CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

Kwa mtindo huu basi Yanga na Simba huenda zitabebwa hadi fainali...
 
mkuu nimeboreka sana, sijui tukoje

Yanga ndivyo tulivyo

Tunatumia pesa nyingi sana kusajili lakini ukija kuangalia kinachofanyika uwanjani unashindwa kuelewa kabisa

Huku kwenye soka nako kuna virada vingi sana msimu wa usajili.
 
Sijui we unauzungumziaje,
dk 90 wamecheza wakatoka 0-0, ikaja zamu ya matuta, wakawatoa Red Sea kwa matuta 6 kwa 5 ingawa kuna malalamiko ya hapa na pale kwa mwamuzi kuzikataa penalt mbili zilizokoswa na Yanga kwa kisingizio wa Gkeeper kuondoka kwenye mstari wa goli kabla ya mpira kupigwa. Vipi we mwana Jf, mpenda mpira wa kibongo, unauzungumziaje huu ushindi?
 
Ha ha haaaaaa iwe mbeleko ya bati au chuma, tumeshinda leo halafu refa ni Mkenya si Mtanzania kipa anatoka golini mnategemea nini? Ile aliyookoa alitoka sasa Refa ili kubalance akatumia hii ambayo hakutoka Good refariii! Thank you Timbe ni kocha wa ajabu. Hivyo hivyo mpaka kombe linabaki!
 
Jamaa anaua kipaji cha dogo kwa kumuweka bench (tegete)
 
Kwa mtindo huu basi Yanga na Simba huenda zitabebwa hadi fainali...

ndio manake, musonye pamoja na kuiporomoshea yanga matusi mwaka juzi walipokimbia mechi ya simba lakini alivyoona mashindano yako bongo akageuka nyuma.

akawasifia mashabiki wa tanzania kwa kujaa uwanjani, tena inasemekana yeye ndo aliwashawishi viongozi wa yanga waandike barua ya kuomba msamaha ili yaishe na wao wajipatie kipato.
 
Nakubaliana nawe lakini siamini kama TIMBE ni kocha wa ajabu!! Labda usema CECAFA ni ya ajabu......
 
mkuu nimeboreka sana, sijui tukoje

Tatizo ni mfumo anaoutumia Sam TIMBE,hauruhusu mashambulizi......Anachezesha mabeki wawili wa kulia(Shadrack Nsajigwa na Godfrey Taita) kwa lengo la kuwachanganya wapinzani wake badala yake anaichanganya timu yake na kudhoofisha mashambulizi....

Pia anawatumia wachezaji wageni zaidi aliowasajili kwa ajili ya msimu ujao na kuwaacha wa zamani benchi,wachezaji hawa wageni bado hawajaelewana.......Na hili ni kosa ambalo hata Basena wa Simba alikuwa akilifanya kabla ya kubadilisha timu mechi ya jana na Bunamwaya...

Hakuna umuhimu wowote wa kuwaweka benchi wachezaji kama Jerry Tegete,Godfrey Bonny na wengine na kuwachezesha wachezaji kama Keneth Asamoah na Julius Mrope ambao ndi kwanza kawasajili na hawajacope mfumo wa timu.....

Anatakiwa abadilike......Nasikia kila siku anagombana na Fred Felix Minziro ktuokana na upangaji wake mbovu wa timu....
 
Tunaomba uzalendo wenu hiyo kesho.................

kwa yanga na simba hakuna kitu kinaitwa uzalendo, labda Mungu afanye miujiza vinginevyo stori ni zile zile

utawasikia tu baada ya muda mfupoi wanalipuka "uzalendo umetushinda"
 
Pooa ila wametutia mshawasha sana leoo Yanga hawa
usisahau pia kwamba mnyama alikiona cha mtema kuni kwa Red sea, lakini leo yanga wamekuja kidedea dhidi ya haohao Red c, Yanga hoyeeeeeeee!Berko, Nurdin hoyeeee!
 
ni ushindi mzuri. Wa kishujaa mkuu.
Red sea wasingeleta chalenge nzuri nusu fainali. Leo walikuwa wanazuia tu. Waliondoa radha ya ftball
 
Wacheni unazi ha WC kama kipa akicheza mpira haujapigwa penati hurudiwa

Ni kweli kabisa mkuu.......

Penati zote 2 kipa alianza kutoka kabla refa hajaruhusu ipigwe penati(alivuka msitari).....

Hata mimi niliamni Refa anawabeba Yanga lakini baada ya kuangalia Replay........Nimekubaliana na maamuzi ya refa
 
kwa yanga na simba hakuna kitu kinaitwa uzalendo, labda Mungu afanye miujiza vinginevyo stori ni zile zileutawasikia tu baada ya muda mfupoi wanalipuka "uzalendo umetushinda"
Nilisema mi jana nikaambia ' play your part'
 

Labda anawajaribu wachezaji wake wapya ili apate pattern ya kuwachezesha ingawa wanazi wa yanga tunataka kikombe mambo ya pattern ya mchezo/timu na formation yatakuja baadae kwenye ligi.

itabidi muwe wavumilivu kidogo, ngoja timbe aendelee kujipanga akivurunda nusu fainali ndo mumkalie kooni, sasahivi ni mapema mno.
 
Nakubaliana nawe lakini siamini kama TIMBE ni kocha wa ajabu!! Labda usema CECAFA ni ya ajabu......
Maajabu ya TIMBE labda ni ile hali ya timu yake kupata ushindi hata kama ni mbovu/inacheza hovyo....

Timbe ni mbishi sana hasa kwenye kupanga wachezaji gani waanze/wacheze na anagombana na msaidizi wake Minziro karibu kila siku....

Na kuna siku alimfukuza Tegete mazoezini kisa kachelewa kufika uwanjani.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…