CDF Mabeyo asilaumiwe: Usalama kupitia njia ya kuficha kitu au usiri sio salama kama inavyo dhaniwa

Comments nyingi humunni kiashirio cha watu kupoteza uelewa kila kukicha. Mtoa mada amechambua kwa mtiririko mzuri na mifano halisi yeny kuhanikiza ukweli wa mambo katka zama hizi tulizopo.

Mwandishi hongera sana. Sio kila mtu ni lazima aelewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeelewa point yako unayotaka kusema lakini nadhani umeshindwa pia kuelewa tofauti ya security na secrecy. Hata kwenye computer unaambia kutumia password imara kama security, at the same time unaambiwa kuwa usimwambie mtu mweingine kuhusu password yakpo; hapo kuna security na secrecy. Secuirty ni ulinzi dhidi ya adversaries, halafu secrecy ni kuwanyima adversaries information za ndani zinazokuhusu.

Kwa mfano, sote tunajua white house ya Marekani ilipo na vile vile kuwa ina ulinzi kiasi kuwa huwezi kuingia pale kirahisi, lakini vile vile hatujui muundo wa ndani wa jumba lile na mahandaki yaliyomo mle ndani. Sote tunajua ilipo Pentagon yaani makao makuu ya jeshi la malekani, lakini vile vile kuna maeneo mengi sana ya siri ambako raia hawafiki na huko ndiko wanatunzia siri za jeshi. Mifano michache ni kama Area 51 huko Nevada ambako ndiko wanatunzia siri za jeshi la anga. Huko Pennsylvania maporini kuna maeneo ambayo hayana hata majina kwa ajili ya jeshi la nchi kavu; ukiingia pale simu inakata mawasiliano yenyewe, hata google maps haionyeshi chochote kuhusu maeneo hayo; hiyo ndiyo secrecy.
 
Ahsante kwa kutuongezea maarifa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…