Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema hakitamvumilia mwanachama yeyote ambaye ataanza kujipitisha majimboni na kuanza kupiga kampeni kabla ya wakati.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Dimwa ametoa kauli hiyo Aprili 12, 2025 wakati akizungumza na kamati za siasa za wadi, Wilaya ya Kusini ikiwa ni ziara ya kukagua uhai wa chama na kuelezea mabadiliko ya katiba ya chama namna ya kupata wagombea na kura za maoni.
Dkt. Dimwa amesema chama kimetoa nafasi kuanzia Mei 1 Mosi mpaka 15 mwaka huu kwa mwanachama yeyote mwenye sifa za kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo lakini bado hakijaruhusu kuanza kufanya kampeni.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema yeyote atakayeingia kwenye jimbo la mwingine kwa lengo la kumfanyia fujo chama kitamchukulia hatua bila huruma.
"Naomba niseme wazi kwamba ole wake mtu yeyote atakayeingia kwenye jimbo la mwenzake kwa lengo la kumfanyia fujo naapa kwamba sitamuonea huruma mtu huyo," amesema.