Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Khamis Mbeto, ametangaza rasmi ratiba ya mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, akieleza kuwa mgombea husika atakwenda kuchukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
Amesema siku ya zoezi hilo muhimu itapambwa na matembezi maalum ya kumsindikiza mgombea, yakihusisha wanachama na wapenzi wa chama kutoka maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, baada ya mgombea kukamilisha zoezi la uchukuaji fomu, kutafanyika mkutano mkubwa wa hadhara ambao utahutubiwa na viongozi wa CCM, ambapo wananchi watapata nafasi ya kusikia dira na matarajio ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mbali na hayo, tamasha kubwa la wasanii nalo limeandaliwa ili kuongeza shamrashamra na hamasa, likihusisha burudani kutoka kwa wasanii maarufu wa muziki na sanaa za asili, sambamba na michezo ya kijamii.