Wakuu
Ngoja niongee ya kwangu pia.
Kwanza sijafurahia hata kidogo the way Yanga walivyofuzu semi final, lakin sina budi kuikubali maana imeshatokea.
Ukweli ni uungwana siku zote, najua wanazi wa Simba SC wataanza kuleta ubishi ili ionekane mechi ya leo Yanga alibebwa.
Ni kawaida kwa timu pinzani kuombea mabaya mwenzake, na kwa wengine watatetea hata uongo ili hayo mabaya waliyoomba yatimie na wapate cha kuongea. Ndio wanachofanya washabiki wa Simba sasa.
Red Sea pamoja na kuizuia Yanga isiwafunge kwenye dk 90, walionekana kutumia "Udogo wao" kushinikiza wanaonewa na maamuzi ya refa. Na uliona mambo yanaanza tangu kwenye kuchagua goli la kupigia penati. Replays zinaonyesha wazi wazi kipa alikuwa akitoka golini kabla ya penati kupigwa, na kama vile haitoshi kibendera kilikuwa juu hata kabla ya penati kupigwa.
Kumalizia tu niseme, Red Sea haikuwa na uwezo wa kuitoa Yanga hata kidogo. Mpira waliocheza unaonyesha kila kitu. Walikuwa wanachelewesha sana mpira, wanajiangusha sana, na hata staili yao ya kupaki basi nyuma ilionyesha walijiandaa kulinda goli tu. Sijaona shuti hata moja walilopiga hawa Red Sea kipindi cha pili.
Tukubaliane tu kwamba Yanga hawakucheza vizuri kabisa leo, wariboronga sana, na vile vile Red Sea hawakuwa na uwezo wowote wa kuifunga Yanga. Mechi ilichezeshwa kwa haki kabisa, sema tu ushindi wa Yanga kuitoa Red Sea kwa njia hii ni aibu kwa Yanga. Lakin wameshinda kihalali kabisa.