Joshi Kanji
Member
- Mar 1, 2008
- 75
- 43
Kufuatia kauli yake kuwa Marehemu Idris Abdul wakil alikuwa darasa la saba..
Zanzibar yambana Mbowe awaombe radhi
Mwinyi Sadallah
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametakiwa kuomba radhi kufuatia kauli yake kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, marehemu Idrisa Abdulwakil, alishika nafasi hiyo akiwa na elimu ya darasa la saba.
Kauli hiyo ilitolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar jana kupitia Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Vuai Ali Vuai.
Vuai alisema kauli ya Mbowe ni upotoshaji kwa Watanzania kwani Rais huyo mstaafu alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri aliyepata Shahada ya kwanza Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.
Alisema CCM imeshitushwa na kauli hiyo na kumtaka Mbowe awaombe radhi Watanzania na wanafamilia kwa vile kiongozi huyo alikuwa ni wa kitaifa.
Hata hivyo, alisema CCM haifikirii kuchukua hatua zozote za kisheria, lakini kiungwana lazima wahusika wakubali wamefanya makosa kutangaza jambo kinyume na ukweli wake.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za chama hicho wiki iliyopita katika viwanja vya Jangwani, Mbowe alisema marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya darasa la saba lakini aliweza kumudu vyema uongozi kwa vile ni hekima na busara.
Mbowe aliyasema hayo baada ya wanachama wa CCM kudai kwamba mgombea mwenza wa urais wa Muungano kupitia Chadema ana elimu ya darasa la saba.
Hatahivyo, Mbowe akizungumzia suala hilo alisema anatafakari hatua hiyo ya CCM na kama itathibitika marehemu Abdulwakil alikuwa na elimu ya chuo kikuu sio makosa kwa yeye kuomba radhi.
"Hilo nalitafakari na kama kweli ikithibitika kiungwana sio makosa kuomba radhi", alisema
Zanzibar yambana Mbowe awaombe radhi
Mwinyi Sadallah
- Ni kwa kauli Rais mstaafu darasa la saba