Du tunafungwa mpaka na Somalia????? kweli mzee ruksa hakukosea
Yaani hii ni aibu ya hali ya juu. Tunafungwa na Somalia kweli nchi ambayo haina serikali na wanauana kila kukicha sijui hata kama timu yao ilikaa kambini!!! maana nchi nzima imejaa vita vya wenyewe kwa wenyewe!!! Duh! hatuna consistency yeyote katika uchezaji wetu maana tunaweza kufungwa na timu ambazo hazistahili hata kutufunga!!!! Wana kazi ngumu sana ya kuendelea na mashindano hayo maana inabidi washinde mechi zote walizobakisha tena kwa magoli mengi na timu nyingine nzuri kwenye kundi lao kufanya vibaya. Yaani mimi nilidhani tutavuna kapu la magoli kumbe bado ni kichwa cha mwendawazimu!!!!!
Kwani Tanzania tuna serikali?
Usizungumzie kufungwa mpira tu, mbona wanatuzidi hata kiuchumi kwania wana pato la taifa kubwa kuliko sisii. Unataka nikukumbushe zile takwimu?
Tuache siasa mkuu,yani una maana sisi ni masikini zaidi ya Somalia?Kwa data zipi hizo?GDP?
Embu leta data mkuu mimi siamini hilo!!
Somali 1 - Tanzania 0, hii nimeona Dullonet Tanzania | Just Call it Real Solutions for News and Informations. Tuna kazi bado, kushangilia timu zetu unaweza ujisababishie "Pressure" bure.
Usiwe na wasiwasi, kwa maneno halisi, hawatuzidi kwa uchumi: tunao kwenye grupu moja tu la umaskini, yaani hatuchekani. Wao ni wa pili kwa umaskini wakiwa na GDP ya $600 na sisi ni wa nane kwa umaskini tukiwa na GDP ya $800. Hata hivyo in reality ukipiga factor ya kuwa wao wamekuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 30 ukianzia na ile ya Ogaden mwaka 1977 hadi leo lakini kwenye mapato ya taifa tunawazid kwa dola 200 tu, ni kama vile wanatuzidi sana kiuchumi.

Tatizo liko wapi? tuliambiwa hili nchi iendelee inaitaji vitu 3, Siasa Safi, Uongozi bora na Ardhi. Sasa najiuliza kitu gani tulichokikosa mpaka sasa tuko fungu moja na Somalia katika uchumi mbovu?
Burundi 1 - Zambia 1
Sudan 1 - Djibouti 1
Kazi ni leo TZ tukipambana na ndugu zetu wa Zanzibar.