BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Vifaa hivyo ni pamoja na kompyuta za mezani, kompyuta mpakato, UPS, vishikwambi, printa, meza, viti, vibanda, vidhibiti na vifaa vingine vya tehama.
Akizungumza leo Jumamosi, Oktoba 29, 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Menejimenti na Maendeleo ya Afya (MDH), Dk David Sando amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa ushirikiano na CDC na ni sehemu ya msaada wa Serikali ya Marekani kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kutambua mapema magonjwa kwa wasafiri wote ndani na nje ya nchi.
“Tangu mwaka wa 2015, serikali ya Marekani imekuwa ikiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuboresha afua za afya katika maeneo ya mipakani ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa,” amesema.
Mkurugenzi wa Taasisiya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (Nimr), Profesa Said Aboud amesema vifaa hivyo vitagawiwa kwa pointi saba za kuingilia ikiwemo Namanga, Horohoro, Mutukula, Rusumo, Kabanga, Murongo na bandari ya Dar es Salaam.
Amesema msaada mwingine wa dharura ni pamoja kuongeza usaidizi kwa wafanyakazi 40 katika viwanja vya ndege vya kimataifa JNIA kwa ajili ya uchunguzi ulioimarishwa wa maabara kuingia na kutoka pamoja na mafunzo ya ziada kwa wafanyakazi 86 wa afya na wasio wa afya.
MWANANCHI