lisiwe na busara wala uwezo wa kuongoza!
 
PHD hasa hizo za JK
 
Kama ni kweli alisema, basi mkuu ameteleza tu kibinaadamu na munkali wa kampeni. Zenji huwa hawaishii darasa la 7 wao huwa wanaenda mpaka chumba cha 11. Kwa hiyo kama marehemu alisomea zenji basi kiwango cha chini kabisa ni darasa la kumi na moja. Kama alisoma bara baada ya Azimio la Arusha ambapo ndiyo mfumo wa darasa la saba ulipoanza (lakini kwa umri wake na kuwa waziri wa Karume na Nyerere) hii haiwezekani.

Tumsamehe tuendelee mbele.
 
..Sheikh Idiris Abdul Wakil Nombe alikuwa m-Zenj msomi.

..Mbowe ameteleza kudai kwamba Sheikh Idiris alikomea darasa la saba.

..anachopaswa kufanya ni kuomba radhi haraka sana and move on.

NB:

..pamoja na kuwa Waziri ktk serikali za SMZ na Muungano, Sheikh Idiris aliwahi kuwa Spika wa Baraza la wawakilishi, balozi nchi za nje, na mkuu wa itifaki.
 
Bila ya shaka alipotoka! Anaweza alikuwa anamaanisha Rais wa Kwanza Sheikh Amani Abeid Karume!

Mbowe, kuwa mwuungwana na waombe radhi tu. Mwambie Bw. Mdogo Mnyika alitolee ufafanuzi.
 
Nasikia marehemu Karume ndio shule hakwenda mbali, sijui aliishia la ngapi!
 
ndo kusema mbowe alipayuka ............:eyeroll2:
 
Zarau kama hizo kwa wa Zenj ndio maana wanaanza kurudisha mipaka ya nchi yake:shocked:
 
labda mbowe alichanganya majina. Hivi mzee karume (rip) alikuwa wa darasa la ngapi? Mbona naye alikuwa kiongozi mzuri tu aliyetuletea muungano na kuwaletea wananchi wa zanzibar maendeleo yaliyolenga watu kwa kuwajengea nyumba za kisasa? Wakati mwingine hicho kigezo cha elimu wala si hoja kwa sababu jitu linaweza kuwa na maphd kibao lakini lisiwe na busara wala uwezo wa kuongoza!
ni sawa mtu ambaye ni mtundu na mjuaji hata kama hajasoma anaweza kutuongoza....lakini ukweli wengi wa aina hii walikua ni makandamizi wengine hua goigoi hawajui chochote cha ulimwengu wa kisasa...zamani sawa lakini sio karne ya 21..huyu tuna mashaka naye....makamu bomu....
 
Zarau kama hizo kwa wa Zenj ndio maana wanaanza kurudisha mipaka ya nchi yake:shocked:

sijui yupi kamdharau mwenziwe zaidi ...

unaweza kusema zanzibar imekidharau chadema kiasi cha kukipa mgombea mwenza wa darasa la saba tu:glasses-nerdy:
 
:becky:....Alikuwa anamaanisha madrasa...yaani Mzee alifika juzuu ya saba...
 
Kumlinganisha mgombea wetu na waasisi kama Mhe Karume waliotawala miaka ya 60 ni kurudisha nyuma hali halisi na kupotosha ukweli. Hata kama Karume alitawala akiwa na elimu ya darasa la saba, hali ya miaka ya sitini ni tofauti sana na sasa. Wakati ule wasomi walikuwa wachache sana na pia kiwango cha elimu alichofikia kilikuwa juu sana ukilinganisha na std 7 ya sasa. Haiingii akilini chama makini kama CHADEMA kumsimamisha std 7 karne hii kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz. Hiki ni kichekesho kwa jamii. CCM mgombea wao wa std 7 ni mmoja tu tena mgombea ubunge.
 
Dokii ameipenda hii:

dokii2.JPG
 
hii nilikuwa sijaiona hebu muangalie huyu mkurupukaji, sasa watu wa aina hii wanafaa kupewa nchi. basi kabla ya kusema si ungeuliza ? jee anajua kuwa kabla marehem idrissa hajawa rais alikuwa spika wa baraza la wakilishi ?

hawa kweli wamo demani

Zanzibar yambana Mbowe awaombe radhi

Mwinyi Sadallah

  • Ni kwa kauli Rais mstaafu darasa la saba

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametakiwa kuomba radhi kufuatia kauli yake kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, marehemu Idrisa Abdulwakil, alishika nafasi hiyo akiwa na elimu ya darasa la saba.

Kauli hiyo ilitolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar jana kupitia Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai.

Vuai alisema kauli ya Mbowe ni upotoshaji kwa Watanzania kwani Rais huyo mstaafu alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri aliyepata Shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Alisema CCM imeshitushwa na kauli hiyo na kumtaka Mbowe awaombe radhi Watanzania na wanafamilia kwa vile kiongozi huyo alikuwa ni wa kitaifa.

Hata hivyo, alisema CCM haifikirii kuchukua hatua zozote za kisheria, lakini kiungwana lazima wahusika wakubali wamefanya makosa kutangaza jambo kinyume na ukweli wake.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za chama hicho wiki iliyopita katika viwanja vya Jangwani, Mbowe alisema marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya darasa la saba lakini aliweza kumudu vyema uongozi kwa vile ni hekima na busara.

Mbowe aliyasema hayo baada ya wanachama wa CCM kudai kwamba mgombea mwenza wa urais wa Muungano kupitia Chadema ana elimu ya darasa la saba.

Hatahivyo, Mbowe akizungumzia suala hilo alisema anatafakari hatua hiyo ya CCM na kama itathibitika marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya chuo kikuu sio makosa kwa yeye kuomba radhi.

“Hilo nalitafakari na kama kweli ikithibitika kiungwana sio makosa kuomba radhi”, alisema
 
Ni kweli Mzee Idrisa Abdulwakil (RIP) elimu yake ilikuwa ni STD VII
 
hapana si kweli, alisoma makerere tena huko alikutana na akina nyerere na aboud jumbe mwinyi

ni kukurupuka tu, nadhani kwa kuwa alimuona marehemu alikuwa ni mtu mnyofu, asiependa makuu na mcha mungu, wakadhani watu wa aina ile hawana elimu

sasa ndio tujue kuwa chadema hakuna kitu wanamlaumu kikwete kuwa ni mtu wa kudanganywa na kama hili amelisikia kwa watu kadanganywa sana tena sana
 
Back
Top Bottom