CDF Mstaafu Mabeyo alivyoaga rasmi Watumishi wa Wizara

CDF Mstaafu Mabeyo alivyoaga rasmi Watumishi wa Wizara

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
1A.JPG

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Mstaafu, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo alivyowasili Wizara ya Ulinzi na JKT makao Makuu Mtumba, kwa lengo la kuaga rasmi kabla ya kustaafu kwa Umri wa Utumishi Jeshini.

Akiongea wakati wa kikao cha Waziri na Menejimenti ya Wizara amesema kuwa mara hii amefikahapo Wizarani kivingine.

“Leo nimekuja hapa Wizarani kivingine kuja kuaga baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda mrefu. Utumishi wa zaidi ya miaka 40 kuanzia mwaka 1979, ni umri wa mtu mzima anayekaribia kustaafu,” alisema.

Amemshukuru Waziri, Menejimenti pamoja na watumishi wote wa Wizara kwa ushirikiano waliompatia wakati analitumikia Jeshi kwa nafasi ya Mkuu wa Majeshi baada ya kuteuliwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu mwaka 2016.

Jenerali Mabeyo amemwomba Waziri, Menejimenti na watumishi wote kumpa kila aina ya ushirikiano anaostahili atakayeteuliwa mteuliwa mpya katika nafasi ya Mkuu wa Majeshi.

4..JPG
Naye, Waziri akiongea Machache kuhusu Jenerali Mabeyo, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) alisema kuwa kuagana si jambo jema sana, lakini inapendeza zaidi pale unapostaafu kwa heshima, kama anavyostaafu Jenerali Mabeyo.

Aidha, Mheshimiwa Waziri alisema “Nakushukuru kwa mchango wako uliotukuka kwa Taifa na kwa Jeshi. Mbali na kulifundisha Jeshi, Jenerali Mabeyo pia, umeliimarisha na kuliheshimisha Jeshi na pia, ulituwakilisha vyema nje ya nchi.

“Yapo mambo mengi umeyafanya amabyo yataendelea kubaki. Maana Bila Jeshi Wizara haipo. Na bila Jeshi hatuwezi kufanya chochote.”

Dkt. Stergomena alimkabidhi Barua ya Shukrani kwa kutambua mchango wake kwa Wizara na Taifa, pamoja na ushirikiano aliompa kwa kipindi chote alipokuwa Katibu Mtendaji wa SADC na hata alipoteuliwa kuiongoza Wizara hii mwezi Septemba, 2021. Kwa maana hiyo, akamhakikishaia kuwa aondoke akiwa kifua mbele huku akiamini kuwa umeliheshisha Jeshi kwa kufanya mambo mengi mazuri yaliyosaidia kulijenga msingi mzuri Jeshi letu.

Jenerali Mabeyo amestaafu rasmi utumishi wake Jeshini tarehe 30 Juni, 2022 baada ya kulitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa miaka 43, nafasi ya Ukuu wa Majeshi ameitumikia kwa kipindi cha miaka sita, miezi minne.

Wakuu wa Majeshi waliomtangulia ni pamoja na Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya (1964 - 1974), Jenerali Abdallah Twalipo (1974 -1980), Jenerali David BUgozi Musuguri (1980 -1988), Jenerali Ernest Mwita Kyaro (1988 - 1991), Jenerali Philemon Robert Mboma (1991 - 2001), Jenerali George Mwita Waitara (2001 - 2007) na Jenerali Davis Adolf Mwamunyange (2007 - 2016).
 
Back
Top Bottom