CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

Document gani inasema hivyo?
Na Je, Mabeyo alikuwa wa kwanza kujua Rais anaumwa?
 
Kama hakuna supportive documents, circular, guidelines or Constitution, haya yanabaki maoni binafsi.
 
Badala ya kushukuru mfumo kuruhusu katiba kufuatwa, mnakaa kualumu laumu, busara zilitumika sana na hata sasa zinatumika. What is Constitution infront of powerful people? Very powerful people ambao wangeweza kufanya lolote na kama kawaida yetu kwa upole wetu tungekubali na kutoa pongezi lukuki na wengine mkapata magonjwa yasiyoambukizwa, wanahitaji kushukuriwa.
 
Magufuli alikua hafuati katiba katika kuongoza nchi kwahiyo hilo wala tusolishangae ndio maana watu kama bashite walikua na sauti kumzidi hata waziri mkuu au makamu wa rais.
katiba iliishavunjwa kwa covid 19 kuingia bungeni maji hufuata mkondo. Tujifunze kuondoa desturi za kuvunja katiba. unaona sasa. liwe funzo kwa viongozi. ukiwazoesha hivyo watu huona kama jambo la kawaida
 
..Na aliyekuwa akimtonya Tundu Lissu kuwa mbaya wake yuko mahututi ni nani?

..Maana Lissu alikuwa na taarifa kuzidi Samia, Kassimu, Bashiru, hata Mama Janet.
Hatari sana! Ugonjwa wa Rais Magufuli ulijulikana zaidi kwa kina Tundu Lisu, Kigogo nk huku Makamu wa Rais akiwa hajui lolote!! Tena Rais akiwa amelazwa Hospitali ya viongozi! Wenye akili wazitumie vizuri kufikiri na kutoa majibu!! Kilichompata Rais Magufuli kinaweza kumpata yoyote! Ni vyema mifumo ikaangaliwa kwa jicho la tatu!!!! Nyoka akiuma huwa anajificha mpaka meno yaote tena na anarudi kuuma!!!
 
Acha bangeeeee!! Daktari wa Rais ndiye mtoa taarifa za Rais? Kasome tena Katiba!!
 
Wabongo bwana ujuaji mwingi Sana

Hivi unadhania mpaka mtu anakuwa CDF ni Jambo simple simple Sana eh

So wewe unajua utaratibu kuliko mkuu wa majeshi?

Tuache kujifanya wajuaji sana
Kama hujui katiba ni vizuri ukapiga kimya.Makamu wa Rais ndio kila kitu hayo mengine mnayakuza tu.
 
Kama hujui katiba ni vizuri ukapiga kimya.Makamu wa Rais ndio kila kitu hayo mengine mnayakuza tu.

Kifo kimetokea mbele ya viongozi wakuu wa ulinzi na usalama

Eh ulitaka katiba ifatwe Kwa kufanyaje?

CDF ampigie simu vice? Ndio katiba inasema hivyo?

Kwanini sio katibu mkuu kiongozi ampigie vice na kumpa taarifa?

Ndio maana akaitwa katibu mkuu kiongozi aende dar kutoka dodoma

Then ndio mambo ya katiba yakafatwa Kwa vice kupewa taarifa
 

..wakati mwingine nashawishika kuamini kwamba kilichotokea ni matokeo ya style ya uongozi au utawala aliyokuwa nayo Magufuli.

..majuzi, Mh.Makamba amenukuliwa akisema, mbele ya Rais Samia, kwamba kuna baadhi ya wateule wa Magufuli walikuwa wakimdharau na kumtenga Samia alipokuwa Makamu wa Rais.

..Zaidi, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa katiba, sheria, na taratibu, uliokuwa ukifanywa na Magufuli na baadhi ya wateule wake.

..Kwa hiyo, utaona kwamba uongozi wa Magufuli haukuwa shirikishi. Kati ya wateule kuna aliowafanya wa daraja la juu, na wengine wa daraja la chini.

..Bila shaka, Samia alikuwa kati ya kundi la wateule wa daraja la chini.

..Kwa bahati mbaya Magufuli akaugua. Na kwasababu alimtenga Makamu wake, ikawa vigumu kumshirikisha ktk usimamizi wa matibabu yake.

..Suala la kusimamia na kuratibu matibabu ya Magufuli likawa chini ya genge lake, badala ya Makamu wa Raisi kama inavyoelekezwa ktk Katiba, Sheria, na taratibu.

..Mwisho wa yote ni genge la Magufuli kuwa ktk mazingira ambayo hawakutarajia watakutana nayo.

..Magufuli aliwafia, lakini hakuna miongoni mwao aliyekuwa na madaraka kikatiba ya kutangaza kifo chake, kumzika, au kuchukua nafasi yake.

Cc Nguruvi3, Kiranga
 
Magufuli ndiye aliyeagiza makamu wake asiwe karibu naye wakati anaumwa.

Haiyumkiniki rais anaumwa, mpaka anaita paroko, mpaka anaita kardinali, lakini hajamuita makamu wake.

Unafikiri Magufuli angesema nileteeni Samia hapa, kuna mtu angepinga?
 
Magufuli ndiye aliyeagiza makamu wake asiwe karibu naye wakati anaumwa.

Haiyumkiniki rais anaumwa, moaka anaita paroko, mpaka anaita kardinali, lakini hajamuita makamu wake.

Unafikiri Magufuli angesema nileteeni Samia hapa, kuna mtu angepinga?

..Yap!

..Yaani Samia kaenda Nairobi Hospital kumjulia hali Tundu Lissu, lakini akashindwa kwenda Mzena kumpa pole Magufuli?!

..Nadhani Rais na Makamu wake walikuwa kama paka na panya.
 
covid 19 bungeni na katiba ni mazoea ya kuvunja katiba tuendelee hivyo hivyo
 
kwamba wewe muelevu kuliko Magufuli?? angefanya ivyo kelele zingezida maradufu upinzani na ndani ya Chama, akapiga moyo konde mambo yaendelee.
 
Tama
duni na katiba vinaingilianaje???
 
Dah leo

Umenifungua,kumbe yule mama Mchembe alikuwa ni mke wa dactari wa Magu??? Mungu buana🤣🤣🤣🙏🙏
Huyu dc alipokuwa gairo alikuwa msumbufu sana

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…