MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Agosti 30, 2025.
Hayo yalisemwa Mjini Unguja, na Katibu wa Nec, Idara ya Itikadi, Mafunzo na Unenezi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis wakakti akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema, majira ya saa 4 asubuhi Dk. Mwinyi atafika katika ofisi za ZEC Maisara Mjini Unguja, kwa ajili ya kuchukua fomu na baada ya hapo mgombea atapanda gari maalum ya wazi na kupita katika maeneo mbali mbali ya Mjini Unguja.
Kwa mujibu wa Mbeto alisema, Dk. Mwinyi atapita barabara ya kwa Raju Magere, kisha atapita Miembeni na baadae kupandisha barabara ya Mapinduzi Square na kuelekea katika ofisi za Kuu za Chama cha Mapinduzi Kisiwandui Mjini Unguja.
Alisema, atakapofika katika ofisi za Chama mgombea atashuka na kwenda kupata dua kwenye kaburi la Hayati mzee Abeid Amani.
Karume na baada ya hapo ataingia ndani ya Ofisi za CCM kwa ajili ya kuzungumza na wazee na kusaini kitabu cha wageni.
Mbeto aliendelea na kusema kuwa, baada ya kutoka hapo Dk. Mwinyi ataelekea katika viwanja vya Mau ambapo ndipo kutakuwa na shughuli za kuhitimisha hafla hiyo ya uchukuaji wa fomu.
Aidha alibainisha kuwa, Dkj. Mwinyi atapata nafasi ya kuwahutubia wananchi wa Zanzibar na kusema muelekeo wake baada ya kuchukua fomu kuwa miaka mitano anaenda kuwafanyia nini wananchiu wa Zanzibar.
“Kwa maana hioyo wananchi wote watakaomsindikiza mgombea barabarani wote watatakiwa walekee kwenye viwanja vya Mau ambapo ndipo kutakuwa na utaratibu kuanza shughuli mbali mbali,” alisema
Hivyo Mbeto aliwoamba wanachama wa chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea wao.