CD za ngono ni dhambi kwenye ndoa?
Jamani nipo kwenye ndoa zaidi ya miaka 10, nilikuwa na package ya cd mbali za ngono na tulikuwa tunafurahia na mywife. Jana nimezikuta zimesagwasagwa...eti zinanichochea niwe na wanawake wengi, je wakuu sijapokonywa haki yangu?
Ndugu mimi nitajaribu kujibu swali lako kwa mujibu wa kichwa cha habari husika. Unapouliza kama ni dhambi, hii moja kwa moja inapelekea, kwenye zile imani zenye kuamini kuwepo kwa dhambi na Thawabu. Yaani ni kitendo kibaya au chema.
Kama Wewe Ni Muislam
Kwa wale wenye kuamini Dini ya Kiislam ni madhambi kwa Muislamu mwanamme au mwanamke kukaa kwenye runinga (TV) na kuanza kuangalia vipindi vya ngono au kinyume na maadili. Huwe mwenye ndoa au si mwana ndoa.
M'Mungu ametukataza hilo pale aliposema:
Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya
Q17: 32
Jambo lolote ambalo litakukaribisha na mambo zinaa pia ni zinaa.
Unapokaa mbele ya TV na kuanza kuangalia vipindi au Video/Dvd/Vcd visivyo na adabu utakuwa una makosa. Ni makosa kwa Muislamu kutazama uchi wa mwenziwe akiwa ni wa jinsiya moja au tofauti.
Uchi ulioruhusiwa kuutazama ni mume kumtazama mkewe na mke kumtazama mumewe basi.
Hapa nakubaliana na wachangiaji wengi walio pita, kwa kusema kwao kuwa uenda kwa kuangalia kwako hiyo mikanda, kukakuperekea wewe kutamani kuiga yale yanayofanywa, na hao porn star (!?) Na ikatokea kuwa mwenza wako si mahiri wa hao unayoyatamani, mwishowe utaamua kwenda kujaribu nje...
Kwa kutunza ndoa zetu inatakiwa tujiepushe na mambo ambayo yanaweza kutupelekea kufanya zinaa yenyewe kama hivyo unavyofanya.
Bila kuwa ni matamanio si kuzini lakini ikiwa utatazama TV yenye uchafu huo na ukapata matamanio utaandikiwa madhambi.
Kama Wewe Ni Mkristo:
Je unapotazama hizo Video hutamani? Kutamani mtu asiye mume au mke wako nikuzini katika Mathayo 5:27-30 tunasoma maneno hayaa:
"
Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
Lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.."
Soma vizuri andiko hilo hapo juu, unapotazama filamu za ngono, jicho lako huangalia na kukaribisha matamanio kwa mke au mume si wako (
Jicho lako la kuume likikukosesha). Kwa mujibu wa andiko ilo utahesabiwa kuwa umezini.
Kisha baada yakutazama, mikono yako itatekelea kile ambacho macho yameona ili kukamilisha matamanio yako. (
Na mkono wako wa kuume ukikukosesha)
Nimapenzi ya Mungu tusizini. Imeandikwa katika Wathesalonike wa kwanza 4:3
"
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, muepukane na usherati."
Basi kumbe hata kutazama tu kwa kutamani ni kuzini pia.
Tafadhali husichoke kunisoma, ila napenda kumalizia kwa kumnukuu Paulo alipokuwa anwaasa wakorintho:
Yakini habari imeenea kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika mataifa
.. Mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo
.. Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyanganyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
1 Wakorintho 5:1,2-11
Je vipi ukiwa wewe ni mkristo unakaribisha filamu za ngono na uzinzi chumbani kwako?