Habari za daylight robbery zimezidi kutia hofu wakazi wa Nairobi baada ya CCTV footage kuonyesha wakati mwanaume aliyekuwa amebeba bastola akiingia katika beauty shop huko Ruaka na kumpora simu mwanamke aliyekuwa amekaa nje ya biashara hiyo.
Katika video hiyo, mshukiwa anaonekana akimkaribia mwathiriwa kwa utulivu kabla ya kutoa bunduki na kumlazimisha amkabidhi simu yake. Baada ya kupata simu hiyo, anaondoka haraka kutoka eneo la tukio huku mwathiriwa akibaki akiwa ameshtuka.
Tukio hilo limetokea broad daylight, jambo ambalo limeibua wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya uhalifu wa kutumia silaha katika maeneo ya Nairobi na viunga vyake.
Incident hii inakuja wiki chache baada ya shambulizi la kutumia bunduki katika mgahawa mmoja Westlands, ambapo wahalifu wenye silaha waliwavamia watu na kuiba mali zao, hali inayozua maswali kuhusu usalama wa wananchi.
Police wanatarajiwa kutumia CCTV footage hiyo kuwabaini na kuwakamata wahusika huku wakitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia uchunguzi kujitokeza. Wananchi pia wamehimizwa kuwa waangalifu wanapokuwa katika maeneo ya biashara na kuripoti watu wanaowatia shaka.
Source:Buzzroom